MISS JUDY, MEDIAMAN et.al: NANI MWENYE UJASIRI WA KIMAONO WA KUPINGA TIBA YA BABU? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MISS JUDY, MEDIAMAN et.al: NANI MWENYE UJASIRI WA KIMAONO WA KUPINGA TIBA YA BABU?

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by NewDawnTz, Mar 24, 2011.

 1. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  [FONT=&quot]Kabla sijaenda kuwasilisha hoja zangu niombe yafuatayo:[/FONT]

  1. [FONT=&quot]Mods naomba msiondoe hii thread maana haina lengo la kidini. Hapa ni huduma za kijamii zinapochanganyikiwa na mitizamo ya kidini ni lazima ijadiliwe katika hali ya uwazi ili ikiwezekana kuwasaidia wanajamii waelewe katika maamuzi ya upataji huduma ya jamii[/FONT]
  2. Nimetaja hayo majina kwenye heading yangu, sio ku-offend mtu wala ku-defend yoyote (as far as bado sina msimamo halisi wa tiba ya babu) bali kufungua vema mjadala juu ya tiba ya Babu
  3. Thread hii ni reflection ya mtazamo wangu juu ya hoja za kupinga tiba ya babu kwa kuonesha kukanganyikiwa kwangu (ambako naamini na wengine pia) na kuhitaji kusaidiwa kama kuna namna sahihi ya kuondoa contradiction
  4. Tafadhali tujadili tukielewa ni jambo linalobeba hatima za watu kwa ustawi wao ulimwengu wa sasa na ule ujao
  5. Let’s face realities and take challenges
  Yako mengi yamesemwa juu ya tiba ya babu na wala sitazamii thread hii (kama zilivyo nyingine) kumaliza utata unaojitokeza kati yetu juu ya Uhalali wa Maono ya Babu ya kutibu pamoja na uhalali wa njia anayotumia kutibu kwa mujibu wa wachambuzi mbalimbali hapa JF na kwenye jamii kwa ujumla (Ikiwamo media na makanisa yetu)

  Kwa kufuatilia mijadala hii nilishawishika kuamini huenda babu hana uhalali wa kimaono wa kutibu watu na kuamini kama wengine wanavyoamini kuwa babu ni “Mganga kama Waganga Wengine”.

  Msingi wa hoja yangu nitayotoa hapa chini, unatokana na tukio lililotokea hivi karibuni ambalo limebadili kuamini huku na kunirudisha njia ya panda kujua lipi la kuamini. Kuna mama mmoja jirani yangu ambae ni mlokole muumini wa dhehebu moja (haya ya uamsho) ambae toka kuibuka kwa swala la babu amekuwa akinihubiria sana kijana wake kuwa babu hakuna kitu zaidi ya uchawi tu na sikuwa na sababu yoyote ya kutaka kuhoji maana mimi siumwi wala sina ndugu yangu wa karibu ambae hakika kwa namna moja au nyingine yuko kwenye desperate need ya tiba ya babu.

  Hata hivyo lililotokea mwanzo wa wiki hii kwa mama huyu liliniacha wazi. Katika hali ya usiri wa hali ya juu, kumbe majuma kama ma-3 hivi yaliyopita mama Mzazi wa mama huyu alianza kuugua gafla (huyu mama yake mzazi ana umri wa kama miaka 72) na akawa kwenye critical condition akiwa amelazwa hospitali moja iliyoko kwenye mkoa mmoja wapo kanda ya kaskazini. Baada ya kupata tiba ya hospitali na kuonekana bado anao udhaifu alitoa agizo kwa ndugu zake walioko karibu na mama yao kumpeleka kwa babu kupata ‘kikombe cha uponyaji’. Nisiendelee zaidi ya hapa na story hii


  Baada ya mimi kupata taarifa hizi kutoka kwa kijana wa mama yangu huyu ambae hunihubiria sana, nilishikwa na butwaa na kujiuliza jambo moja “JE ALIMPINGA BABU KWA KUWA ALIPATA MAONO YA KIMUNGU KUWA TIBA YAKE SIO YA KIMUNGU AU KWA KUWA HAKUWA MGONJWA NA WALA HAKUWA ANAUGULIWA NA MTU WA KARIBU ASIEPENDA KUMPOTEZA? Je ni wangapi kati yetu ambao tunampinga lakini kesho mke au mume au mtu yoyote ambae kumpoteza ni ngumu hali yake ikawa tishio na tiba ya babu ndio suluhu kwa wakati husika tutaacha tumpoteze au tutakana vinywa vyetu? Ndio maana nauliza “Nani mwenye ujasiri wa kimaono wa kumpinga Babu na tiba yake ya “Maono”?
  [FONT=&quot]
  Tukio hili lilinifanya nianze kuhoji baadhi ya hoja na kuomba ufafanuzi kwa wana-JF ambao wamekomaa na wanaelewa zaidi (wengine wachungaji wetu kama miungu watu, hukawii kuwekwa pembeni benchi la nyuma kwa kuhoji) ili tusaidiane kwa utata huu ili nisije kuwa mnafiki kukataa tiba ya babu kesho mama yangu mpenzi akaumwa nami kifichoni nikampeleka kwa babu au nikaunga mkono uhalali wa babu huku nakosea
  [/FONT]

  Hebu tusaidiane hoja hizi za kumpinga babu kwa kutazama mtazamo wangu (kuunga au kupinga)

  [FONT=&quot]1. Wako wanaokataa uhalali wa dawa ya babu kwa kuwa inatozwa fedha. Swali langu ni kuwa, Je kama Babu kweli ameitwa na Mungu, hana haki na uhalali wa kula madhabahuni (maana anafanya huduma kama Mchungaji wa kanisa lako) kama agizo kuwa Makuhani watakula madhabahuni?[/FONT]

  2. Unaposema masikini wakikosa 500/- hawatatibiwa hivyo inagawa makundi, akili yangu inawaza juu ya makanisa yetu tunayoambiwa tunapotoa sadaka ndipo Mungu anatubarikia…..Je Mungu ni Mungu wa wenye navyo tu kwa kubarikia wale walionavyo na kutobarikia wasionavyo (yaani masikini). Utasema sio lazima utoe fedha unaweza kutoa vitu…..lakini kama nikiwa na kitu (kile ambacho nitatoa sadaka) na ninahitaji fedha kwa tiba, Je si nitakiuza nipate fedha ya tiba? Upo utofauti wa kimantiki au kimaandiko hapa? Mbona pia nakumbuka Mungu aliweka kitu kinaitwa Divine/Religious Tax kwenye Kutoka 30:11-16, Je hapa alipitiwa? Mnisaidie Mkanganyiko huu wandugu.

  Pia kuna hoja kinyume nah ii inayouliza ni kwa nini babu hapokei wakati makuhani wameambiwa wale vya madhabahuni….Je Mungu hatoi kanuni na miongozo yake kuendana na tukio? Je Mungu hakuwaambia waisraiel washambulie mataifa mengine wakati ule na kuichukua nchi yao ya ahadi na kuteka mateka na kuyafanya yao? Lakini je sie Mungu huyu pia aliekata wakati fulani wana wa Israel wasichukue kitu toka mikononi mwa taifa mojawapo (silikumbuki) ambalo yuko mmoja (bila shaka ni Akani) ambae kwa siri aliiba na kuficha na kisha hasira ya Mungu ikawa juu ya hema ya Israel mpaka walipomtoa na kumuua kwa kwenda kinyume na Mungu?

  Je Mungu huyu huyu anaesema makuhani wale maddhabahuni kwa huduma yao sie Yule aliemwambia Elisha asipokee kitu kwa Naaman baada ya kupona na mtumishi wake Gehazi alifanya kosa kuokea? Je hatuoni kuwa mambo ya Mungu ni specific under some kind of circumstance na sio kukariri? Je si ndio maana ya wito wa kumsikiliza Mungu? Can we call HIM Double Standard? No ni katika kutaka tufikiri na kumsikiliza na sio kukariri kama kasuku

  3. Kuna mtu anatoa hoja kusema Babu angekuwa mtumishi wa Mungu angeanza maono pale alipopata maono mara baada ya kufunuliwa na Mungu (Ishara ya Kukosa Utiifu) (Mwaka 1991) na asingengoja mpaka watu wafe wengi ndio atekeleze maono. Akili yangu inajiuliza swali hili, Wakati wa Kuhani Eli ulikosekana uongozi wa kimungu Israel na Mungu akamwita Samweli toka mtoto na kuja kuanza huduma yake akiwa mtu mzima…Je kwa nini Mungu aliacha taifa liende bila maongozi kungoja mtoto akue wakati aliweza kuchagua mtu yeyote mzima akashika jukumu? Je kulikuwa na miaka mingapi iliyopita toka Daudi apakwe mafuta na kuwa mfalme mpaka alipokuja kuwa mfalme? Pia je ni mika mingapi toka wanadamu walipoasi mpaka masihi Yesu alipokuja kutoa hakikisho la ukombozi, Je Mungu hakujali miaka yote watu kupotea dhambini wakati huo? Who has got the idea here to help me out?

  4. Kuna wanaosema babu hana maono ya kimungu kwa kuwa dawa yake inatoa kwanza nafuu kisha ndipo itibu….Nakumbuka kuna siku mchungaji wangu alihubiri habari ya mtu ambae Yesu alimponya upofu lakini haku-gain instant vision kwa wakati huo kiasi cha kuona watu kama miti inatembea…..Je huyu hakuwa Yesu aliefanya hivi? Au nilikosea kumnukuu mchungaji? (maana andiko lenyewe silikumbuki ni kitabu gani japo bado ninakumbukumbu ya mchungaji akihubiri neno hili)

  5. Kuna hoja ya “Mtaweka mikono yenu juu ya wagonjwa” na sio mtawachemshia dawa (Normal Human Procedures)….Lakini bado kumbukumbu za mchungaji wangu zinanijia kunasiku alifundisha juu ya uponyaji na kuna mifano alitoa inayogusa watu ambao waliponywa bila “kuwekewa mikono” bali kwa njia za kawaida kabisa…..Mbona Mungu alishusha Mana ili kutibu ugonjwa wa njaa uliokuwa unakabili wana wa Israel, kwa nini “hakuweka mikono yake juu yao” na kuwashushia upako wa Mshibo ili ijulikane kuwa ni njia ya kimungu kwa context yetu? Mbona alitumia nyoka wa Shaba kuwatibu wana wa Israel walipoasi, Je kwa nini hakumuambia Musa “weka mikono yako juu ya watakaong’atwa nao watapona”?

  Vipi kuhusu Naaman mkoma alieoga kwenye ziwa (2 Kings 5:1-27) Je, hoja yetu hapa sio kama mwitikio wa Naaman kwa kauli ya Nabii kuwa akaoge mtoni na kusema hakutarajia kuambiwa hivyo wakati kafungishwa safari na alikotoka kuna vijito vingi ambavyo angeoga? Sio Naaman alikuwa na imani kama sisi kuwa ili uponyaji uwe wa kimungu lazima mtu wa Mungu akuwekee mikono na kukushindilia kwa nguvu kwa jina la Yesu hadi uanguke?

  Mbona Elisha alitumia njia ya kawaida (maji yaliyochanganywa na unga) ili kuponya waliokutwa na mauti sufuriana kutokana na kula matango ya porini (2Kings 4:38-41)…Je kwa nini hakuwawekea mikono? Vipi Yule kipofu ambae Yesu alimponya kwa kupaka macho yake matope ya MATE (msisitizo, kama nakosea nisahihishwe), Je huyu hakuwa Yesu huyu tunaesema hawezi mtuma babu kwa njia ile? Pia vipi ile birika ambayo ilikuwa Bethseda (Yoh 5:1-16) ambayo ilitumika kutibu watu ambao hawawezi? Mbona na yenyewe ilikuwa ni ya kawaida na yenye Procedures (kutibuliwa kwanza na malaika) Mbona Yesu hakui-crash wakati wake duniani?


  6. Kuna hoja ya Babu kutibu magonjwa baadhi na sio ya kila aina: Ni seme wazi kuwa kwa muda mchache nimeona wanaoenda ni wenye magonjwa zaidi ya wale walioenda. Hata hivyo hata kama wangeenda hao tu, je mbona kuna maeneo Mungu analeta uponyaji kulingana na hitaji husika?

  Tukiacha hoja hii, Je ni kweli kuwa Mungu ni “single-principle minded” kwa maana ya kuwa mara zote hufanya kama alivyofanya jana? Can’t he change some procedures kulingana na haja na kile anachotaka kujifunua kwacho kwa wakati husika? LAKINI PIA WAKATI WA YESU HAKUKUWA NA UKIMWI….

  Pia suala la kuponya magonjwa yote sio lazima lifanywe na mtu mmoja kwa wakati wote. Je sina uhalali wa kutumia lile andiko (silikumbuki vizuri liko wapi japo naamini ni andiko sahihi) linalosema “Karama hizi hugawiwa na Mungu mwenyewe kama aonavyo vyema”. Je hapa Mungu atakuwa kakosea kumpa Babu karama za baadhi na kutompa yote? Je hatufundishwi makanisani mwetu kwamba Mungu hawezi kukupa vyote yaani MCHUNGAJI WEWE, DOCTOR WEWE, MBUNGE WEWE, MWALIMU WEWE, MTUNZA HAZINA WEWE, MWINJILISTI WEWE, ASKOFU WEWE….Everything wew….Je hakutoa wengine kuwa mitume, wngine waalimu, wengine na karama za uponyaji na wengine karama za roho n.k KAMA APENDAVYO YEYE (na sio sisi tafadhali)? Je hii haiwezi ku-apply kwa babu kuwa ndicho Mungu alichomuitia? (itapothibitika kweli kaitwa na kutumwa na Mungu)


  7. Iko hoja ya babu hawambii watu waache dhambi: Je kauli na kanuni ya babu ya tiba yake ya “tumia mara moja usirudi tena” sio njia nyingine ya kuwaambia watu waache dhambi? Je anaposema usiende kurudia kilichokufanya upate ukimwi inamaanisha nini kwa ndani zaidi? JE SIO SAWA NA KUSEMA USIENDE KUZINI TENA? Au anapowaambia watu ukishaipata nenda kamshukuru Mungu kwa uponyaji hii inamaanisha nini? Au Yule niliemsikia akisema hivi hakuwa Babu? Je hii maana yake nini?

  Au babu mpaka asimame masaa 4 atoe hotuba ya injili ndio tujue anaponya? Birikani Bethseda kulikuwa na mtubishaji? Je sio malaika alipaswa kutibua tu kisha mtu aoge then apone akamshukuru Mungu mbele kwa mbele kwa uponyaji? Je wa kulaumiwa ni babu au ni watu wasiomshukuru Mungu? Kuna kipimo hapa cha kuhoji uhalali wa huduma ya Babu?


  8. Wako wanaosema haiwezi kuwa huduma ya kimungu maana inavuta watu wengi hadi inahatarisha maisha ya wengine: Hapa napo nina swali la kujiuliza….Nikitumia mfano wa hapo juu kwenye birika la Bethseda(Yoh 5:1-16), Je tunaposoma vizuri hatuoni kuwa hata kwenye huduma hii ya kimungu ya uponyaji ya wakati ule pia kulikuwa na msongamano? Huyu mtu ambae Yesu amemkuta anangoja kudumbukia birikani (Sio kunywa kikombe kimoja) tena kwa kungoja maji yatibuliwe. Je tunafahamu mtu huyu alikuwa hapo kwa muda gani akisubiri? Biblia inasema alikuwa hapo yapata miaka 38, ooh! My what a Congestion that was? Vipi tushangae hawa wa kukaa wiki 1 au siku 3?

  Lakini mbona Yesu pia alifanya muujiza wa maltitude pale alipolisha watu 5,000/= (waume bila wake na watoto), Je hapa Yesu anajipinga au sisi ndio tunaompinga? Au kwa kuwa huu ni uponyaji wa njaa na sio Kansa? Je kuna madaraja wa miujiza/uponyaji?


  Kwa kumalizia nitoe nukuu moja ninayoipenda sana. Bishop Adeyemo ambae ni Executive DIRECTOR wa Centre for Biblical Tranfsormation anasema “God does not always use the same methods, and we must learn to listen for different instruction (from Him) in different stages and circumstances”. Je kwa nukuu kama hii hatuoni tunajaribu kumuweka Mungu katika “mabano” ya kuwa mwenye kutumia njia moja tu katika ufanyaji kazi wake tunapotumia hoja hizi kuhoji uhalali wa tiba ya babu?

  Pia kuna Author mmoja (sikumbuki vema jina lake) aliwehi kusema hivi “We find answers to hard question and confusing one through Godly prophetic words……”

  Babu anasema ameoneshwa na Mungu, Je mnaopinga na nyie mmeoneshwa na Mungu? Ndipo ninapouliza, Je kati ya tunaopinga maono ya Babu, Je yuko kati yetu ambae Mungu amesema nae kwa wazi kuwa sio maono ya kimungu na anaweza kusimama wazi kabisa mbele ya watu (kama babu) na kusema Mungu amemuonesha kuwa tiba ya babu ni ya kishetani (Mganga kama waganga wengine wa kienyeji) na ya kuwa watu hawapasi kumuendea kupokea uponyaji wa kimungu?

  JE YUPO, JE UJASIRI ANAO, JE ANAWEZA KUSIMAMA? Kama sivyo, basi wote tutaungana na Kakobe ambae sijamsikia akitoa Message zaidi tu kuikata on the ground itahamisha “washirika” wa huduma zao za uponyaji?
  Au ndio sisi ambao leo hatuuguzi wala hatuuguzi tunampoinga babu kesho yakiba tunawapeleka kifichoni (kama huyu mama jirani yangu)?

  Nawasilisha
   
 2. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Soma maoni haya hapa.

  Source:MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo


  "Hapa Arusha KILA HOSPITALI IMEPOKEA WATU WA MAGONJWA YA PRESHA, KISUKARI, PUMU, N.K. AMBAO WALIKWENDA LOLIONDO "KUTIBIWA" MARADHI HAYO NA BAADA YA KUPATA "NAFUU" (PSYCHOLOGICAL) KWA KAMA WIKI MBILI TU WAMEANZA KUUMWA SERIOUSLY NA KURUDIA DAWA ZAO ZA HOSPITALI TENA.


  Pili, mimi nikiwa mfanyakazi wa maabara ya hospitali ya MT Meru, sijaona hata mgonjwa mmoja wa ukimwi aliyepata "seroconversion" yaani kurudi "seronegative from serpositive status". Kinachosikitisha ni kuwa kuna watu hawataki kabisa kusikia yanayosemwa na madaktari na wafanyakazi wa hospitali mbalimbali hapa Arusha ambao kila siku tuna-deal na watu wanaozidiwa baada ya kwenda Loliondo.


  Mbaya zaidi kuna magazeti, tv na redio hayataki kabisa kusikia ukweli wa majanga yaliyowafika watu waliokwenda huko. Ajabu pia ni kuwa kuna watu ambao ukitaka kuwaeleza ukweli wanakuona wewe ni mpagani usiyemwamini Mungu. Naomba waandishi wa habari wawe proactive katika kutafuta ukweli na si kutegemea mass hysteria iliyowakumba maelfu ya watu wanaotafuta miujiza kwa nguvu."
   
 3. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Angalau cases kama hizi zinapojitokeza zinaweza kutupa picha halisi na kutusaidia kupata conclusion

  Pia kuna mtu ambae mimi namfahamu amekuwa mgonjwa wa kifua for more than 5 years na huwa hatoki ndani kukiwa na baridi mpaka mchana au jua litoke.....jana nilikuwa nae anasema amepona kabisa.........Should it mean kuwa ni kwa mujibu wa kila anaeamini au kwa watu kadhaa???

  Which is which?

  Bado nahisi kama vile iko haja ya devine revelation kutoa muongozo wa wazi juu ya babu.......
   
 4. A

  Ame JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Nitabia ya kishetani kutumia desperation ya watu kuwaletea tumaini pale ambapo unauhakika kabisa hilo tumani halipo. Sikuwa nimelifikiria hili lakini sasa naanza kupata wasi wasi kwamba kuna nguvu za giza zinatumika pamoja na political motives ili kufikia malengo binafsi. Nimetoka kuangalia rapid research iliyofanywa na wakenya inayoonyesha madaktari wakipinga kupata evidence yeyote ya walioponywa. Swali langu ni je kwanini waandishi wetu hawako tayari kuinvest katika hili huku hili swala likigusa sana maisha ya watu pamoja na conscious zao? Je hakuna power nyuma yake inayozuia haya kutokea? Haya nayo yauliza yakipata majibu basi nitashukuru.

  Kwa upande wa imani hiyo kwa all standards inaenda kinyume na imani ya kikristo ambayo iko rooted kwenye redemption of Jesus christ; kwamba baada ya resurection hakuna kitu kingine kinaweza leta solution katika problem yoyote ile nje na jina la Yesu; huyu Babu nimeangalia ile utube hakuna sehemu anamtaja Yesu; yeye kakazana Mungu, je huyo Mungu jina lake linaitwa nani? Mungu hafanyi kitu chochote duniani bila kuji Identify kwa specific name tangu enzi za mababu na hasa wakati huu hasa yuko specific jina lake linaitwa Yesu. Nje ya Yesu basi huyo ni Mungu mwingine siyo wa wakristo. Mtu kwamfano akiniambia Mungu wake anaitwa for example (Respect waislamu ntawatumia kama mfano tu hapa) anaitwa Alah, mimi huyo si mungu wangu wala simjui lakini haina maana kuwa yule anayemwamini Alah ni mwongo no ila tu ni kwamba huyo ni Mungu wake na si Mungu wa wanaye mwamini wakristo. Ukijiita mkristo basi jina la Mungu wa kikristo anaitwa siku hizi Yesu na zamani alikuwa na majina mengi na kila alipokuwa anatokea mtu alikuwa anamwambia jina lake tofauti. Kwenye uponyaji alikuwa anaitwa Jehova Yire (God my healer); kwenye vita alikuwa anaitwa Jehova Nisi (Yaani Bwani ni bendera ya ushindi wangu); sasa hayo majina yote akayaleta pamoja na kulifanya likawa moja yaani Yesu.

  Kwangu mimi muislamu kuniita kafir kwa mfano ni sawa kabisa maana ndivyo nilivyo katika imani ya Kiislam na waislamu kukataa Yesu ni Mungu ni kweli kabisa kwasababu jina la Mungu wanayemjua anaitwa Allah. Sasa ikija tokea huyo Mungu akajitokeza baadaye akasema mimi ninayeitwa Yesu ndiyo huyo huyo Allah basi kunatatizo gani? Mungu si mjinga atamhukumu kila mtu kwa jina la Mungu anayemjua. Itachekesha sana wewe uko America (Raia) unakataa kufuata sheria za Obama eti kwasababu wewe ulizaliwa Tanzania na jina la Rais wa nchi uliyozaliwa anaitwa Jakaya Kikwete alafu unataka ulazimishe watu wa America watambue eti JK ndo rais na wa wa America walio zaliwa huko lakini wana ishi Tanzania (Raia) nao wanalazimisha eti jina la rais wao anaitwa Obama.

  Tuache blind faith let us know what we are supposed to know in fully ili kuepusha mikanganyo na confusion with the end results of human sufferings.
   
 5. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  NewDawnTz,

  Hata kama huduma anayotoa babu ni ya kimungu Si wote watakaopona.
  Huyu babu nasikia anahudumia hadi watu 3000 - 4000 kwa siku, hao wa Mt Meru wanatoa uwakilishi gani ili tufikie hitimisho.
  Maelezo kwenye hoja yako ingawa wewe uemleta kwa mfumo wa maswali kimsingi hayo ndio majibu ya kila swali.

  Binafsi nimeamua kuchukua msimamo wa kumpa babu "benefit of doubt" ili kama huduma inatoka kwa Mungu I'll praise Him for that lakini kama sio ya Mungu bado waliokunywa sijaona wakipagawa ama wakimwabudu babu kama ilivyokuwa Kibwetere.

  Kama ulikuwa mfuatiliaji wa siasa za makanisa utakumbuka huyu Kakobe mwenyewe alipigwa vita sana miaka ya 90. Aliitwa kila jina la ushetani unalolijua. Leo yuko kundini anawaita wengine mashetani, hapo ndio ujue kuna mushkeli mahali fulani na unaweza kuita siasa za makanisa.
   
 6. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  watanzania tu wanafiki sana!mkuu wa mt meru hongera kwa kueleza uhalisia unaotokea arusha ambao kwa makusudi unafumbiwa macho na media zetu,niliwahi kutoa post inayowakumbusha waandishi wa habari majukumu yao.nilisema wafuatilie mgonjwa kabla ya kunywa kikombe na vipimo vyake baada ya kunywa kikombe,hakuna aliyethubutu kufanya hivyo kwani taarifa ya kwamba dawa ya babu ni uongo haiwezi kuuza gazeti.
  Mimi pia ninawafuatilia waliotoka kwa babu hasa wenye kisukari na hypertension.sijaona aliyepona.nimeweka pembeni wale wenye ukimwi kwa sababu kipimo kinachotumika ni antibody based test hivyo tunaweza sema kirusi kimeondoka lakini antibodies bado zipo,nakushauri lab technician wa mt meru kuendelea na uchunguzi wako,peleka sample zako K.C.M.C kwa ajili ya PCR hapa utaweza kutambua kama kirusi kimeondoka au la.pia nakushauri kama mtaalamu uweke rekodi specific kwa watu waliokunywa kikombe,hapa tutajua mbivu na mbichi.tusiwategemee wanasiasa wetu hawataki kusema ukweli.
  Big up! ndibalema.
   
 7. A

  Ame JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Hii hapa scandle nyingine ya urgent wa shetani alipojifanya angle of light.
  YouTube - Belgrade Healer: The other life of Radovan Karadzic

  Former Bosnian Serb leader Radovan Karadzic was put on the international wanted list in 1996. He was charged with genocide, crimes against humanity and violation of the laws and customs of war in Bosnia and Herzegovina. Karadzic was only found and arrested in 2008. He was immediately brought before the Hague tribunal. Where had he been hiding all those years? Why could the police not track him down? A secret love affair, miracle healer, heartbreaking betrayal and more - in a new XL Report, only on RT.
   
 8. A

  Ame JF-Expert Member

  #8
  Mar 25, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Jibu ya how to know the secret things of God liko hapa. Sasa jipe homework and you will come to know why we oppose Babu by all strength and power we have in our Lord Jesus ili tuweze kuokoa roho zinazopotea kwa kutolijua neno la Mungu.

  || Pastor Chris Online - Channel ||

  http://www.pastorchrisonline.org/channel/watch/cha1936492a2ed/?videoID=vid34d3ea81560

  http://www.pastorchrisonline.org/channel/watch/cha1936492a2ed/?videoID=vid3bdd

  http://www.pastorchrisonline.org/channel/watch/cha1936492a2ed/?videoID=vid5296a495c

  http://www.pastorchrisonline.org/channel/watch/cha1936492a2ed/?videoID=vid1d8fb06

  In 2011 I am burning and a shinning light and I will cause that light to shine in JF

  Glory to God!
   
 9. A

  Ame JF-Expert Member

  #9
  Mar 25, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Kasome tena bible yako taratibu na kabla ya kusoma omba kwanza uvuvio wa roho mtakatifu...Injili ya Yohana inaanza kwa kusema "Hapo mwanzo kulikuwepo na neno naye neno alitoka kwa Mungu naye neno alikuwa Mungu.." Injili zote zina elezea kuwa neno akatwaa mwili akakaa kwetu..... naye bikira atachukua mimba atazaa mwana naye atamwita jina lake Emanule, yaani Mungu pamoja na sisi.. Na evidence kibao kuanzia utabiri wa prophet Isaya kama bado hujafahamu kuwa Yesu ndo huyo Mungu basi ukristo wako bado ni wa mashaka sana maana hulijui neno bado.

  Sasa huko Sunday school huwa wanawafundisha kati ya Mungu baba na Yesu mwana wa Mungu nani mkubwa kuliko mwenzake? Bila shaka kwa maoni yako utasema kwavile Mungu ni baba basi Yesu lazima awe mdogo maana ni mwana wa Mungu. Kwasababu mimi ni muhubiri acha nikusaidie kuwa kama unavyoliona Jua basi lina mwanga, linajoto na lina umbo sasa sijui kati ya nguvu ya mwanga wa mwali wa jua na joto lake kipi ni kubwa kuzidi kingine? Unapolikaribia jua basi jinsi mwanga wake unavyokuwa mkali basi ndivyo inavyokuwa kwa joto lake so huwezi kusema unaweza kutofautisha kati ya mwanga na joto katika mwali wa jua japo kila moja lina impact ya tofauti katika out put. Ndivyo ilivyo kwa Mungu katika utatu mtakatifu wake hakuna aliyeanza na hakuna aliyemdogo wote kwa pamoja they function as one japo output na impact zao zinaweza ku vary. Mfano ilibidi yesu atwae mwili wa binadamu aje afe na baada ya kufufuka atuokoe na utawala wa Ibilisi (Hapo yesu ni neno la uzima wa Mungu). Roho mtakatifu naye matendo yake ni mengi, yeye ndiyo wisdom and power of God na Mungu baba yeye ndiye mwenye enzi na mamlaka so different office to the same God.
   
 10. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo mnataka kusema wale wote waliokunywa kikombe cha babu wanaweza kutuacha soon au sijaelewa????

  Msitake kuwapa pressure bana.................:lalala:
   
 11. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #11
  Mar 25, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Alafu mambo ya babu yameingiaje kwenye Bible?????
   
 12. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #12
  Mar 25, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,568
  Likes Received: 1,932
  Trophy Points: 280
  JOHN 8 : 56 - 58
  56 Your father Abraham rejoiced to see my day: and he saw it, and was glad. 57 Then said the Jews unto him, Thou art not yet fifty years old, and hast thou seen Abraham? 58 Jesus said unto them, Verily, verily, I say unto you, Before Abraham was, I AM.
   
 13. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #13
  Mar 25, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,568
  Likes Received: 1,932
  Trophy Points: 280
  Umekimbilia hoja ambazo unahisi zita-justify uganga wa babu. Umeacha hoja ya msingi kabisa, imani. Babu anatibu wenye imani. Sasa wewe ukiwa mdau wa babu hebu tusaidie ulikwenda pale ukiwa na imani ipi kati ya hizi;
  1. Kwamba dawa inaponya
  2. au babu anaponya
  3. au Mungu anaponya
  4. Yesu anaponya

  Mfikirie na Abdala, Kingunge, Somji n.k. Je wanashare Mungu? Mimi nahisi huu ni mpango mahsusu toka kwa maitrea kuileta dunia yote katika dini moja. Babu ameunganisha watu wa kada zote.

  Pia habari ya kama sisi tumepata maono kupinga, nakushauri usiwe mvivu wa kusoma biblia. Yote yamo humo.
   
 14. A

  Ame JF-Expert Member

  #14
  Mar 26, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Thanks bro unajua tunaugulia madhara ya dini ambayo hapo mwanzo ilikatazaa watu kutokusoma bible na viongozi wa dini bila kujua au kwakujua walikuwa wanatimiza mission ya shetani.

  And this IAM is actually a specific name of God which He used to reveal Himself to Moses when he appeared to him in form of burning fire in the bush. Moses asked him if Israelites ask me what is the name of that God what would I say? He answered tell Them IAM who IAM. Sasa tunapowaambia watu kuwa ni muhimu kuuliza Mungu anayetenda kazi ndani ya babu jina lake ili tujue kama kweli ndiye huyu wetu wanakuja juu.

  Hawajui kuwa names have purpose maana zina describe personalities. God's trinity each has its specific personality. They worship God in blindness; kwenye new testament God is saying zamani zile za ujinga Mungu alimvumilia mwanadamu maana walikuwa wanamwabudu kwa tradition na mazoea huku wakiwa hawamjui huyo Mungu mwenyewe. sasa watu walio bado katika 'ujinga' illiterete wanataka wote tumwabudu Mungu bila kumjua identity yake, ukiwa uliza wanakwambia eti huwezi kumchunguza wala kumjua Mungu. If this statement is true then Hollyghost mission in this world is a failure maana yeye hasa ndiyo office yake ku mreveal God in His true name/identity and characteristics. Hawataki kukubali kuwa wanahitaji kuwa humble na ku learn through Hollyspirit who is actualy this God ili wasijetapeliwa na miungu wengine na elimu ambazo hasa ndiyo mpinga kristo isipotumiwa kwa manufaa ya imani.

  God is real and not vague He is seen and can be seen with both physical and spiritual eyes. The design is you first have to be spiritualy open for you to see him in physical eyes. Hata science inaeleza jinsi physical eyes through reflection ya light rays inavyoweza kumfanya mtu aone physical object. Kwa hiyo the same principle ina apply between spiritual eyes na physical eyes. And actually its been stated in the word that God is light. Sasa hakuna forms of physical objects bila reflection ya light rays. Atleast in my elementary physics I can still understand who is God through his word. I can write pages jinsi ya kumjua Mungu wa kweli.
   
 15. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #15
  Mar 26, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0


  May be i can say sorry kwa sababu sijakwenda kwa babu na nilishasema toka mwanzo kuwa sijui kama namwamini babu au simwamini babu

  Na nilichozungumza mimi sio kumuunga mkono babu au kumpinga ila ni kuhoji je sababu kama hizi zilizotolewa hapo juu zinatosha peke yake kusema babu ni mganga? Je hakuna maeneo ya kwenye biblia ambapo Mungu alifanya kinyume kwa mfano mtu anaposema Mungu huponya kwa kuwekea mikono kama ilivyoandikwa "mtaweka mikono yenu" je hakuna maeneo Mungu alifanya pasipo kumwekea mtu mikono na kushandaraizi kwa sana? .........wewe unazungumza katika "pre-judgement" mind lakini hujui kuwa kuna watu wengi ambao ili mambo wayaelewe wanahitaji miguu yako "uliekomaa sana kiroho na unaejua biblia" kwa kumsaidia kuondoa utata kama niliouanisha hapo juu?" mtu anaelewa nini unapomuambia Mungu anaponya kwa kuwekea mikono na anaposoma Biblia au anapokumbuka aliwahi kuhuniriwa kuwa Mungu alimponya Naamani kwa kuoga tu kwenye Mto wa Yordani...Je lipi ashike? Je peke yake inatosha ku-justify?

  Hiki ndicho lengu la thread yangu ili kusaidia kujua kwamba unapozungumzia sababu kama hizi watu wanatazama katika maandiko nakukuta kuna mambo yalifanyika na Mungu kwa namna tofauti na hivyo hata ile shaka yao kuondoka kwa sababu sio sababu tosha pekee za ku-justify

  Ndio maana pia nauliza je kwa kutumia sababu hizi watu waseme Mungu ni double standards?
   
 16. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #16
  Mar 26, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,568
  Likes Received: 1,932
  Trophy Points: 280
  My apology. Sikukusoma vema ndugu.
   
 17. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #17
  Mar 27, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  You have mine brother....

  Ni katika kusaidiana na kueleweshana....Ahsante kwa kunielewa
   
Loading...