Moto wazuka kanisani Misri, 41 wafariki

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,023
1,609
Watu 41 wanadaiwa kuuawa na wengine 55 kujeruhiwa baada ya moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme kuzuka katika kanisa la Abu Sifin Coptic katika mji wa Giza, Cairo

Mamlaka zimesema kuwa moto ulizuka wakati waumini 5,000 wakiwa wamekusanyika kwa ajili ya ibada ya Jumapili , na kusababisha mkanyagano

Aidha, Vyombo vya kuzima moto 15 vilitumwa kwenye eneo la tukio kuzima moto huku majeruhi wakikimbizwa katika hospitali za karibu

……………..

Egypt’s Coptic Church, citing the health ministry, has said 41 people were killed and 55 others injured in a fire at a church in the city of Giza, near Cairo.

Egypt’s health ministry earlier said “several” people were killed in the fire at the Abu Sifin Coptic church in the Imbaba neighbourhood on Sunday.

Two security sources told Reuters news agency an electrical fire broke out as 5,000 worshippers gathered for mass, causing a stampede.

Fifteen fire engines were dispatched to the scene to put out the flames while ambulances ferried the casualties to nearby hospitals.

President Abdel Fattah el-Sisi spoke by phone with the Coptic Christian Pope Tawadros II to offer his condolences, the president’s office said.

“I have mobilised all state services to ensure that all measures are taken,” he said on his Facebook page.

Fire services later said the blaze had been brought under control

Source: Al Jazeera
 
Hujuma.Haina kupepesa macho wala kutikisa masikio.Wafuasi wa dini fulani huwa ni miuaji.
Una uhakika hayo mambo yenu ya kum point mtu au dini fulani ndyo yanasababisha machafuko hata mm ukinisingizia kitu ambacho sijafanya lazima nikukwarue mnajiona nyie ndyo hamfanyi dhambi wakati kila kukicha huko hao mapadre wenu wanalawiti watoto kuna kipindi mpaka papa wenu akawa anawaombea msamaha
 
Una uhakika hayo mambo yenu ya kum point mtu au dini fulani ndyo yanasababisha machafuko hata mm ukinisingizia kitu ambacho sijafanya lazima nikukwarue mnajiona nyie ndyo hamfanyi dhambi wakati kila kukicha huko hao mapadre wenu wanalawiti watoto kuna kipindi mpaka papa wenu akawa anawaombea msamaha
Andika kwa utulivu.Huna kituo,kiulizo wala kielekezi cha mstari unaanzia wapi!Punctuation!
 
Hujuma.Haina kupepesa macho wala kutikisa masikio.Wafuasi wa dini fulani huwa ni miuaji.
Ndugu yangu
Mimi ni Mkristo pia ni Mwanafunzi wa Yesu.

Nakusihi uondoe hizi tuhuma kwa sababu zinacbochea hasira za kidini. Watu wabaya kuliko wote duniani hakuna. Propaganda zisitutoe kwenye utu
 
Wakristo 35 wamefariki dunia na wengine 45 kujeruhiwa katika mji wa Gazi nchini Misri kwa kile kilichodaiwa kuwa Ni bomu la kurushwa kwa mkono kulipuka kanisani wakati ibada ya jumapili ikiendelea.

=======

Watu 41 wamefariki dunia na wengine wengi kujeruhiwa nchini Misri baada ya kutokea kwa mlipuko wa moto kwenye kanisa moja jumapili ya August 14 mjini Giza wakati wa ibada ya kawaida ya jumapili inayojumuisha zaidi ya waumini 1000.

Uchunguzi wa awali unaonesha chanzo cha moto huo kuwa ni hitilafu ya umeme kwenye mojawapo ya viyoyozi vinavyopatikana kwenye ghorofa ya pili. Hii ni kwa mujibu wa Waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo.

Inaripotiwa kuwa mkanyagano mkubwa ulitokea baada ya mlipuko huo na namba kubwa ya watu ilivuta moshi mchafu, hali iliyopelekea kutokea kwa vifo hivyo. Idadi kubwa ya watu waliofariki ni watoto.

Kama sehemu ya kifuta machozi, serikali itatoa paundi 100,000 za nchi hiyo ambazo ni zaidi ya milioni 12 za kitanzania kwa familia zote zilizopoteza wapendwa wao kwenye kadhia hii.

Giza ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Misri, unapatikana karibu kabisa na mto wa Nile kutoka mji wa Cairo.

Chanzo: Reuters

FB_IMG_1660493325030.jpg
FB_IMG_1660493322173.jpg
FB_IMG_1660493318409.jpg
 
Mungu azipe pumziko la milele roho za marehemu wote, na majeruhi wapate nafuu ya haraka Amina.
 
Back
Top Bottom