Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu na mama yake wahamia CHADEMA kutoka CCM

Angemalzia kwa kuchana kadi

Wakuu:
Hii yote imesababishwa na mkuu wetu wa mkoa.
Cheo alicho nacho hakiendani na Umri/Hekima/Busara sambamba na wadhifa wa ukuu wa Mkoa.

Na hii ni ishara mbaya kwa CCM.
Wanachama ni kama wateja kwenye biashara yeyote ile yenye ushindani, haitakiwi kumpoteza hata mwanachama mmoja.

Hivyo mkuu wetu wakaya ni vyema angetafakari kwa kina na kuchukuwa uamuzi wa haraka.
"...........vinginevyo............."
 
Wema, kila la kheri huko CHADEMA. Naamini umefika kunakostahili hadi kumsindikiza na kukaa beneti na M/Kiti mahakamani! Heshima hiyo ungeipata wapi!

HAHAHAHAAAA WAJINGA NDIYO WALIWAO
 
Wema sasa huku ukipata nafasi ya kugombania ubunge utapata sio chama lile la maharage.

Ndukiiiii
Huku lakini tunajali sana suala la kujiheshimu akamate njemba moja likalipe mahari alichune kwa staha asituletee leo karuka na huyu kesho yule ,anaweza kumegwa na michepuko ila kisirisiri sio hii ya ovyo ovyo!
 
Mimi siwezi kutafakari faida ama hasara kwa chama alichokihama.
Maana tangu jana kuna clip ina"display" youtube kuonesha jinsi tangu mwaka juzi alivyotaka kuhongwa dolar 2k ili ahamie Chadema, nadhani sasa watakuwa wameongeza dau na kufikia kiasi alichokuwa anakihitaji.
Kwa hiyo hamahama hii ni biashara ya maslahi binafsi, hakuna jambo lolote lenye taswira ya tijara kwa umma hapo, hakuna.
Hizi ngebe zinazopigwa humu jf kiushabiki, hazioneshi jinsi gani mawazo ya waTz makini wanavyoona Cdm inavyozidi kuwa dodoki la kufyonza kila aina ya taka.
Kinazidi tu kupoteza umaarufu kwa watu wapenda mageuzi na kuonekana sasa ni chama cha wachumia tumbo, wavuta bangi na kila aina ya mawaa.
Tunakoelekea, muda utaongea , pia muda utakuwa ni hakimu wa hizi figisufigisu zinazoendelea sasa nchini.
Mambo yote haya yatafikia tamati chungu, mbichi na mbivu zitafahamika. Na tukae tusubiri.
 
Kahama kwa kunyong'onyezwa yeye kama yeye...anataka freedom (hisiyo na mipaka)....! Tumekusikia...!
 
Mimi siwezi kutafakari faida ama hasara kwa chama alichokihama.
Maana tangu jana kuna clip ina"display" youtube kuonesha jinsi tangu mwaka juzi alivyotaka kuhongwa dolar 2k ili ahamie Chadema, nadhani sasa watakuwa wameongeza dau na kufikia kiasi alichokuwa anakihitaji.
Kwa hiyo hamahama hii ni biashara ya maslahi binafsi, hakuna jambo lolote lenye taswira ya tijara kwa umma hapo, hakuna.
Hizi ngebe zinazopigwa humu jf kiushabiki, hazioneshi jinsi gani mawazo ya waTz makini wanavyoona Cdm inavyozidi kuwa dodoki la kufyonza kila aina ya taka.
Kinazidi tu kupoteza umaarufu kwa watu wapenda mageuzi na kuonekana sasa ni chama cha wachumia tumbo, wavuta bangi na kila aina ya mawaa.
Tunakoelekea, muda utaongea , pia muda utakuwa ni hakimu wa hizi figisufigisu zinazoendelea sasa nchini.
Mambo yote haya yatafikia tamati chungu, mbichi na mbivu zitafahamika. Na tukae tusubiri.
Kweli KBS chadema wabgekuwa na akili nao wala wasingempokea siasa ni.unafiki mtupuu
 
Mama wema sepetu atawashangaza wengi tu kuelekea 2020, atakuwa hana tofauti na marehemu Bibi Titi Mohamed, kipndi cha Tanu. Nimesikiliza clip yake leo wakati anaongea na waandishi wa habari nyumbani kwake, na moral ya kuunganisha wanawake ndani ya chadema. Anaonekana ni mswahiliswahili na anavimaneno maneno. kiufupi chadema ilikuwa haina watu wa dizain yake. ukiangalia wengi wapo ccm. Ila aangaliwe sana asije akasepa baadae. Kitu kingine tunaomba asiongelee habari za ccm huku, hatuzitaki aje asema atafanya nini ndani ya chadema, na sio blabla ooh makonda, sijui wema kukosa dhamana. Yaani star kama wema angepata dhamana sikuileile ingeleta picha mbaya sana, tungesema kwakuwa ni star au kwakuwa ana hela. Kwahiyo tunaomba asilalamike masuaka hayo huku.
 
Nifananishe harakati ya CDM kupokea wanachama waliokata tamaa baada ya kutofikia malengo Yao kisiasa na harakati za fisi kujipatia mlo wake.Mnyama huyu hutamani nyama fresh na hana jeuri ya kuipata
 
Mama wema sepetu atawashangaza wengi tu kuelekea 2020, atakuwa hana tofauti na marehemu Bibi Titi Mohamed, kipndi cha Tanu. Nimesikiliza clip yake leo wakati anaongea na waandishi wa habari nyumbani kwake, na moral ya kuunganisha wanawake ndani ya chadema. Anaonekana ni mswahiliswahili na anavimaneno maneno. kiufupi chadema ilikuwa haina watu wa dizain yake. ukiangalia wengi wapo ccm. Ila aangaliwe sana asije akasepa baadae. Kitu kingine tunaomba asiongelee habari za ccm huku, hatuzitaki aje asema atafanya nini ndani ya chadema, na sio blabla ooh makonda, sijui wema kukosa dhamana. Yaani star kama wema angepata dhamana sikuileile ingeleta picha mbaya sana, tungesema kwakuwa ni star au kwakuwa ana hela. Kwahiyo tunaomba asilalamike masuaka hayo huku.
Aitsee! Eti atafanya nn! Kwani huko CCM alifanya nn?
Kwa akili ya kawaida tu, unafikiri kuna jipya kwenye usajili wa leo?
 
Back
Top Bottom