Miss Tanzania afutiwa mashitaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miss Tanzania afutiwa mashitaka

Discussion in 'Celebrities Forum' started by ngoshwe, Apr 22, 2010.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Miss Tanzania afutiwa mashitaka
  [​IMG]
  Mrembo wa Tanzania, Miriam Gerald

  MAHAKAMA ya Wilaya Kinondoni, imemfutia mashitaka Mrembo wa Tanzania, Miriam Gerald, baada ya mlalamikaji kuiambia mahakama kuwa hana mpango wa kuendelea na kesi aliyofungua.

  Miriam pamoja na rafiki yake wa kiume, Kennedy Victor wamefutiwa mashitaka yaliyokuwa yanawakabili ya kumshambulia Shaaban Moshi kwa vitu vyenye ncha kali wakati shitaka la pili, ni kufanya uharibifu wa mali yenye thamani ya Sh720,000.

  Hakimu waliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Kwey Lusemwa aliwaambia washtakiwa kuwa wako huru baada ya mlalamikaji kuonyesha kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo.

  Awali, Mwendesha Mashtaka Mrakibu wa Polisi, David Mafwimbo alisema mahakamani hapo kuwa mlalamikaji ametoa taarifa ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi na akaagiza iondolewe.

  Mrembo huyo alitwaa taji hilo, Oktoba 2, 2009 kwenye Ukumbi wa Mlimani City lakini alifanya vibaya kwenye mashindano ya dunia yaliyofanyika Afrika Kusini mwishoni mwa mwaka jana.

  Akizungumza jana, Mratibu wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga alisema: "Niliwaambia Watanzania tuiachie mahakama ifanya kazi yake na leo hii ukweli umeonekana.

  "Mimi siamini kama hili lilikuwa na ukweli ndani yake, ni mambo ya kupandikiza lakini tuyaache imeshaamriwa hivyo...," alisema Lundenga.

  "Watu wanahukumu Miss Tanzania, lakini sivyo, sisi tunakaa na warembo muda mfupi sana, akitwaa taji, tunamtumia pale tunapomuhitaji na baada ya hapo anaendelea na maisha yake hatuwezi kumbana muda wote, sasa ni akili za wao wenyewe wajitambue nafasi yao.

  Lundenga ambaye alirejea kuwataka radhi mashabiki wa urembo, aliwataka warembo kujitambua nafasi yao badala ya kufanya mambo yasiyokuwa na maana na kuharibu taswira nzima ya mashindano ya urembo.
  http://www.mwananchi.co.tz/michezo/18-michezo-mingine/927-miss-tanzania-afutiwa-mashitaka
   
 2. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,951
  Trophy Points: 280
  lundenga anaongea UPUUZI PLUS...mshitaki "ameamua" kuwasamehe yeye anaropoka kuwa mahakama imefanya maamuzi yake....sie tunataka kujua kwa nini wameamua kuyamaliza kiaina nje ya mahakama...waerevu tunajua kuwa mumemlipa mlalamikaji plus kumtongoza kwa vijirushwa ili afute kesi na fani yenu "chafu" ya urembo iendelee maana muda sio mrefu mtaanza kumtafuta mrithi wa miss wenu 'mchafu wa maadili ya kitanzania".....

  Lundenga bana usitake kutufanya watanzania wototo ni "wapuuzi na mindondocha" ya kukubali uongo wako kirahisi namna hiyo.....nakuomba na kukushauri pia yafuatayo kama kweli unayo nia ya dhati ya kuwatafutia watanzania mrembo sahihi na wa ukweli.

  1- Wewe na kamati yako "mujisafishe" ili muweze kutuletea miss tanzania msafi..na sio matunda ya uchafu wenu wana kamati

  2-Safisheni kuanzia ngazi ya chini ya vitongoji ili dada na wajomba zetu ma-miss wa ukweli wa kitanzania waweze kushiriki katika kinyanganyiro cha kumpata miss tanzania wa "ukweli"

  3- wekeni masharti magumu kwa hawa ma-miss wanaopatikana..skendo yeyote itakayohusu maisha yake akiwa kama miss tanzania inatosha kumvua taji maramoja bila kujadiliwa...miss ni kioo cha jamii anatakiwa awe "MSAFI SANA"..kama pesa mpya.

  Naamini Lundenga haya nilokushauri ni magumu sana kwenu "KUTEKELEZEKA" maana "uchafu" umekuwa sehemu ya maisha yenu waandaji wa miss tzania ili muweze kukuza vipato vyenu na familia yenu...kaa chini tafakari uzito wa hayo nilosema kisha "uamue" maamuzi magumu kadiri ya kipimo chako na heshima ya taifa kwa ujumla.

  NI MAONI TUU YALOJAA HISIA ZA UTHAMINI WA MTANZANIA HALISI
   
 3. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  mlalamikaji keshahongwa na washika dau wa miss TZ so wameamua kuitupilia mbali kesi hiyo....
   
 4. I

  Irizar JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2010
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 217
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Lundenga yote hiyo ni FIX tuu, huyu Miriam alitakwa na Pedeshee Papa Msofe, basi alipomkataa ndiyo akahakikisha anakwenda kunyea ndoo huko Segerea, na Lundenga anayajuwa yoteeeeee haya.
  Hawa wasichana hawawezi kuwa wazuri kwa sababu kamati ya Miss Tanzania inachaguwa cheap, cheap,cheap girIs, ambao wanaweza kulala nao yaani kufanya nao matusi.
  Wale wasichana wenye akili timamu wanaokataa kulala na akina Lundenga na wenzake mara nyingi huwa hawapewi ushindi.
  Nilishangaa sana mwaka mwaka huu Miss Talent alikuwa mkata viuno vya taarabu, na msichana aliyefanya bonge la talent show aliyetoa ujumbe mzuri kwa jamii wala hakupata ushindi, kweli nikaamini kwa macho yangu, maana hata mimi siku hiyo nilikuwepo hapo Giraffee Hotel, kwa kweli niliona kila kitu. Na nilisikitika sana, sana. Mimi binafsi ni mpenzi na mdau sana wa Miss Tanzania, ila mambo ya Lundenga yananichafuwa sana roho yangu.

  Tutafanikiwa kimataifa kama tu Lundenga akiaacha ujinga wake wa kutembea na watoto wa watu. Au Tanzania imunyanganye hii kazi ya Miss Tanzania.
   
 5. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,951
  Trophy Points: 280
  sasa si ndio mie namshangaa lundenga anavyosema "mahakama imetoa maamuzi"....miss tanzania na lundenga wake wanalinda maslahi yao maana wadhamini walikuwa wawapige chini "wakalime mwani" na ndio kuwadi lundenga angelijua jiji na mipaka yake
   
 6. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  Hii miss Tanzania haina mvuto kuisikia sasa..maadiri yameshaporomoka
   
 7. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Wadau hebu tufikirishe hii habari kuwa mujibu wa link iloonyeshwa. binafsi naiona nia hatua ambayo ,japo ni njema IMECHELEWA kutekelzzwa.. laiti ingetekelezwa tangu enzi za marehemu baba wa taifa.. Leo hii Tanzania ingekuwa na uwezo wa kukabiliana nchangamoto nyingi zinazotukabili kiuchumi..kijamii.. kielimu...na kimaadili


  Kiswahili kutumika rasmi serikalini
  Imeandikwa na Na Shadrack Sagati, Dodoma; Tarehe: 19th April 2010
  http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=6714

  SERIKALI imeagiza kutumika kwa Kiswahili katika usaili kwa watu wanaoomba kazi kwenye Wizara na Idara za Serikali na pia imetaka matangazo yote ya kazi za idara za umma yatolewe kwa lugha hiyo badala ya lugha ya kigeni kama inavyofanyika sasa hivi.

  Katika agizo hilo, pia serikali ambalo lilitolewa jana na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika bungeni, imeagizwa dhifa mbalimbali za kitaifa, hotuba za viongozi, warsha, semina na mikutano ya kitaifa iendeshwe kwa Kiswahili.

  Pia alisema maofisa wa serikali na mashirika ya umma watumie Kiswahili katika shughuli zote kama vikao vya Bodi na mawasiliano ya kiofisi pia yaendeshwe kwa lugha hiyo ya taifa pamoja na kuandika madokezo.

  Pia aliagiza sheria zote ziandikwe kwa Kiswahili ikiwa ni pamoja na kutafsiri zile zilizoandikwa kwa lugha za kigeni. Alisema jitihada za makusudi zifanyike ili shughuli za Mahakama katika ngazi zote ziendeshwe kwa Kiswahili pia.

  Mijadala inayohusu shughuli za umma iendeshwe kwa Kiswahili na kumbukumbu zote zihifadhiwe kwa lugha ikiwa ni pamoja na nyaraka zilizotumika katika mijadala kuandikwa kwa Kiswahili. Waziri pia aliagiza majina ya barabara, mitaa na mabango yaandikwe kwa Kiswahili.

  Serikali imetoa kauli hiyo baada ya Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein katika kikao cha Baraza la Mawaziri Februari mwaka huu, aliagiza na kusisitiza suala la matumizi ya Kiswahili katika shughuli za serikali na kuwakumbusha watendaji serikalini kuzingatia Waraka wa Makamu wa Kwanza wa Rais, Rashidi Kawawa wa mwaka 1967.

  Mkuchika pia alisema mwaka 2005, Serikali kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera), William Lukuvi aliagiza taarifa za mikutano, semina na warsha nchini zitolewe kwa Kiswahili kwa manufaa ya wananchi.

  Alisema taarifa za miradi inayohusu wananchi ni lazima zitolewe kwa Kiswahili ikiwa ni pamoja na vipeperushi na nyaraka zinazohusu miradi hiyo.

  Mwaka 1974, aliyekuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais (Utumishi), J. Mganga alitoa waraka alioelezea kuhusu matumizi ya Kiswahili katika ofisi za serikali ambao ulisisitiza barua kati ya Wizara na Idara ziwe za Kiswahili isipokuwa kama anayeandikiwa ni raia wa kigeni.

  Pia aliagiza vibao vyote vya majina ya ofisi au wizara na matangazo kama ya mahafali, sikukuu mbalimbali yaandikwe kwa Kiswahili, madokezo baina ya maofisa maofisini yawe ni kwa lugha ya Kiswahili, fomu zote za kujazwa ziwe za Kiswahili.

  Waziri huyo alirejea Waraka wa Kawawa ambaye ulimtaka kila ofisa wa Serikali na viongozi wote wawe mfano mwema katika kutumia lugha ya Kiswahili na kusiwe na kuchanganya changanya lugha na mfano mzuri katika mijadala ndani ya Bunge na watu wote waone fahari katika Kiswahili.

  “Kwa kuzingatia matamko haya na umuhimu wa lugha ya Kiswahili ikiwa sasa ni lugha ya kimataifa inayotumiwa mathalani kwenye Jumuiya ya
  Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika, Serikali inasisitiza matumizi ya lugha ya Kiswahili katika shughuli za serikali na kutoa kauli kuwa pamoja na vipengele vilivyosisitizwa awali,” alisema Mkuchika.
   
 8. RR

  RR JF-Expert Member

  #8
  Apr 22, 2010
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,720
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Lundenga anataka kutuamainisha kwamba Miriam hakufanya vurugu????? :angry:
  Kama ni uongo basi wamshitaki huyu bwana aliyewadhalilisha na kuwapotezea muda.
  My take: Tatizo la msingi Miss Tanzania ni Lundenga mwenyewe! Hadi hapo Lundenga atakaponyang'anywa leseni ya mashindano haya, hakuna mabadilko ya msingi.
   
 9. A

  Alpha JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 614
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  How did this girl even become Miss Tanzania... our standards just seem to be dropping year after year instead of the girls getting better and better they are getting worse.
   
Loading...