johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,598
- 141,415
Ukiondoa CCM na Nccr mageuzi ambavyo vimejengwa katika msingi wa umoja wa kitaifa, vyama vingine vyote vimejengwa katika misingi ya maeneo nk...nk. Na hii ilisababishwa na ukweli kwamba vyama kama Chadema na Cuf baada tu ya kuanzishwa vilikuwa vinajitahidi kuimarika haraka ili vishiriki uchaguzi wa 1995. Matokeo yake wakajikuta wanawekeza nguvu kubwa kwenye maeneo wanayojulikana na hasa ya nyumbani na hata baada ya uchaguzi wakashindwa kujiongeza hivyo vyama vikaonekana ni vya maeneo. Utakumbuka hata UDP kilikuwa cha usukumani, TLP uchagani/wahaya, NRA iliegemea udini pamoja na ukweli kwamba vyama hivi vilikuwa na nguvu katika maeneo fulani lakini vilibomolewa kirahisi sana. Na hata ACT wazalendo wanabomoka haraka kwa sababu hiyo hiyo. Ni wakati sasa viongozi wa vyama hivi vikubwa vya upinzani wakajiadjust kwa haraka ili viwe vya kitaifa kweli vinginevyo vitafutika kwenye ramani. Si kwamba wabunge wananunuliwa NO bali wanakwenda sehemu wanayohisi watakuwa salama. Wabunge kama Cecil Mwambe wa ndanda au Easter Bulaya wa Bunda hawa hawahitaji kununuliwa bali kuambiwa tu " karibuni tena nyumbani " basi kwa moyo mkunjufu wanarejea kwani walitoka CCM baada ya hila tu za watu binafsi na hii ya sasa ni CCM mpya. Cuf na Chadema bado hamjachelewa na taifa bado linahitaji upinzani, lakini ule makini na wenye tija vinginevyo pale mjengoni mtabakia na wabunge kutoka Pemba, Moshi - Arusha, na yule wa Ujiji. Nawasilisha!