#COVID19 Misri: Watu watatu wakamatwa baada ya kutupa chanjo za Corona

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Waendesha mashtaka nchini Misri wametoa amri ya watu watatu kukamatwa baada ya maelfu ya dozi za chanjo za corona kutupwa katika mji wa Minya, ambao uko kilomita 200 kutoka kusini mwa mji wa Cairo.

Picha zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii wiki iliyopita zikionesha masanduku ya chanjo ambayo hayajafunguliwa yakiwa yametapakaa katika ukingo wa maji.

Mamlaka imesema ni karibu dozi 20,000 kutoka China- za chanjo ya Sinopharm , zenye thamani ya zaidi ya $300,000 (£220,000), zimepotea baada ya kutunzwa katika kiwango cha joto kilicho sahihi.

Ni 11% ya idadi ya watu wa Misri ndio wamepata chanjo ya uviko 19 huku 6% ndio wamepata dozi kamili.

1633939071000.gif
 
Back
Top Bottom