Misri namba moja Africa kwa nguvu za kijeshi

Soma unielewe wewe mimi sijakataa kuhusu nguvu za kijeshi za Misri mimi nimeongelea ari na uwezo wa kuzitumia hizo nguvu.

Goliath kwenye bible alikuwa na nguvu nyingi mno pande la mtu miraba mine amevalia mavazi ya chuma huwezi mpiga upanga ukamuingia lakini Daudi kakijana kadogo sana hakuwa na chochote zaidi ya kombeo na jiwe lakini alilitumia vizuri kwa ustadi akamuangusha Goliath akamkata kichwa.

I walk the talk naongea nikiwa na uhakika niliongelealo hivyo vita nilishiriki bro

Ni kweli nchi zimeendelea ki technologia ujue hata sisi hatukusimama tumeendelea pia japo hatuwezi wafikia Wamarekani
Umetumia vigezo gani kusema jeshi letu ni bora kuliko Misri?Yaani unaenda vitani,unataka umpangie adui namna ya kupigana?
Kunapokuwepo na vita,kila upande unatumia uwezo wake wote kuhakikisha inashinda,na ndio nguvu ya kijeshi inayozungumziwa hapa!

Hizo nyingine ni porojo tu!Hata mifano ulitoa ya Alishabaab kuwatesa kenya haina mantiki kabisa!
Vita ya kigaidi ni ngumu kupigana kwa maana adui humjui maana anatokana na wananchi wako wenyewe!Yaani ukipigana vita ya kigaidi kama unavyopambana vita na nchi nyingine basi utamaliza raia wako hata wasiokuwa na hatia!Maana hawa jamaa ni raia na wanajificha kwenye raia mpaka wakati wa kuattack!
Kwahiyo huo mfano wako ni mfu kabisa!
 
Misri wana maendeleo hata kwa huduma za usafiri wa anga, elimu na kilimo cha umwagiliaji. Misri ina zalisha madaktari wengi sana kila mwaka na wengi wanapata ajira Ulaya na Uarabuni.
Bila kusahau misaada mikubwa ya kijeshi kutoka Marekani.
 
Umetumia vigezo gani kusema jeshi letu ni bora kuliko Misri?Yaani unaenda vitani,unataka umpangie adui namna ya kupigana?
Kunapokuwepo na vita,kila upande unatumia uwezo wake wote kuhakikisha inashinda,na ndio nguvu ya kijeshi inayozungumziwa hapa!

Hizo nyingine ni porojo tu!Hata mifano ulitoa ya Alishabaab kuwatesa kenya haina mantiki kabisa!
Vita ya kigaidi ni ngumu kupigana kwa maana adui humjui maana anatokana na wananchi wako wenyewe!Yaani ukipigana vita ya kigaidi kama unavyopambana vita na nchi nyingine basi utamaliza raia wako hata wasiokuwa na hatia!Maana hawa jamaa ni raia na wanajificha kwenye raia mpaka wakati wa kuattack!
Kwahiyo huo mfano wako ni mfu kabisa!
Bora umemuuliza wewe
 
Ukubwa wa pua sio wingi wa makamasi wewe.Hizi nchi kama utakuwa unaongelea mavifaa tu utakuwa sawa tu lakini kwenye medani za kivita ujasiri wa guerrilla war haziko sawa.

Ni sawa na upigane na mwenzako amevaa ring box na kwa mbele ameweka ma vyuma ya kukuumiza na amevaa helmet ila hana mbinu za kurusha ngumi pamoja na wewe uko peku peku.

Ukitaka kujua Tanzania tuko vizuri angalia medani za kulinda amani na pia chungulia vita vya Kagera sina hakika muanzisha mada ulishazaliwa?

Vita ya Kagera na umasikini wetu tulipigana kwa miezi minne tu na siku 18 hadi kuisafisha nchi ya Uganda na kumkimbiza Idi Amini hakuna nchi duniani yenye record kama hii.Sisi nikuambie kitu askari wetu japo tulikuwa hatujawahi pigana vitani wakati huo lakini askari wetu constantly walikuwa kwenye mafunzo walipokuwa wanasaidia nchi zingine kujikomboa kwa wakoloni.

Nikuambie tu kitu marekani si lolote si chochote maguvu yao yako kwenye mavifaa hasa vita vya anga wanachofanya wanakutwanga kwa mabomu na makombora na ndege zao zikiwa juu ambapo huwezi kuzitungua na wana uwezo wa kukupiga wakiwa kwao bila kukufuata kwako.Wakaisha kutwanga kwa mabomu ndio sasa wanajifanya wananza vita vya ardhini lazima washinde.

Nina uhakika wamarekani ni waoga mno askari wao kwani wakiondoka wanaaga watarudi.Ona Marekani walivyotolewa berenge Vietnam.Ikitoea marekani tukapigana nao tukaruhusiwa tupigane kavu kavu porini wasitumie anga tunawapiga vibaya sana.

Tukija Kenya ni kweli sana vifaa vya kisasa kuliko sisi lakini ari ya wapiganaji wao inanitia shaka maana hawajashiriki vita vyovyote zaidi ya MAU MAU ambapo kwa kweli MAU MAU nawavulia kofia.Wangekuwa na maarifa ya medani wasingesumbuliwa na ALSHAABAB kwa karibia muongo mmoja.

Ona jinsi mauwaji ya West Gate yalivyotokea jamaa walifanya uharamia wakaondoka kiulani bila kukamatwa iko shida
Vita huwa ni ari na solidarity Marehemu Simba wa Yuda mzee Rashidi Kawawa alisemaga wakati wa vita vya Kagera vita havina nchi ndogo ona nchi ya Korea inavyoitoa Makamasi Marekani na udogo wake hata mkoa wa Tabora na Mwanza ni kubwa kuliko eneo la nchi yao.
Umeandika propaganda tupu.
 
Back
Top Bottom