Miss Tanzania - By Solo Thang: Wimbo bora wa Hiphop Bongo

KIMAROO

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
453
258
Baba yake alikuwa mkoloni kipindi huyu Miss mwali
Mchonga alikata utepe lakini hakuvinjari
Sababu alikua busy kumlinda na geti kali
Kumbe wenzake wanabinjuka, kushtuka akakaa mbali

Demu alikua na heshima kabla haijatangazwa Rukhsa
Chukua Chako Mapema ukimkonyeza tu umegusa
Ana kifua kimebetuka sio maziwa ni madini
Kayaacha wazi, watu wanashika hapo ndio anaponiudhi mimi

Watu wanagonga tu Ikulu tena kwa mitindo huru
Kavu kavu bila kinga hajali vinavyodhuru
Kawa shangingi na amedata hana uwoga wa kunguru
Anapenda sana chapaa haimtoshi kodi na ushuru

Ana kijungu matata laini kama nyanya masalo
Anatingisha Afrika nzima na mzigo Kilimanjaro

Usimchezee kwa vidani sio pete sio hereni
Anamiliki Tanzanite kama ardhi ya Mererani

Sura dhahabu inaita kama amezaliwa Geita
Tatizo ndio kicheche kila mwanaume ndio amepita
Hata Benja hakutoka Kapa huyu demu hajatulia
Kama rushwa ndio kikwapa ananuka na kunukia


[Kiitikio]
Miss Tanzania
Nakupenda ila hujatuliaa
Vitendo vyako sitojivunia
Sifa yako kubwa umefulia
Miss Tanzania


[Ubeti wa Pili]
Bora angebaki kuwa modo kama Flavian Matata
Ila demu amejiachia kisa anaendekeza bata

Sitachoka kuwakilisha jinsi anavyoniacha hoi
Juzi juzi kaopolewa na Handsome Boy

Kabla hapo shoga zake wote kashawaona mabwege
Sababu hawana dira na yeye ameshahongwa ndege

Anafaa kuwa Miss Dunia maandalizi longolongo
Tatizo anakula sana akijamba ni Songosongo

Mara ghafla kanenepa kumbe mimba B.O.T.
Kumbe demu aligawa EPA watu wamepiga hafu jii

Alizugwa na akaunti hewa kuwadi Bwana Bilal
Mara mdomo naye kazimwa bila hata picha ya kaburi
Kinachomponza huyu shawty utulivu sifuri
Ila hakuna anayepinga kwamba huyu demu ni mzuri

Mixer siasa na biashara demu ameshakuwa chotara
Mishe za Dar akimaliza Mjengoni anakwenda lala
Kadri miaka inavyokwenda demu anazidi fulia
Kumbe weupe ni mkorogo ona mwili sasa umefifia

Demu kazidi umalaya wacha mabwana wamteme
Haogopi kuliwa mtungo kisa anagawa umeme


[Kiitikio]

[Ubeti wa Tatu]

Wadaku walishamfuma anakula denda na Richmond
Dowans akazidi kete akamvisha pete ya diamond

Binti masikini akanasa bwana mshenga ndio Lowasa
Shemeji hataki hata picha ndio tabia gani sasa
Ndoa ilifungwa kwa vifijo vigogo wakala pizza
Keki nzima wale wao share yetu si ni giza
Sio hayo demu ana mengi ya kuchukiza
Malighafi ashazinadi for sale anajiuza

Mtaani ilivuma rumor demu kawa mama huruma
Uchumi umefungwa drip maendeleo ndio kali homa

Mali asili ndio kitasa kila ufunguo ndio unapita
Toka alipovunja ungo nusu karne imeshapita

Mapenzi kafanya mradi anamegwa na mafisadi
Amani kwa time bomb binti amekumbatia radi

Vitendo vyake vibaya vinafanya adharaulike
Tabia Katiba sio Msahafu ndio useme isibadilike

Mikosi inayomkuta ndio kwanza anatabasamu
Hajali waliomzunguka kama nao binaadamu

Mbagala walimbaka mpaka akamwaga damu
Na juzi Gongo la Mboto kaanza kujamba mabomu


[Kiitikio]
 
Yaah jamaa ni mkali kazungumzia vitu vya kawaida kwa style ambayo sio ya kawaida
 
Hizi ndo tungo mtu katulia sio zao zile za kusifia ngono na pombe kisha wanajisifia"mwanangu nimetunga bonge la pili subiri nikusikilizishe"
 
Really jamaa ameandika mambo makubwa katika uhalisia wa nyimbo moja tu kama IQ yako ndogo haumuelewi.
 
Huu wimbo mara ya kwanza kuuelewa niliishia kutabasamu tu.
 
mwana ulamaa huyo wa mbagala,hivi tuzo za kili zinavigezo gani hadi ma Great Thinker kama huyu wakose!,yaani Tz kuanzia uongozi mchongo,siasa mchongo,michezo mchongo hadi tasnia ya mziki nayo watu wamejimirikisha.,,kha wanarudisha nyuma juhudi za wasanii chipukizi kama mo music non nominated upcoming artist@kill music awards,endeleeni kuua mziki.
 
mwana ulamaa huyo wa mbagala,hivi tuzo za kili zinavigezo gani hadi ma Great Thinker kama huyu wakose!,yaani Tz kuanzia uongozi mchongo,siasa mchongo,michezo mchongo hadi tasnia ya mziki nayo watu wamejimirikisha.,,kha wanarudisha nyuma juhudi za wasanii chipukizi kama mo music non nominated upcoming artist@kill music awards,endeleeni kuua mziki.

Alivyochoka na longolongo za hawa wagawa tunzo aliwaimbia wimbo wa GUNDU ft Q- Chilla
 
Alivyochoka na longolongo za hawa wagawa tunzo aliwaimbia wimbo wa GUNDU ft Q- Chilla

umeona Mkuu,bila hongo autambi kimziki,nahisi kutokuwa karibu na redio fulani ya mzee Kukoboa maana naona yeye ndo basata na kila kitu kinachohusu mziki bongo,akiwa na kijana wake mtendaji mutahaba
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom