Uchaguzi 2020 Misingi ya katiba yetu na uchaguzi mkuu: CCM na viongozi wa dini mnaijua/ mnaikumbuka/ mmeisoma?

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,329
6,447
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, toleo la 20 Juni 2005 imeainisha misingi inayohakisi maamuzi mazito ya watanzania wote juu ya nchi yao kwenye utangulizi wake. Misingi hiyo ni uhuru, haki, udugu na amani. Nukuu yake ni: "KWA KUWA SISI Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na amani: NA KWA KUWA misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye demokrasia, ambayo serikali yake husimamiwa na Bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowakilisha wananchi, na pia ..."

Sasa: 1. mbona 'haki' ambayo ni sehemu ya msingi haihubiiriwi wakati huu muhimu wa uchaguzi? Na misingi ilivyopangwa amani ni ya mwisho, yaani ni tokeo la yanayotangulia,

2. Je, ilani ya chama inayogusa haki ipo imara na ya kufaa kwani imelalia kwenye hiyo misingi?

3. kama wajumbe wa Bunge lazima wachaguliwe na wananchi, huyo anayepita bila kupingwa anamwakilisha nani? Pia hawezi kuwa halali na sheria inayomlinda si halali kwani inakinzana na misingi ya katiba.

4. Bunge linawakilisha wananchi, sasa iweje mgombea wa Urais anaomba apewe wagombea ubunge wa chama chake ili awazibe midomo, je sio kuvunja misingi ya katiba yetu?

5. Enguaengua ambayo inafanyika kwa style nyingi ndio mising ya katiba yetu? Je, ni haki?

6. Je, kutumia mali za umma kupigia kampeni ni haki? We mwananchi kama hili si haki, kwa nini bado unamwacha aendelee?

Jamani huu ndio muda muhafaka wa kuilinda na kuitetea katiba yetu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom