Miss East Africa 2009: What a JOKE? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Miss East Africa 2009: What a JOKE?

Discussion in 'Entertainment' started by n00b, Dec 21, 2009.

 1. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  Read these stories:


  =========================

  Title: Miss East Africa 2009 LIVE in Tanzania
  When: 18.12.2009 - 19.12.2009
  Where: Mlimani City - Dar-es-salaam

  Miss East Africa 2009 will be held at the Mlimani City Complex in Dar es Salaam.

  28 girls from 14 regions will contest the title. They will come from Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Ethiopia, Eritrea, Djibouti, Comoro, Seychelles, Madagascar, Reunion, Mauritius and hosts Tanzania.

  The lucky winner will get a Range Rover Vogue Sport worth 165,000 US dollars (about 200m/-), from CMC Automobile.

  =========================

  [​IMG]

  CAPTION: Mkurugenzi wa Lena Event Lena Calist akizungumza na wanahabari katika mkutano uliofanyika kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski August 9, 2009 wakati wa uzinduzi rasmi wa bahati nasibu ya Miss East Africa ambapo gari aina ya Range Vogue Sports litashindaniwa


  [​IMG]

  CAPTION: Mkurugenzi wa Lena Event inayoandaa Miss East Africa Lena Calist akionyesha gari aina ya Range Vogue Sport lenye thamani ya dola za Kimarekani 165.000 litakaloshindaniwa katika bahati nasibu ya Miss East Africa iatakayoanza kesho mpaka siku ya fainali ya Miss EastAfrica itakayofanyika desema 18 2009 jijini Dar es salaam, Lena ameongeza kwamba ili kucheza bahati nasibu hiyo utatakiwa kununua tiketi kwa shilingi 1000 au kucheza kupitia simu ya mkononi kwa mitandao yote ukituma neno SHINDA kwenda namba 15567 kwa shilingi 1000 na kujipatia nafasi zaidi ya kushinda zawadi hiyo ya Gari,wengine waliopo katika picha ni Foti Gwebe Nyirenda Mshauri wa Mauzo CMC Motors na katikati ni Miss East Africa namba mbili mwaka 2008 Annete John

  Angalia, dhamira yangu ni njema sana, mimi ni mpenda ukweli na muwazi, wizi wa wazi kwa watanzania wakati Gaming Board ipo na inaukalia wazi wizi wa namna hii inakera SANA. Hatutokaa kimya, ahsante JF kwa kutupa uwanja wa kutoa uwazi wa mambo haya, naendelea zaidi chini kuuanika uwizi wa jamaa hawa...


  Read the news:
  Kwenye gazeti la Oktoba 18 la Citizen wanaendelea kujinadi tu:

  Gakwaya says, "We shall field the best two from Rwanda for finals in Dar Es Salaam ." This year, Miss East Africa will walk away with a prize of Range Rover, worth US$165,000 on December 19.


  Lakini Disemba 16 angalia kwenye Daily News walichoongea mbele za waandishi wa habari:

  Chairman of the organizing committee, Rena Calist told reporters today that the winner would drive home a Toyota Celica sports car worth over 30m/- plus a one-year contract with the company valued at 50,000 US dollars (about 60m/-).

  [​IMG]

  Thats:
  Warembo wanaoshiriki kwenye shindano la Miss East Afrika linalotarajiwa kufanyika desema 18 kwenye ukumbi wa Mlimani City wakiwa wamepozi pembeni mwa gari la zawadi ya mshindi wa shindano hilo aina ya Toyota Celica Sports kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach and Resort.

  Nadhani nina matatizo ya ubongo wakuu, au nachanganya madawa????
   
 2. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,120
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Range Rover ni kwenye bahati na sibu ya Miss East Africa, yaani mimi na wewe tunaweza tukashinda hiyo range tukinunua hizo ticket za buku.

  Hiyo Celica ni kwa ajili ya atakayeshinda umiss wenyewe.

  Waandishi wa habari nadhani wamechanganya.
   
 3. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #3
  Dec 21, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  That means kuna mtanzania alijinyakulia hiyo Range Rover mkuu? That's a great news for him/her!

  Alitangazwa siku hiyohiyo? Nani huyo? Nadhani ni mshindi zaidi ya Miss mwenyewe! Basi hapa waandishi walichanganya madesa kwelikweli
   
 4. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #4
  Dec 22, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,754
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Ha ha ha Rena Calist... Waiter leta Tusker Bariiiidi!!!!
   
 5. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2009
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Nionavyo mimi haya mashindano ya urembo watanzania hayatufai maana sijui ni vigezo vipi vinatumika kuwapata hawa washindi kila nikinyambulua mashindano yote yatakayoshirikisha nchi zaidi ya moja hatuwezi kushinda, yaani tunakuwa kama watalii na wasindikizaji. sababu ni zipi hasa.?

  Nilikuwa nategemea mshindi wa EA atoke Tz lakini wapi, katoka Rwanda yaani hata nafasi ya pili hakuna, Miss world ndio kabisa ni ndoto kushinda, Tusker project ndo usingizi watu kutolewa round za mwanzo hata top ten mtu haingii, Miss universal vilevile, afadhali hata Miriam anejitahidi Miss Earth. Sasa nakua sioni faida ya haya mashindano. maana sielewi tatizo linalotufanya tushindwe kila siku nini. yaani kila anayeenda kushiriki haya mashindani tumaini linakuwa halipo ila ni kuongeza namba ya wale walioshindwa.

  Jambo lingine hizi zawadi za magari ya kifahari zinazotolewa kwa upande wangu sioni kama zinamanufaa sana kwa hao washindi maana magari kweli ni ya kifahari sijui inakuwaje pale linapoharibika ni kweli hawa ma-miss wana uwezo wa kuyamudu kwa matengengezo na service ya kila mara? kizuri gharama ati. Yaani mimi ningeona ingekuwa mtu anazawadiwa nyumba hata yenye thamani ya hiyo gari ingekuwa bora mara mia. Mtu anakuwa na uhakika wa maisha yake au kama siyo nyumba basi hizo pesa zinge- invest kwenye elimu yake mpaka atosheke ingekuwa vizuri zaidi maana tungekuwa tunaongeza wataalam ambao wangeleta tija kwa jamii sio kujishoo tu wakienda nje wasindikizaji. kuondoka kwa shangwe na bendera inapepea kurudi kimiyakimya bendera imekujwa. hata sijui wahusika wafanyaje nadhani wanalo jibu.

  Ukirudi kwenye michezo mingine kama riadha, kuogelea, mpira yote ni yale yale sijui Tanzania katika michezo ni mchezo upi tunaweza kujisifia kama wenzetu wengine mfano Kenya, ethiopia n.k. Mimi nafikiri huu mchezo wa bao tungejitahidi angalau ufikie ngazi za kimataifa pengine tungeweza kuwa ma-champion. sidhani kama bao nalo tungefungwa. unajua siku zijazo wazungu wanawezavumbua hili bao na kulifanya mchezo maarufu mpaka kwenye Olympic halafu tukashangaa wakati TZ wazee wanajua bao kama nini wakiwa na kahawa yao pembeni. zinduka.
   
 6. d

  daddi5 Member

  #6
  Dec 22, 2009
  Joined: Aug 24, 2008
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  sijawahi kusikia gari inaitwa Range Vogue Sport!!!! kuna range rover vogue and range rover sport, huge difference sport version is way cheaper than vogue, sasa hiyo bei aliyosema ya 165,000$ du sijui wameipataje, hata vogue na usafirishaji wake, ushuru na insurance na reg sio bei hiyo
   
Loading...