Misingi ya Wakoloni Ndiyo iliyofikisha Dini hapa Zilipo. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Misingi ya Wakoloni Ndiyo iliyofikisha Dini hapa Zilipo.

Discussion in 'Jukwaa la Historia' started by babalao 2, Oct 19, 2012.

 1. babalao 2

  babalao 2 JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,218
  Likes Received: 1,270
  Trophy Points: 280
  Ndugu Watanzania kwa kuwa tumeruhusu tofauti ya udini kukita mizizi miongoni mwetu kwa mgongo wa siasa hatuna budi kukaa na kujiuliza nini watu wanataka. Kwanza na tutazame jinsi gani dini hzi zilivyoingia nchini mwetu.

  UISLAMU ulitetwa na kuenezwa na jamii ya kiarabu kutoka ASIA.
  Hawa waliwajaza watu imani ya dini zaidi na kusahau kuwa mtu ana mwili unaohitaji kupata mahitaji yake hivyo kutowafundisha waumini wa dini yao jinsi ya kujikomboa kiuchumi na kielimu dunia kwa kuanzia misikitini. Hii ikapelekea misikiti mingi kukosa miradi midogo na mikubwa kwa maendeleo yao. Mfano SHULE NA HOSPITALI Ambazo ni msingi wa yote. Pia walishindwa kusimamisha mabaraza ya maamuzi na usimamizi wa Rasilimali watu na Vitu. Hii yote imepelekea Taasisi hii kubwa ya kiislamu kukosa miradi ya kujivunia kwa mafanikio yake.

  UKRISTO Kama ilivyo Uislamu umeletwa na watu kutoka ULAYA wakati wa ukoloni.
  Hawa licha ya kueneza imani yao waliwapatia watu elimu dunia ambayo zao lake ni viongozi wengi wa mwanzo waliosaidia kudai uhuru wa AFRIKA. Pia waliwekeza katika mashamba mashule na hospital katika maeneo mengi waliyoishi. Hii ilipelekea maeneo mengi waliyoeneza dini yao ikakubalika walisambaza miradi ya MAJI UMEME NA BARABARA. Utamaduni huu umejengeka miongoni mwa Wakiristo kujitolea mpaka leo kwa miradi ya makanisa yao na kupelekea jamii yote kufaidika na miradi hyo.

  Hata kama SERIKALI imeingia mkataba na dini zote ktk masuala ya miradi yao kama huna miradi utaona mwenzako anapendelewa tu, mfano serikali imeondoa kodi kwa pembejeo za kilimo wasio na mashamba huona ni upendeleo kwa wenye mashamba tena makubwa ilihali fursa ni kwa wote. Mfano mwingine ni kama vile KATIKA JUMUIA YA AFRIKA MASHARIKI KENYA WAMEWEKEZA KTK ELIMU SISI WENGINE TUMEBAKI KULALAMA KWA KUWA HATUKUWEKEZA KTK ELIMU hivyo ni wajibu wetu kuweka mkazo sasa katika elimu na si kuvunja jumuia kupata suluhisho.

  Ushauri wangu ni kwamba taasisi za kidini ziwekeze kwa viongozi wenye taaluma bora na uadilifu ili kujenga waumini wao Kiroho na Kimwili tulete ushindani mzuri ktk kuibua na kuwekeza katika huduma za jamii na kuimarisha UCHUMI KUTOKEA KWENYE NYUMBA ZETU ZA IBADA.

  TUSIBAGUANE TANZANIA NI YA WOTE HATA WAPAGANI WAPO TUISHI KWA AMANI WATU HAWAKULAZIMISHWA KUJIUNGA NA DINI HIZI NI MAPENZI YAO TULINDE TAMADUNI ZETU.
   
Loading...