Miss Tanzania hoi tena

Sokomoko

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,915
127
SANYA, China
MREMBO wa Tanzania, Genevive Mpangala ameshindwa kutamba katika mashindano yote pamoja na kuchaguliwa kuingia kwenye orodha ya washiriki 22 walioshindania Miss World Talent 2010.

Mshindi wa mrembo wenye kipaji alikuwa Emma Britt Waldron wa Ireland akiwa ni mshiriki wa nne kupata nafasi ya kuingia moja kwa moja kwenye hatua ya nusu fainali ya Miss World 2010.

Emma Britt Waldron alishinda baada ya kuwashinda warembo Belarus, Canada, Cyprus, Guadeloupe, Ireland, Korea, Malta, St. Lucia, Venezuela, Wales, Canada na Korea.

Mwingine aliyepata nafasi ya kuingia nusu fainali ya moja kwa moja ni mrembo wa Norway, Mariann Birkedal aliyeshinda Miss World Top Model 2010 ambaye aliwashinda warembo wa Argentina, Belgium, Botswana, Jamhuri ya China, Ethiopia, French Polynesia, Ghana, India, Norway, Russia, St. Lucia, Slovakia, Afrika Kusini, Hispania, Sweden, Thailand, Venezuela, Ukraine, Marekani na Zimbabwe.

Pia mrembo wa Ireland ya Kaskazini, Lori Moore alishinda tuzo ya Miss World Sportswoman 2010 na kupata nafasi ya kuingia nusu fainali moja moja kwa moja baada ya kuwashinda warembo wa Australia, Cayman Islands, Botswana, Brazil, Canada, Finland, Guyana, Ireland, Hungary, Iceland, Mongolia, Paraguay, Martinique, Ireland Kaskazini, Norway, Slovakia, St. Kitts and Nevis, United States Virgin Islands, Uturuki na Wales.

Katika mashindano ya Miss World Beach Beauty 2010 mshindi alikuwa Yara Liz Lasanta Santiago wa Peru ambaye pia amepata nafasi ya kushiriki nusu fainali ya mashindano ya Miss World Beach Beauty 2010.

Waandaaji wa Miss World wameanzisha mashindano ya mpira wa wavu ambayo yalianza juzi kwa warembo wanaowania taji hilo la dunia kushindana.

Mechi ya ufunguzi ya mashindano hayo ilichezwa kati ya timu ya China dhidi ya Uingereza, ambapo warembo wa Brazil, Bolivia, Cayman Islands, Costa Rica, Kenya, Malawi, Panama, Peru, Philippines, Slovakia, Uturuki na Uganda pia walihudhuria.

Wakati huo huo, washindi wa zamani Miss World wameingia nchini China kwa ajili ya kusaidia kuchagua mshindi wa Miss World 2010 katika fainali ya mashindano hayo inayotarajiwa kufanyika Jumamosi Oktoba 30 mjini Sanya, China.

Washindi hao wa zamani ni Denise Perrier Lanfranchi wa 1953,Ann Sidney wa 1964, Mary Stavin wa 1977, AgbaniDarego wa 2001, Maria Julia Mantilla wa 2004, Zhang Xi Lin wa 2007 na Ksenia Sukhinova 2008.

Source: mwananchi
 
Sishangai. Mashindano ya mwaka huu hayakuwa na warembo wa quality.

Kwa ujumla fani ya urembo TZ bado ni changa sana; kuanzia kuwepo na mtazamo hasi katika jamii kuwa mashindano ya urembo ni uhuni, recruitment ya suitable applicants inafanyika kiholela, maandalizi duni ya washiriki etc. Hata ukiangalia uendeshwaji wa mashindano yenyewe - mambo ni yaleyale miaka yote, hii inamaanisha waandaaji hawajifunzi na hawako innovative. Focus kubwa inawekwa katika zawadi za washindi. Wanasahau motivation ya wasichana wazuri na intelligent sio zawadi (gari) tu bali future prospects watakazozipata kwa kushiriki.
 
sisi huwa tunawapeleka hawa mamiss kule kutimiza wajibu tu, jitihada za kutosha zinahitajika ili tuweze kuwa kwenye top list kama wenzetu walivyo,
 
Lundenga yuko kibiashara zaidi hana mpango wowote wa kuiboresha anachoangalia nii atapata yeye kama yeye shiligi ngapi ili maisha yasonge mbele,juhudi na creativity ya kuifanya Tanzania siku moja ing'ae hana mpango huo,ubabaishaji tu Tanzanians tutafika?
 
Back
Top Bottom