SoC 2022 Misingi ya ukuaji kiuchumi kwa mtazamo na uzoefu wangu

Stories of Change - 2022 Competition

Omari Frank

Member
Jul 22, 2022
14
4
Mada Kuu: MISINGI YA UKUAJI KIUCHUMI KWA MTAZAMO NA UZOEFU WANGU.

Nimefurahi kupata nafasi ya kueleza jambo kuhusu uchumi kwasababu binafsi nimejikita katika shughuli za kiuchumi kwa muda mrefu hivyo basi ninaweza kuwa na jambo la kusema kwa wadau wa maendeleo na wanajamii Forums.

Kimsingi maendeleo ya kiuchumi huanza na mtazamo aliokuwa nao mtu kichwani mwake, uwezo wa kuona, kuvumbua au kutengeneza fursa, uthubutu na nidhamu.

Kukua kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja ndio msingi haswa wa kukua kwa uchumi wa Taifa zima. Tukianza kuangalia ni namna gani sasa mtu anaweza kukuza uchumi wake basi tutaangalia mambo yafuatayo:-

  1. MTAZAMO
Kuwa na mtazamo chanya na shughuli za kiuchumi kama vile biashara, kilimo na ufugaji. Kujitizama kama mtu ambae unaweza ukajaribu na ukafanikiwa bila kujali ni changamoto kiasi gani utapitia. Mtazamo chanya utakupa nguvu, tumaini jipya na imani thabiti kuelekea kufanya shughuli za kiuzalishaji mali na mwishowe kukuza kipato chako na uchumi wa Taifa kupitia kulipa kodi.


  1. TENGENEZA FURSA
Fursa hutengenezwa, angalia mahali unapoishi na jamii inayokuzunguka kisha angalia ni kitu gani katika mahitaji muhimu ya binadamu hakipatikani hapo au kinapatikana kwa uhaba sana mfano: Huduma za kifedha, Afya, Usafiri, Maduka, Chakula, Mavazi, Elimu, n.k kisha wewe anzisha tena kwa ubunifu wa hali ya juu na matangazo ya kutosha, toa huduma bora pia jali sana wateja wako. Mwanzo unaweza kuwa mgumu sana lakini baadae utakula matunda ya uwekezaji wako.

MFANO: Saluni ya kike unaweza ukaanza kwa kusuka kibarazani tu nje ya nyumba unayoishi, Shule ya malezi ya watoto chini ya umri wa miaka mitano pia unaweza ukaanzisha chini ya mti, kwenye kibaraza cha nyumba au Frame kubwa. Hiyo ni mifano tu ambayo inaonesha kwamba unaweza ukawa hauna mtaji lakini bado ukaanza biashara hata kwa kuunga unga kabisa na inawezekana.

  1. UTHUBUTU
Zungumza na watu waliokutangulia katika biashara au shughuli hiyo, Jifunze mitandaoni, jifunze faida na hasara, raha na changamoto kisha thubutu. Usiogope maneno ya watu kwasababu changamoto huwa hazifanani, maeneo hayafanani kwahiyo changamoto za muuza chipsi wa Mbagala haziwezi kuwa sawa na zile za yule wa Masaki, Hivyo basi anza kidogo kidogo huku ukizisoma changamoto zinazoikabili shughuli yako na kuzitafutia ufumbuzi mapema.
  1. NIDHAMU
kuwa na nidhamu kwa wateja, nidhamu ya fedha na utendaji kwa ujumla. Yote hayo yanaweza kukutoa chini na kukupeleka juu.

MFANO HALISI
Mimi ni mwalimu lakini pia ninamiliki biashara ndogo ndogo za vyakula yaani mabanda ya chipsi pamoja na mama ntilie, Sabasaba na Mawenzi mkoani Morogoro.

Niliiona fursa ya biashara za vyakula katika maeneo hayo ambapo ndipo ninapoishi, licha ya kwamba wapo wengine lakini na mimi nikaja na ubunifu wangu ambao kwa kuzingatia mambo niliyoeleza hapo juu leo hii kwa mwezi ninafunga kiasi ambacho pengine nikisema hapa kila mtu atasema nadanganya.

Na bado nina malengo ya kuendelea kufungua biashara nyingi katika maeneo mengi zaidi ili niendelee kukuza uchumi wangu binafsi na taifa kwa ujumla. Nina mpango wa kuanza kulima mpunga, mahindi na kilimo cha mboga mboga ili vyote viwe vinatumika katika mabanda yangu.

Hakuna lisilowezekana, changamoto ni nyingi sana ikiwemo kukosa mitaji na elimu na ujuzi juu ya shughuli za kiuchumi kama ufugaji lakini penye nia pana njia, unaweza kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kama vile Vocha, Soda na Bia, n.k kisha ukakusanya pesa zako na kuanza kidogo kidogo kwasababu wafanya biashara wengi tunaanza hivyo.

Niishukuru JamiiForums kwa kutoa fursa hii, licha ya kwamba kuna kitita kinashindaniwa lakini naamini kwa sehemu kubwa sana kuna elimu itasambaa na kuwafikia watu wengi juu ya mambo haya ya maendeleo.
 
Upvote 1

Omari Frank

Member
Jul 22, 2022
14
4
Hapana, sijagoogle na pengine nikukaribishe Mawenzi na Sabasaba Mkoani Morogoro ili nikuoneshe baadhi tu ya miradi pia ukutane na watu wanaofaidika na miradi yangu na uwaulize namna tulivyoanza hadi tulipofikia, watakueleza kila kitu.

Shughuli za kiuchumi huwa nazifananisha na mtoto anapozaliwa, huanza kukaa, kutambaa, kusimama na hatimae kukimbia kabisa.. Kwaio unahitaji kujituma na nidhamu ya hali ya juu unapoamua kujikita katika shughuli za uzalishaji mali ili kukuza uchumi wako na hakuna miujiza bali ni mapambano kaka. Ahsante.
 

Avith almachius

Senior Member
Aug 20, 2022
104
40
Hapana, sijagoogle na pengine nikukaribishe Mawenzi na Sabasaba Mkoani Morogoro ili nikuoneshe baadhi tu ya miradi pia ukutane na watu wanaofaidika na miradi yangu na uwaulize namna tulivyoanza hadi tulipofikia, watakueleza kila kitu.

Shughuli za kiuchumi huwa nazifananisha na mtoto anapozaliwa, huanza kukaa, kutambaa, kusimama na hatimae kukimbia kabisa.. Kwaio unahitaji kujituma na nidhamu ya hali ya juu unapoamua kujikita katika shughuli za uzalishaji mali ili kukuza uchumi wako na hakuna miujiza bali ni mapambano kaka. Ahsante.
Sio kwamba niliposema unagoogle ni kuwa una miujiza wala hata but hakuna jipya kwamba ukagoogle badooo ukawa uelewki what we need is just uniqueness
 

Omari Frank

Member
Jul 22, 2022
14
4
Nashukuru. 🙏
Naomba niipitie hiyo makala lakini naamini itakua nzuri na maono makubwa kwamaana hata kichwa cha habari tu kinasadiki.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom