Miss Tanzania siku hizi inafanyika kwa siri ?

Cashman

JF-Expert Member
Jun 8, 2018
2,271
3,925
Nimeona leo baadhi ya watu wakituma picha za kuonesha mashindano yamefanyika jana na kupatikana mshindi.

Napenda kujua tu,je shindano hilo linafanyika kwa siri?
Nimeuliza hivi kwa kuwa zamani tuliona matangazo mengi,na wakifanya vipindi kadhaa kwenye vituo tunavyoangalia wengi hata tukiwa safari kama vile TBC,Clouds,ITV na Star TV.
Nakiri mwaka huu na sikumbuki hata mwaka jana kama yalifanyika.

Je kuna masharti yaliwekwa ama waandaaji walibadilika?Ama yamemilikiwa na watu wa ving'amuzi?
 
YALIRUSHWA KUPITIA STARTIMES... ST BONGO CHANNEL
 
Wanaoyaendesha hayo mashindano wabahili na wanataka faida kubwa wale peke yao.

Kufanya promo hawawezi na hawataki kuwapa watu kazi wafanye promo wagawane nao faida.

Jaribu kuwaza miss Tanzania promo deal angepewa diamond na wasafi yake ile.
 
Back
Top Bottom