Misri yawaapisha majaji takriban 100 wanawake katika hatua ya kwanza kama hiyo

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,203
4,677
Misri imewateua kwa mara ya kwanza wanawake 98 kama majaji katika moja ya vyombo vikuu vya idara ya mahakama nchini humo - Baraza la kuu la serikali.

Majaji waliapishwa mbele ya jaji mkuu wa baraza hilo katika hafla iliyofanyika katika mji mkuu Cairo Jumanne.

Inakuja miezi kadhaa baada ya Rais Abdul Fattah al-Sisi kuwataka wanawake wajiunge na vyombo vikuu viwili vya mahakama - baraza na Mashtaka ya Umma.

Tangu kuanzishwa kwake mnamo 1946, Baraza la serikali limekuwa likiwateua wanachama wa kiume pekee na hadi sasa limekataa kabisa maombi ya wanawake.

Katika miaka iliyopita, wanawake walipinga maamuzi ya baraza, hilo wakisema kuwa wanabaguliwa

BBC
 
Back
Top Bottom