Misingi ya CCM imara, yenye Maadili na Nidhamu kama ya Hayati Mwalimu Nyerere ingekuwepo, leo hii Wagombea 'Uspika' wasingefikia hawa '66' waliopo

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
44,032
2,000
Kwa idadi hii tu ya Watu 66 ( hasa wana CCM ) waliojitokeza mpaka sasa kutaka Kugombea Uspika ni Zuzu ( Hambe ) pekee ndiyo hatoweza Kugundua kuwa ndani ya CCM ya sasa ( ya Rais Samia ) kuna Tatizo Kubwa, lakini pia ile Misingi imara ya iliyokuwa CCM ya Mwanzilishi ( na Role Model wangu GENTAMYCINE Kisiasa na Kimaisha ) Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere imeshaachwa na kuifanya CCM ya sasa ionekane kama Guest House / Lodge ambapo kila Mtu ( hasa Wahuni na Malaya ) wanaweza Kuingia muda Wowote wajisikiapo.

Kwa Sisi akina GENTAMYCINE ambao ndiyo Wafuasi na Warithi Tukuka wa Siasa za Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na iliyokuwa CCM yake Imara kuanzia Kimaadili na Kiutekelezaji tunaamini kuwa CCM ile ile ya Mwalimu ingethaminiwa mpaka leo hii idadi ya hawa Wagombea Uspika isingefikia hawa 66 sana sana wangejitokeza Watu ( wana CCM ) makini Watatu ( 3 ) au Watano ( 5 ) tu na ambao hakuna Mtu angekuwa na Mashaka nao.

Kwa Jicho la mbali hii siyo dalili njema ndani ya CCM na Siasa zake na huenda sasa taratibu ile CCM iliyokuwa ya Kipuuzi, ya Madili na Usanii ya mwaka 2005 hadi 2015 ikarejea na kibaya zaidi hata aliyeko anapenda kuonekana ni Mama au Bibi na siyo Kiongozi na Mtendaji ili aogopwe na aheshimiwe na Wanafiki walioanza Kumjaribu na Kumsanifu baada ya Kumsoma na kuijua Pumzi yake Kiuongozi.

Najua mtaninunia, ila nawapenda mno!!
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
8,892
2,000
Hii tabia imezuka miaka ya karibuni baada ya siasa kugeuzwa fursa, watu wanajitokeza kugombania hizo nafasi wengine wakijua wazi hawana sifa ili kujisogeza karibu na jikoni.

Mbele ya safari mwenyekiti wao ajue nao ni wenzao ili awakumbuke kwenye teuzi zake hasa ukizingatia teuzi nyingi hazihitaji CV, ni uamuzi tu wa mwenyekiti na kuwa kada wa kijani.
 

Puncler

JF-Expert Member
Jul 17, 2017
659
1,000
Eti Hadi Baba levo anautaka uspika, chama kimekua mdebwedo sana na mwijaku kachukua fomu nahisi uspika umeshuka thamani sana na job naona ndio kinara wa hayo yote
Jobu ndiyo chonzo cha haya yote, alikuwa spika mpuuzi kuwahi kutokea katika historia yetu tangu enzi na enzi.
Spika aliyeongoza kunyima haki stahiki za wabunge, spika aliyeng'ang'ania wabunge wasio na chama kitendo ambacho ni ubadhilifu mkubwa wa fedha za umma, spika aliyedai mbunge ni mtoro bungeni ilhali akijua kuwa yuko hospitali amelazwa, spika aliyeendeshwa kama gari bovu na rais(Jiwe) mpaka akaonekana kana kwamba ni houseboy wake, spika aliyepiga magoti kutubu baada ya kutoa maoni yake.

Spika mwenye upuuzi mwingi wa kujidhalilisha na kudhalilisha bunge. Bora hata Baba Levo na Mwijaku kuliko huyo Jobu.

Alivyo haribu kwenye issue ya Prof Assad ni kichefuchefu kilichopitiza.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom