Misosi Ya Kibongo

Nzokanhyilu

JF-Expert Member
Feb 19, 2007
1,078
93
Hivi wenye maduka ya misosi ya kibongo kupitia Bakhressa, kuna mayai ya kienyeji? Mimi haya mayai ya Sainsbury sijui Asda yanaharibu tu ulimi hamna ladha tumbo kuvimba. Mimi nataka mayai ya kienyeji, ukilipasua ile york inaonekana proper yellow. Je yapo?
 
iiiiiiiihi, Ng'hungurume, kinehe egeteh?!

naona umeanza kuhofia afya yako mapema; mayai ya kopo, nyanya za kopo, mchicha wa kopo, vitunguu vya kopo, dagaa wa kopo, maembe ya kopo, nanasi za kopo, n.k. 700 kutoka kwenye masupa maketi yenu huko. Pole sana, hayo mayai yasiyo jogoo sijui ubaya wake ila nina uhakika mayai ya kuku wa kienyeji ni bomba zaidi kwa miili yetu, sema huwa yana ka harufu fulani hivi (kama sea water hivi...!!!), sijui kama huwa unakashitukia,mimi huwa kanani put off sometimes....
BTW, je umesha kula mayai ya bata?... yana afya nzuri na ni makubwa zaidi, ila sina uhakika kama unaweza kuyapata huko ulaya... hapa bongo ni kibao sema watu hawajayashitukia tu, na production rate yake ni ya nguvu, si unawajua tena bata jinsi walivyo.... lol...

Anyway, kuna huyu kuku wa kienyeji wa jirani hapa nimempiga picha leo nadhani atakuriwadha kinamna kumwona anataga yai... !! :), walau upate mawili matatu ya kufikirika!! lol

313fwcm.gif

Nzoka, angoh shokagi kokaya mlye shinonu!!
 
Kuna Kampuni Moja Nimesahau Jina Lake Labda Wiki Ijayo Naweza Kukutafutia Jina Na Contact Zake Hawa Huwa Wanatuma Na Kuuza Mayai Hayo Na Vitu Vingine Vya Asili Kwa Watu Wa Ulaya Na Sehemu Zingine Ambazo Watanzania Huishi Kwa Wingi

Nitakutafutia Nikupe Contact Zao Wanaweza Wakawa Wanakutumia Hivyo Vitu

Ahsante
 
We SteveD, hako kaharufu labda wewe ulikuwa unakula mayai vinza.
Huyo sio kuku wa kienyeji. Kuku wa kienyeji lazima awe amenyonyoka na hajanona namna hiyo, labda awe anakula mtama for breakfast. Cheki kuku anadonyoa donyoa barabarani. Aisee Bata sijaona sainsbury, ila wanauza maini ya kuku.
060208_nigeria_bird_vlrg_5a.widec.jpg

Juzi niko uswahilini nanunua chairfire si nikaona maza anapewa nyama ya njiwa. Nikauliza hivi wapo? wakasema spesho oda. Wazungu sijui wakajua mi natoka kijijini, wakaniambia kuna Quail...sasa si ni Kwale hao? Mwanawane ulimi ulilainika. Ila stoki ikawa imeisha, sasa inabidi nipige oda. Walinikumbusha enzi zileee, unamkimbiza kwale mpaka anachoka.

SteveD, Wanaigeria wanaleta mihogo, sato wanapatikana, maharage na makande yapo, hadi mafanta yasiyo na kipimo cha sukari. Natoshokaga ngosha.

Ila nimemiss siku ile kijiji chetu kiliwapiga bao katika kucheza ngoma za bulabo. labda mwaka huu mtashinda. Ila mlipendeza na hizo pamba za yellow yellow.
nyanghanga-65.3.jpg

Shy, hao jamaa wanaoleta mayai ya kienyeji, yamewekewa mhuri wa tarehe? Maana unaweza kufungua kayai ukakutana na tunyoanyoa.
 
Hivi wenye maduka ya misosi ya kibongo kupitia Bakhressa, kuna mayai ya kienyeji? Mimi haya mayai ya Sainsbury sijui Asda yanaharibu tu ulimi hamna ladha tumbo kuvimba. Mimi nataka mayai ya kienyeji, ukilipasua ile york inaonekana proper yellow. Je yapo?

We lazima utakuwa uko Uingereza...
 
Hivi wenye maduka ya misosi ya kibongo kupitia Bakhressa, kuna mayai ya kienyeji? Mimi haya mayai ya Sainsbury sijui Asda yanaharibu tu ulimi hamna ladha tumbo kuvimba. Mimi nataka mayai ya kienyeji, ukilipasua ile york inaonekana proper yellow. Je yapo?

Mkuu ukiingia Asda au Tesco na Sainsbury's kwenye sehemu palipo mayai angalia yale mayai ambayo yana maelezo kwamba ni "Free Range"

Ila ukihitaji bidhaa za asili basi maeneo ni Upton Park- market, Walthamstow- market ambayo ipo high street karibu na Sainsbury's na Peckam high street-south London.

Ila kuhusu Peckam uwe mwangalifu, risasi inaweza kutokea upande wowote na watu hufukuzana na kukatiza barabara wakikimbizana huku visu vikipepea, maana vurugu baina ya gangsters haziishi.
 
We SteveD, hako kaharufu labda wewe ulikuwa unakula mayai vinza.
Huyo sio kuku wa kienyeji. Kuku wa kienyeji lazima awe amenyonyoka na hajanona namna hiyo, labda awe anakula mtama for breakfast. Cheki kuku anadonyoa donyoa barabarani. Aisee Bata sijaona sainsbury, ila wanauza maini ya kuku.
.....Nzoka, je unawajua jina lake hao?... wanaitwa 'kuchi' !!
Wanapigana hao, yaani usipoangalia wanaweza kuwa na ugonvi na kuku wa jirani wiki nzima, au hadi mmojawao mauti imkute!

Juzi niko uswahilini nanunua chairfire si nikaona maza anapewa nyama ya njiwa. Nikauliza hivi wapo? wakasema spesho oda. Wazungu sijui wakajua mi natoka kijijini, wakaniambia kuna Quail...sasa si ni Kwale hao? Mwanawane ulimi ulilainika. Ila stoki ikawa imeisha, sasa inabidi nipige oda. Walinikumbusha enzi zileee, unamkimbiza kwale mpaka anachoka.
...nini kumkimbiza, mimi bado nina ndoto mbaya baada ya kutolewa baruti na jogoo kama huyu hapa chini:

jogoobaruti.gifSteveD, Wanaigeria wanaleta mihogo, sato wanapatikana, maharage na makande yapo, hadi mafanta yasiyo na kipimo cha sukari. Natoshokaga ngosha.
..... Nzoka, naomba unipatie konneksheni huko ng'wanone, ninampango wa kuanza ku ekspoti michembe na matobolwa huko kwenu ughaibuni, can you help pls?!! :)

Ila nimemiss siku ile kijiji chetu kiliwapiga bao katika kucheza ngoma za bulabo. labda mwaka huu mtashinda. Ila mlipendeza na hizo pamba za yellow yellow.
.... El Nino bana, yote hayo yalisababishwa na el nino, mavuno mwaka huo hayakuwa mazuri, majaruba yote yalifulika na mchele tulio uza mwaka huo hivyo haukuwa mwingi. si unajua tena, maandalizi mengi ya ngoma zetu hufana kutegemea na mauzo. Ila maleba (costumes) hamtuwezi, mwaka kesho tunampango wa kuomba kibali kutoka kwa meya wenu Ken Livingston ili tupate visa ya group letu kuweza kuja shiriki Nottinghill carnival huko mliko... je, unaushauri gani ndugu, nasikia bunduki huko nje nje?!!

Shy, hao jamaa wanaoleta mayai ya kienyeji, yamewekewa mhuri wa tarehe? Maana unaweza kufungua kayai ukakutana na tunyoanyoa.
......aaah, mimi nilifikiri hiyo ndiyo bomba, yaani unakula kuku na yai kwa wakati mmoja!! lol :)
 
.....Nzoka, je unawajua jina lake hao?... wanaitwa 'kuchi' !!
Wanapigana hao, yaani usipoangalia wanaweza kuwa na ugonvi na kuku wa jirani wiki nzima, au hadi mmojawao mauti imkute!

SteveD

`Kuchi` neno tata baba, usilitoe kihivyo
 
...nini kumkimbiza, mimi bado nina ndoto mbaya baada ya kutolewa baruti na jogoo kama huyu hapa chini:

lovely...hiyo picha cha kukimbizwa na kuku imenikumbusha kisa cha "pazi na jogoo" kwi kwi kwi kwi
 
.....Nzoka, je unawajua jina lake hao?... wanaitwa 'kuchi' !!
Wanapigana hao, yaani usipoangalia wanaweza kuwa na ugonvi na kuku wa jirani wiki nzima, au hadi mmojawao mauti imkute!

SteveD

`Kuchi` neno tata baba, usilitoe kihivyo

Mama, naomba unielezee... neno kuchi lina maana gani iliyo batili. (kama ni too sensitive naomba uniwekee kwenye PM au liweke kwenye jukwaa la lugha) Ahsante.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom