Miss Tanzania na maswali ya papo kwa papo

crome20

JF-Expert Member
Feb 5, 2010
1,130
721
Naomba tutoe ushauri kwa kamati ya MISS TANZANIA kuhusu kipengele muhimu cha ufahamu kwa jinsi ya kujibu maswali kuliko aibu tuliyoipata Jmosi usiku.
Fikiria mrembo anaulizwa utatumiaje Taji lako katika kupambana na tatizo sugu la madawa ya kulevya na HIV, anasema ( TENA KWA KISWAHILI) nitawaomba mwaswala hayo yaishe!! How?

Kakolaki ambaye alionekana angeibuka kidedea, kapata swali rahisi. Kaulizwa utafanyanye kukuza utalii Tz, akaanza kuzunguka kwa kutaja vivutio, ok jibu swali sasa, anasema nitashirikiana na tume ya utalii kutoa elimu kwa watanzania, basi. Ni swali ambalo angeenda mbali zaidi kwa kutoa plan ya elimu, kwa mbinu gani hasa kutumia taji la Miss VodacomTz, na je utalii wa njeitakuwaje, tena kwa kiswahili alichochagua angetiririka vya kutosha kuliko kutoa sentensi moja. Nilivyokuwa nimekasirika hata Miss wetu cjui aliulizwa nini na akajibu nini.

Mie ushauri wangu, ni kuwa warembo waandaliwe makongamano makubwa angalau mawili kabla ya fainali na yawe laiv na kila mmoja apewe topic ya kuwakilisha ( presentation) ili kuwajengea confidence ya public presentation. Ninaamini kamati ina wataalamu wa kufundisha public presentation.

...Hio kamati yenyewe ya Miss Tanzania mie tangu nimezaliwa nimeikuta inaendeshwa na mtu yuleyule/walewale, Hashim Lundenga na wenzie unategemea kuna jipya hapo??!!. Mawazo mgando, mipango mgando, kila kitu mgando.
Nchi hii kila mtu anakula katika nafasi yake aliyonayo.

ni kweli yaani kwa ujumla wote hawakujibu maswali jinsi yalivotakiwa,yaani inaonyesha maswali yote walikuwa wanayajua na walichofanya ni kukremisha majibu na sio kujibu kwa ufahamu wao.ufahamu mdogo hata kwenye lugha yao ya kuzaliwa.....aibu na hao kina hashim lundega ni walewale watu wenye kung'ang'ania mambo hata kama hayaleti faida kwa taifa miaka yooote hakuna jipya zaidi ya kubadlisha aina ya magari.

Mh mh maswali yalikua mazuri sana tena kama lile la vita ndio kabisa unajibu vizuri hadi unapigiwa ngengele, sasa nashangaa hao ma miss walikua wanakimbilia wapi hadi washindwe kujibu maswali!sasa kama hata huwezi kuongelea kuhusu namna ya kuzuia vita katika nchi utakuaje ambassador!! they are day dreamers

...Hio kamati yenyewe ya Miss Tanzania mie tangu nimezaliwa nimeikuta inaendeshwa na mtu yuleyule/walewale, Hashim Lundenga na wenzie unategemea kuna jipya hapo??!!. Mawazo mgando, mipango mgando, kila kitu mgando.

Nchi hii kila mtu anakula katika nafasi yake aliyonayo.

Heri umeliona hilo maana mwandahaji mwenyewe shule zero unategemea nni hpo,c utumbo mtupu bwn lundega achana na kazi hyo muda wko umekwisha.

mashindano yenyewe yamebakia jina tu ambalo nalo linaenda kaburini!! sasa hakuna haja ya kuweka warembo kambini, siku ya tukio wanaita mnawapa gari basi...... nadhani itasaidia kupunguza gharama za kutengeneza vituko!

Nilipata hasira zaidi kwa majibu ya ovyo yaliyotolewa na wale mabinti, kwa kweli niliyategemea ila not to that extent! Kilichonifurahisha ni kusikia baadhi ya mashabiki wakishangilia majibu yaliyokuwa yanatolewa, nikajiuliza hivi ushabiki unaweza kuvuruga uelewa wetu kwa kiwango kile?

Haki ya mungu kama kuna siku nilichukia ni usiku wa juzi ile. Sijui waziri atakapokuwa anakabidhi bendera ili mwakilishi wetu aende huko miss world atamwambia nini. Pale kwa watu ambao wana uwezo wa kuhesabu moja hadi tano bila kushika vidole wanajua tu kuwa hao mamis na miss wao mkuu hashim watakwenda tu kutalii na wala si kushiriki.

lakini cha kushangaza kuliko vyote, pale nilisikia mamis wakijitambulisha kutoka UDSM, Open University na ustawi wa jamii. hivi jamani hata huko nako ndo kumebaki kweupe hivyo? This is too much for this country totally unbearable!. mtu anaulizwa kuhusu masuala ya kijamii, katoa utumbo wa definitiion ya culture aliyokariri, wa amani nae ndo kama tuluvyojione, na hiyo aibu ya madawa ya kulevya ndo sitaki hata kukumbuka. we need something else jamani kuliko mchefuko ule.

Hivi huwa mnaenda kufanya nini huko miss Tz. Huko warembo wameenda kuuza sura ili waongeze soko. Is that really hard to understand???!! Mimi nadhani ninyi mnaoshangaa ndio vilaza kwelikweli maana madhumuni ya hayo mashindani kwa hawa wadada yako wazi kama mchana halafu bado mnalalamika, mnaboooooooooa kwakweli.

ah aise miss Tanzania. kusema kweli mi nataka nizungumzie mavaz yan ni uzalilishaj wa hali juu. wantanzania mulete mabadiliko chanya sio has munatumalizia nguvu za kiume banaa

Hivi huwa mnaenda kufanya nini huko miss Tz. Huko warembo wameenda kuuza sura ili waongeze soko. Is that really hard to understand???!! Mimi nadhani ninyi mnaoshangaa ndio vilaza kwelikweli maana madhumuni ya hayo mashindani kwa hawa wadada yako wazi kama mchana halafu bado mnalalamika, mnaboooooooooa kwakweli.

No Mjasiria, Mashindano hayo kama yatachukuliwa kwa mantiki yenyewe ni mazuri maana vigezo vingi vinatumika kumpata mrembo. Tatizo letu ni uendashaji wenyewe wa akina Lundenga. Usifananishe ya kina Wema Sepetu maana wapo warembo walioiletea heshima tZ, wanaojiheshimu na kuheshimika katika jamii. Nakubali hoja yako kuwa mashindano ya urembo yanawaongezea soko dada zetu kama ilivyo kwa msichana kwenda shule kunavyomuongezea soko, hivyo huwezi kusema wasichana wanahangaika kusoma kwa kuwa kuwa vyuoni ni kuuza sura ili kuongeza soko, no.

Ikumbukwe kuwa mashindano hayo ni ajira pia maana kuna wengine wekuwa sponsored kusoma, na kuajiriwa katika makampuni makubwa. Ni kama ilivyo kwa BSS, Tusker project fame n.k. Kinachotakiwa ni kuwa wabunifu, kuwa na recruitment nzuri,kuweka sheria kali kwa wanaokiuka maadili, wawe washiriki au waandaaji ili yawe na heshima.

Aah. Mamis. Mimi naona siku zote tutakuwa wasindikizaji ji huko miss world .

Kwanza hatujikubali uhalisia wetu yaani tukienda na nywele zetu naona ndio tunaweza kushinda.
lakini kama mawigi au manywele ya bandia na maenjofesi ndio yakayo kuwa yanaenda huko katu hatutashinda.

Tatu ufahamu mdogo yaani ni kukariri tu akiongeza na zigo la mawigi kichwani basi anaelemewa anashindwa kujieleza kabisa, wakati kule kwenye miss world pamoja na mambo mengine wanacheza sana na kichwa cha mtu (ufahamu na uelewa wa mambo mbalimbali)

Acha tu wakatalii wasijekosa cha kusimulia kuwa na mimi nimepanda ndege nimeenda mpaka uingereza.

Rubi kwa kweli hii tasnia imekuboa mpaka...

Back
Top Bottom