Miss Tourism Tanzania Organisation yatufa leseni ya waandaaji wa Miss Utalii Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miss Tourism Tanzania Organisation yatufa leseni ya waandaaji wa Miss Utalii Dodoma

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yericko Nyerere, Nov 26, 2011.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  Nov 26, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,250
  Likes Received: 3,857
  Trophy Points: 280
  26/11/2011

  *

  Bodi ya wakurugenzi ya*Miss*Tourism*Tanzania*Organisation, wenye dhima ya kikomo ya kuandaa mashindano ya*Miss*Utalii Tanzania, imewafutia leseni waandaaji wa*Miss*Utalii Mkoa wa Dodoma, na kuwapiga marufuku kujihusisha na mashindano hayo kwa namna yoyote mwaka mmoja.

  Hatua hiyo imekuja baada ya uchunguzi uliofanywa kubaini mapungufu makubwa katika shindano la*Miss*Utalii Dodoma 2011/12 lililo fanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Club La Aziz Dodoma.

  Mapungufu hayo ni pamoja na kushindwa kuingia mikataba ya maandishi na wadhamini mbalimbali walio semekana na kutangazwa kuwa ni wadhamini wa shindano hilo, zikiwemo kampuni za Peter Fashion na Ngoto Furniture za mkoani Dodoma, ambazo baada ya shindano hilo zilikana kuingia Makubaliano, na kutoa ahadi walizo toa hata mbale ya waandishi wa habari wakati wa ziara za washiriki katika makampuni hayo na waandaaji wa shindano hilo la*Miss*Utalii Dodoma 2011/12.

  Mapungufu mengine ni pamoja na kuruhusu Baadhi ya majaji kutumia pombe wakati wa kazi ya ujaji na wengine kuruhusiwa kuwa majaji wakiwa wamelewa, hivyo* kutaka kukiuka kwa taratibu na kanuni za mashindano za kupatikana kwa washindi kwa njia za haki, hali iliyo sababisha kutokuelewana baina yao na kufanya vurugu, ambapo hata rais wa mashindano hayo alipo itwa katika meza ya majaji ilikutoa ufafanuzi na mwongozo wa kikanuni na taratibu za mashindano walimvaa na kumfanyia vurugu, hivyo kuhatarisha amani hadi jeshi la polisi Dodoma lilipoingilia kati na kusimamia maamuzi ya majaji wengi na ya haki kutangazwa .

  Bodi imeridhika kuwa kulikuwa na hisia na ushahidi wa kimazingira wa mahusiano ya karibu baina ya washiriki na Baadhi ya wadhamini, majaji na hata Baadhi ya wajumbe wa kamati ya*Miss*Utalii Dodoma, jambo ambalo ni kinyume na maadili, kanuni na taratibu za mashindano.

  Mapungufu mengine yaliyo bainika, washiriki karibu wote kudanganya kiwango cha elimu hivyo kutokuwa na sifa ya kushiriki shindano hilo kwa mujibu wa kanuni, sifa hizo ni pamoja na washiriki kutokuwa na elimu ya kidato cha sita au yenye kulingana nayo, kwani karibu washiriki wote walikuwa na elimu ya kidato cha nne au chini ya hapo.*

  Bodi inakamilisha taratibu za kuwavua mataji washindi wote na hadhi ya ushiriki washiriki wote ambao hawakuwa na sifa za kushiriki mashindano haya kwa mujibu wa kanuni na taratibu za mashindano, hivyo nafasi za washindi zitapewa washiriki walio na sifa za kushiriki mashindano haya.

  Kwa mujibu wa taratibu za mashindano haya, washiriki wote hugharamiwa na waandaaji gharama zote za kushiriki tangu mavazi, Saluni, Vipodozi, usafiri, chakula na malazi wakati wote wa mashindano na mazoezi.

  Washiriki wote wa*Miss*Utalii Dodoma 2011/12 waligharamiwa kila kitu, hivyo wale walio ongopa wanapaswa kurudisha gharama za waandaaji, lakini bodi imeamua kuwa wasidaiwe gharama hizo kwani kulikuwa na uzembe miongoni mwa waandaaji na uongozi wa*Miss*Utalii Dodoma 2011/12.

  Katika shindano hilo, mshindi alizawadiwa zawadi yenye thamini ya sh. 1,670,000/= ikijumuisha nafasi ya Kusoma Chuo cha Dar City Collage kozi yenye thamini ya sh. 1, 600,000/= pamoja na vitu vingine vyenye thamini ya shilingi 70,000/=, mshindi wa pili alizawadiwa zawadi yenye thamini ya Sh . 1,650,000/= ikijumuisha kozi katika chuo cha Dar City Collage na vitu vingine vyenye thamini ya sh.500, 000/=, mashindi wa tatu alizawadiwa zawadi yenye thamini ya Sh. 1,640,000/= ikiwemo kozi katika chuo cha Dar city collage na vitu vingine vye thamini ya sh. 40,000/=, mshindi wa 1-5 na wa Vipaji kila mmoja alizawadiwa yenye thamini ya sh.1,620,000/= ikiwemo kozi Dar City Collage na sh.20,000/= Taslimu, waliobaki walipata vifuta jasho vyenye thamini ya sh.20,000/= kila mmoja.

  Waandaaji wa*Miss*Utalii Dodoma 2011/12 walikuwa ni Gabriel C.Mashayo, Zaina Allen, Adrinai Laswai na Said Mungele.*Wakati huohuo, baada ya kuvunja uongozi wa Dodoma, bodi ya Taifa ya*Miss*Tourism*Tanzania*Organisation imemteua mfanyabiashara maarufu wa maduka ya Mitindo na saluni za kike Dodoma. Salama Selemani Mgogo kuwa Mkurugenzi wa*Miss*Tourism Organisation Kanda ya Kati kuanzaia 1-11-2011.

  *Aidha shindano la kumpata*Miss*Utalii Vyuo Vikuu 2011/12 kanda ya kati limepangwa kufanyika siku ya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru 9-12-2011 mkoani Dodoma na kushirikisha vyuo vyote vya mikoa ya kanda ya kati.

  Asante,
  Gideon Erasto Chipungahelo
  Rais*Miss*Tourism*Tanzania*Organisation
   
Loading...