Misri kuipiga Ethiopia?

Swat

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
4,198
1,968
Source: BBC NEWS/Swahili this eveing. Ni mkataba wa kikoloni ambao haujali haki za binadamu hata kidogo!. Mkataba wa kikoloni uliimilikisha Misri asilimia 85 ya umiliki wa mto Nile. Na kwa kuogopa kidogo iliipa Sudan umiliki wa asilimia 15!. Ajabu nchi zilizobaki zozote ambazo Mto Nile unatokea au unapita hazikupewa umiliki au haki za matumizi kwenye mkataba huo!. Ethiopia imeamua kutumia maji ya mto huo kuzalisha umeme. Misri inapinga hilo na imesema leo kwambaitatumia nguvu yeyote ikisimamia mkataba ilioingia kati yao na waingereza!.Walishawahi kututisha hivyo Tanzania wakati Mheshimiwa Lowasa ni Waziri wa Maji lakini tuliendelea na mipango yetu ya maendeleo. Huu naona ni sawa kabisa na mkataba wa waingereza na wajerumani pale Ziwa Nyasa. Waafrika tupinge mikataba ya kikoloni ambayo inanyima haki za msingi za baadhi ya waafrika.
 
Bunge la Ethiopia, limefutilia mbali mkatabauliosaniwa wakati wa utawala wa kikoloni, ulioipa Misri na Sudan, haki ya kutumia maji mengi ya mto Nile.
Serikali ya Ethiopia, imehoji kuwa mkataba huo ulioidhinishwa mwaka wa 1929, umepitwa na wakati.
Serikali ya Misri, imepinga vikali hatua hiyo na imekasirishwa nauamuzi wa Ethiopia wa kujenga bwawa la maji, katika mto huo wa Nile, ikidai kuwa itapunguza maji yake.
Siku ya Jumatatu rais Mohamed Morsi, alisema hataki vita, lakini anachunguza njia zote.
Awali, nchi sita zilizoko katika eneo la bonde la mto Nile, ikiwa ni pamojana Ethiopia, zilisaini mkataba ambao unafutilia mbali mamlakaya Misri ya kuzuia ujenzi wa bwana katika mto Nile.

Source: bbc
 
hawa misri wa***e kabisa sasa maji yanatoka huku na yanapita katika nchi kadhaa kwanini wajimilikishe si basi wangejuja na kulibeba ziwa victoria na vyanzo vyote vya mto nile vihamie kwao...
 
ITV Tanzania
Bunge la Ethiopia, limefutilia mbali
mkataba uliosaniwa wakati wa utawala
wa kikoloni, ulioipa Misri na Sudan, haki ya
kutumia maji mengi ya mto Nile. Serikali ya Ethiopia, imehoji kuwa
mkataba huo ulioidhinishwa mwaka wa
1929, umepitwa na wakati. Serikali ya Misri, imepinga vikali hatua hiyo
na imekasirishwa na uamuzi wa Ethiopia
wa kujenga bwawa la maji, katika mto
huo wa Nile, ikidai kuwa itapunguza maji
yake.
Siku ya Jumatatu rais Mohamed Morsi,
alisema hataki vita, lakini anachunguza
njia zote.

Bunge la Tanzania Limeshindwa nini kuvunja Mikataba ya Kifisadi serikali inayosaini?????????

OMBI MAALUMU:
Naomba Mods msipeleke hii mada jukwaa la Kimataifa,ina Maslahi ya Kitaifa na hapa ndipo watu wengi wanaiona!
 
Tukipata Serikali yetu ya Tanganyika tutavunja mikataba yote iliyoingia serikali ya Tanzania
 
Aiseee Misri hawatakubali na wanaweza hata kutumia nguvu.. Ila nadhani wanatakiwa waelewe kwamba Haki walionayo wao ndo wanatakiwa kuwa nayo Waethopia..
 
wanaangalia possible ways za kuteketeza storkpile ya milipuko waliyonayo, so sad wanaweza kuamua iteketeze bin adamu.

wamisri noma, kuanzia wananchi sasa wanataka na jeshi nalo lipambane.
 
Aiseee Misri hawatakubali na wanaweza hata kutumia nguvu.. Ila nadhani wanatakiwa waelewe kwamba Haki walionayo wao ndo wanatakiwa kuwa nayo Waethopia..

wakianza kupigana, sisi tuharakishe mpango wa kuyaleta Dodoma maji ya ziwa victoria, kwa hili lazima kunguru ajipatie mlo wake kiulainiiiiii.
 
wakianza kupigana, sisi tuharakishe mpango wa kuyaleta Dodoma maji ya ziwa victoria, kwa hili lazima kunguru ajipatie mlo wake kiulainiiiiii.

Ha ha ha.. Unajua wengi hawaelewi hili lakini Wamisri wanatakiwa wamshukuru sana Mwl. Nyerere.. Mwaka 1967 walikuja waisraeli hapa wakampa ofa Mwalimu ya kujenga mifereji ya maji toka ziwa Victoria mpaka Mikoa ya kati yaani Dodoma na Mikoa mingine ya jirani yake.. Lengo la Waisraeli ilikuwa ni kukata flow ya maji Misri.. Mwalimu alikataa na ndo ikawa salama yao..
 
Aiseee Misri hawatakubali na wanaweza hata kutumia nguvu.. Ila nadhani wanatakiwa waelewe kwamba Haki walionayo wao ndo wanatakiwa kuwa nayo Waethopia..
Siku zote hujiuliza kama mto Nile ni mali ya Misri peke yake na nchi nyingine ni watazamaji tu,sijui ingekuwaje kama mto Nile ungekuwa unaanzia Misri si ingekuwa wanauza maji kama mafuta.
Pia najiuliza ule mradi wa maji wa Lowasa wa kuchukua maji ziwa Victoria hadi mikoa ya Shinyanga na Tabora imefikia wapi kwani huo mradi nao ulikoromewa sana na Misri
 
nilisikiliza hotuba ya museven jana pia aliwasapot waethiopia akasema ili nchi kuendelea kiviwanda na umeme lazima tutumie ayo maji si misri peke yake,umefika wakat nchi zetu za mashariki tuamke,awa wa misri washatunyanyasa sana kwa mikataba yao tya kikolon
 
Misri hana jeuri ya kuipiga Ethiopia hata asaidiwe na Waarabu wote
 
ITV Tanzania
Bunge la Ethiopia, limefutilia mbali
mkataba uliosaniwa wakati wa utawala
wa kikoloni, ulioipa Misri na Sudan, haki ya
kutumia maji mengi ya mto Nile. Serikali ya Ethiopia, imehoji kuwa
mkataba huo ulioidhinishwa mwaka wa
1929, umepitwa na wakati. Serikali ya Misri, imepinga vikali hatua hiyo
na imekasirishwa na uamuzi wa Ethiopia
wa kujenga bwawa la maji, katika mto
huo wa Nile, ikidai kuwa itapunguza maji
yake.
Siku ya Jumatatu rais Mohamed Morsi,
alisema hataki vita, lakini anachunguza
njia zote.

Bunge la Tanzania Limeshindwa nini kuvunja Mikataba ya Kifisadi serikali inayosaini?????????

OMBI MAALUMU:
Naomba Mods msipeleke hii mada jukwaa la Kimataifa,ina Maslahi ya Kitaifa na hapa ndipo watu wengi wanaiona!

watu huangalia kwenye menu, ni uzi upi mpya umeingia na kuufungua. labda kama uzi umewekwa kule ambako kuna watu maalum ndo hautaonekana. ondoa hofu mkuu
 
Siku zote hujiuliza kama mto Nile ni mali ya Misri peke yake na nchi nyingine ni watazamaji tu,sijui ingekuwaje kama mto Nile ungekuwa unaanzia Misri si ingekuwa wanauza maji kama mafuta.
Pia najiuliza ule mradi wa maji wa Lowasa wa kuchukua maji ziwa Victoria hadi mikoa ya Shinyanga na Tabora imefikia wapi kwani huo mradi nao ulikoromewa sana na Misri

Mkuu ninadhani hawa viongozi wetu ama waoga au wanapata kitu toka kwa Misri.. Kwanza kwa akili ya kawaida huwezi ukaendelea kuuheshimu mkataba uliongiwa na wakoloni miaka karibu mia iliopita ambayo inahusisha rasilimali za yako.. Ethopia wametangulia inabidi wengine tuchukue nafasi hii.. Kuna wakati walijaribu naona wakalainishwa na Wamisri wakalainika..
 
Back
Top Bottom