Misri, Tunisia na sasa Iran mfano wa "mapinduzi ya kizalendo" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Misri, Tunisia na sasa Iran mfano wa "mapinduzi ya kizalendo"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by saggy, Feb 15, 2011.

 1. s

  saggy Senior Member

  #1
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 153
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Vuguvugu la Mageuzi linaloendea Mashariki ya kati ni Ishara ya Mwanzo wa mfumo mpya Utawala ambao Kidemokrasia inatawaliwa Nguvu ya Umma ambayo haitokani na Uchaguzi a mfumo wa Kisiasa bali "Mapinduzi ya Kizalendo" Mfumo huu utakomesha tabia ya Wanasiasa kutumia vibaya nafasi zao kwa kusingizia Demokrasia kukandamiza Matakwa ya Wananchi walio wengi.

  Sasa naitisha " Mapinduzi ya Kizalendo kwa Watanzania Wote",Tukomeshe na kuwafukuza Wanasiasa ambao wamevaa Joho la Demokrasia ya Vyama huku wakinufaisha wenyewe bila kujali matatizo ya Wanachi,kwa mfano angalia katikati ya matatizo makubwa ya Kiuchumi yanayokabili nchi yetu sasa (Mfano matokeo ya Mgao wa Umeme na nk ) WANASIASA ambao ni Wabunge wetu wanalipana MILION 90 kila mmoja kukunua Magari ya Kifahari na Kukatiwa Bima katika Hospitali Binafsi huku wakituacha Mamilioni ya watanzania tukiugulia kwenye Hospitali zisizo na Madawa,Vitanda na Madaktari na wala Vifaa vya Kisasa vya Maabara!Hawa ni WANASIASA,waliovaa KOTI la Demokrasia kutudanganya.

  Natangaza kwamba Wananchi tumechoka na Wanasiasa,tumechoshwa na maneno yao,tunaomba watoke kama wameshindwa na haya ndio "Mapinduzi ya Kizalendo" ninayoitisha kufanyika Tanzania nzima.

  Bila Mapinduzi haya Taifa letu litadidimizwa katika Umaskini kwa Miaka mingi sana huku tukishuhudia WANASIASA Wakila na Kugawana mema ya nchi yetu na Rasilimali zetu.

  Shime Watanzania Wenzangu,Tuwafukuze wanasiasa hawa kwakuwa wametusaliti kwa kusahau kero zetu na Matatizo yetu na kushughurikia Matumbo yao tu.


  Shime Watanzania,tusidanganyike na maneno yao,mara kATIBA,Mara hili mala lile,SISI Wanachi ndio DOLA na tunasema WATOKE Kama wameshindwa kutekeleza matazamio yetu.


  Naitisha Maandamano makubwa nchi nzima kwa kuanzia Mikoa ya Mwanza,Arusha,Mbeya na Kigoma na baadaye nchi nzima ili kuangusha Utawala huu ambao umetusaliti wanachi Maskini na kuanzisha enzi mpya ya "Nguvu ya Umma" tarehe ya KUANZA MAANDAMANO Haya ni 19/02/2011
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  TUNATAKA MCHAKATO WA KATIBA MPYA NA TUME HURU
  YA UCHAGUZI BUNGENI SASA HIVI!!!


  Enyi Ndugu Waheshimiwa viongozi wetu

  akina Kikwete, Dr Slaa, Prof Lipumba, Mbowe, Julius Mtatiro, Zitto Kabwe, Mbatia, Dr Mvungi, Prof Baregu, Prof Mukandala, Dr Bana, Dr Azaveli, Mama Nkya, Ndg Mgaya, Makwaia wa Kuhenga, Jenerali Ulimwengu, Reginald Mengi, Pius Msekwa, Fredrick Sumaye Fredrick Msuya, John Malecela, Mama Anna Makinda, Sheik Issa Bin Simba, Mhe Iddi Simba, Maaskofu na Wachungaji wote nchini, Denis Mwamnyange, Said Mwema, The Othma's, Tundu Lissu, Sitta, Mwakyembe, Mzee Mkapa, Mzee Salim Ahmed Salim, Mzee Sinde Warioba, Mzee Butiku, Prof Sarungi, Selasini, Ole Sendeka, Tido Mhando, Mama Maria Nyerere, Mama Karume, Selelii, Prof Bangu, Dr Matumaini, Bashe, Celina Kombani, Kafulila, Hamad Rashid, Regia, Lukuvi, Mama Maghimbi,Mama Anna Abdala, Pombe Magufuli, Mstaarabu wa Siasa Tanzania - Dr Mohammed Shein, Salmin Amour, Godbless Lema, Mzee Mwanakijiji, Maxence Melo, Candid Scope, Fareed, Mwakalebela, Mnyika, Halima Mdee, viongozi wote wa serikali za wanafunzi vyuoni ... na wengine wengi wengi wengi tu, sisi kama vijana wa nchi hii sasa hivi tunawaulizeni nyote kwa pamoja kwamba ...

  ... suala letu la michakato wa kujiandikia KATIBA MPYA na kuunda Tume Huru ya Uchaguzi ZINAANZA LINI BUNGENI???
   
 3. s

  saggy Senior Member

  #3
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 153
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  WAKATI NI SASA HAKUNA KUNGOJA!!!!

  Mimi nasema hawa WATOKE ni WAONGO na wametusaliti wananchi na wamekalia maneno tu,nasema Watupishe watokee,nimechoka na WANASIASA,Dunia nzima imechoka na mfomo wa wanasiasa,Katiba sawa lakini ni kifungu gani cha Katiba kinwaruhusu kula Rushwa,kuingia Mikataba Mibovu na etc.

  Dawa yao ni Kuwaondoa madarakani kwa Maandamano makubwa kama walivyofanya Wenzetu,leo nasema nimechoka na Wanasia,how LONG WE WILL WAIT? Tungoje katiba kuandikwa lini?

  1.Watoto zaidi ya 250,000 walipata daraja la IV na 0 kwenye Mitihani yao ya Kidata cha nne kutokana na kupata Elimu duni kwenye shule za kata wangoje mapaka lini?

  2.Mamilioni ya Vijana wasio na AJIRA Wanaolala na hawajua maisha yao yatakuwaje nao wangoje mpaka lini Katiba iandikwe?

  3.Wakulima wasio na masoko ya uhakika na Pembejeo za kilimo wangoje mpaka lini?

  4. Maelfu ya akina mama waja wazito wanaokufa kwa kukosa Huduma bora za Afya wakati wa Kujifungua wangoje mpaka lini?

  5.Walimu wanaolipwa mishahara midogo,mazingira duni ya kazi na mdai yao kutolipwa kwa muda mrefu wangoje mapaka lini?

  6.Mgao wa umeme unaondelea sasa uliosababisha Mfumuko wa Bei na kupunguza uzalishaji wa Taifa na kutuingiza kwenye umasikini mkubwa ungoje Katiba mpya kuandikwa hata lini?

  7.Wanafunzi wa Vyo vya Elimu ya Juu wanaopoteza muda kwa kuhangaika kwakuwa Pesa ya kujikimu haitoshi na mazingira magumu ya kusomea na hawana uhakika wakimaliza watapata Ajira au la Wangoje mpaka lini?

  8.Polisi,askari magereza wanaoishi maisha ya dhiki kwa nao wangoje mpaka lini?


  WAKATI NI SASA,HAKUNA KUNGOJA!!!1
   
 4. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mie nakuunga mkono mia kwa mia tulikomboe taifa letu kutoka na maangamizi ya uhai wa taifa shauri ya watawala mafisadi wote na CCM kwa ujumla wao walarushwa wakubwa hawa.

  Ukombozi wa nchi hii unatakiwa kufanywa umma.

  Dawa sahihi kwa uhai wa taifa hili sio tu kuleta mapinduzi ya kizalendo kuondoa utawala mbovu madarakani, bali ukombozi utakamilika kwa kuipiga marufuku CCM na kufuta ofisi zake zote kama walivyofanya Tunisia kwani CCM ndio chanzo cha kufa kwa uhai wa nchi kiuchumi naufidhuli dhidi ya demokrasia ya umma, na jamii kujaa umaskini na kuoza kutokana na ufisadi.
  Yafaa viongozi wake wakamatwe na hukumu kali ya umma ipite juu yao kama China wawafanyiavyo wala rushwa na wahujumu mfano wa CCM.
   
 5. s

  saggy Senior Member

  #5
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 153
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Naunga mkono hoja 100% kwa mia mkuu
   
 6. m

  mbombongafu Member

  #6
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  niambieni tunakusanyikia wapi?
   
 7. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,692
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Jamani, kwanza tupate maelezo kuhusu huyu muitisha maandamano. Amejiandaa vipi kuongoza hayo maandamano. Ujumbe wake anaupeleka kupitia hapa JF peke yake au ana mikakati mingine zaidi? Na ikiwezekan a kuwang'oa madarakani nini kinafuata? Nani atajaza hilo ombwe? Ni malaika au kundi lingine la wanasiasa? Tafakari kwanza.
   
Loading...