Source: BBC NEWS/Swahili this eveing. Ni mkataba wa kikoloni ambao haujali haki za binadamu hata kidogo!. Mkataba wa kikoloni uliimilikisha Misri asilimia 85 ya umiliki wa mto Nile. Na kwa kuogopa kidogo iliipa Sudan umiliki wa asilimia 15!. Ajabu nchi zilizobaki zozote ambazo Mto Nile unatokea au unapita hazikupewa umiliki au haki za matumizi kwenye mkataba huo!. Ethiopia imeamua kutumia maji ya mto huo kuzalisha umeme. Misri inapinga hilo na imesema leo kwambaitatumia nguvu yeyote ikisimamia mkataba ilioingia kati yao na waingereza!.Walishawahi kututisha hivyo Tanzania wakati Mheshimiwa Lowasa ni Waziri wa Maji lakini tuliendelea na mipango yetu ya maendeleo. Huu naona ni sawa kabisa na mkataba wa waingereza na wajerumani pale Ziwa Nyasa. Waafrika tupinge mikataba ya kikoloni ambayo inanyima haki za msingi za baadhi ya waafrika.