Misri: Waandishi watatu waachiwa huru kutoka jela

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,456
FRoNI6uXsAI625t.jpg
Mamlaka za Serikali Nchini Misri imewaachia huru waandishi wa habari watatu ikiwa ni mwendelezo wa Rais wa Nchi hiyo, Abdel Fattah el-Sisi kumalizana na wakosoaji wake.

Waandishi hao ni Ammer Abdel-Moneim, Hany Greisha na Essam Abdeen waliruhusiwa kutoka jela jana Mei Mosi, 2022 baada ya kuwa kizuizini gerezani kwa mwaka mmoja na nusu wakikabiliwa na kesi mbalimbali.

Kiongozi wa Umoja wa Waandishi wa Misri, Khaled el-Bashy aliposti picha mtandaoni akiwa na waandishi hao.

Waliachiliwa huru wakisubiri uchunguzi wa mashtaka ya awali ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii na kujiunga na "kundi la kigaidi" chenye uhusiano na Muslim Brotherhood.

Misri ilitaja Kundi la Brotherhood kuwa shirika la kigaidi mwaka 2013, lakini kuhusu wakosoaji wa kisiasa ambao wako jela wameendelea kubaki huko, hawajapewa msamaha.

Misri.JPG


Source: Aljazeera
 
Back
Top Bottom