Misingi au nguzo kuu nne zinazofanya mahusiano yawe imara na yadumu kwa mda mrefu

MISULI

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
7,826
5,451
Na Sir Taylor.

Habari wadau,
Leo ningependa tuzungumze kidogo kama kichwa cha mada yangu kinavoeleza.

Katika swala zima la mahusiano hasa ya kimapenzi kuna vitu vinne ambavyo vyote kwa pamoja vinafanya mahusiano kuwa na nguvu au imara zaid,hakuna kitu kimoja ambacho kinaweza kuwa mbadala wa mwenzie. Kila kimoja kina nafasi yake na umuhim wake.

Ili mahusiano yaende vizuri na uone umuhim wa ke,lazima hivi vitu uvifanyie kazi kwa usahihi kabisa maana kama nilivosema hakuna hata kimoja kinachoweza kusimama kama mbadala wa mwingine,yaani useme sasa natendea kazi hivi viwili au vitatu na hivi vingine sio muhimu.

Ni sawa na ujenzi wa nyumba,kwa mfano ukitaka nyumba imara lazima msingi uwe imara,na msingi unavitu muhim na ukiacha kimoja tu tayar huwezi kuwa na msingi imara na mwisho nyumba yako haiwez kuwa imara.

Nisiwachoshe na utangulizi mrefu sana,tuanze kuangalia msingi mmoja baada ya mwingine. Karibuni sana.

1. UPENDO.

Huu ni msingi muhimu sana katika kufanya mahusiano yawe imara na ya mda mrefu.Ili kuhakikisha mahusiano yana upendo vitu kama vinne hivi yaani SAFETY and SECURITY ,SUPPORT ,CARE na ACCEPTANCE lazima vizingatiwe.

a)Safety and security.

Yaani usalama na ulinzi. Kwa mtu unaempenda lazima utahakikisha yuko salama mda wowote kwa kila mazingira anayoyapitia. Je unamlinda vipi dhidi ya maadui zake?Unamlinda vipi dhidi ya mapungufu yake?Huwez sema flani unampenda wakati unashindwa kumlinda na wewe ndo mlango mzima wa maadui zake.Kila mtu anapenda kuishi sehem salama. UKIMPENDA LAZIMA UTAMLINDA.

b) SUPPORT.

Katika mahusiano yenu kuna kusaidiana?PENYE UPENDO WA KWELI kuna kusaidiana. LOVE IS GIVE AND TAKE. Huyu anaesema anakupenda, je huwa anatoa msaada wowote pale unapokwama? Lazima msaidiane kwa hali na mali.

Na kusaidiana sio kwenye matatizo tu hata kwenye mambo mazuri. Leo ni siku yako ya kuzaliwa,mwenzio anamchango gani katika furaha yako?Je huwa anakupa msada wowote wa kimawazo au ushauri ktk kutatua shida zako?Au matatizo yako ni yako mwenyewe hakuna cha kusaidiana?ANAYEKUPENDA ATAKUSAIDIA.

c) CARE.

Nacho ni kitu muhim sana ktk hiki kipengele. Mtu anaekupenda lazima atakujali. Lazima aoneshe kujali ktk kila unalopitia,iwe shida au raha. Mtu hawez sema anakupenda hajui hata kuanzia jua linachomoza hadi linazama umeshindaje, unamwambia naumwa au na Ttz flani hata kushtuka hakuna. Yuko busy tu na mambo yake.

Hajali hisia zako,hajali mda unaopoteza kumtafuta au kufanya ye awe ktk mazingira flani mazuri. Ye kila kitu kwake ni kitu cha kawaida. UNAYEMPENDA UTAMJALI TU.

d ) ACCEPTANCE.

Upendo lazima kuwe na kumkubali unadai unampenda.Anaweza kuwa na mapungufu mbali2 may be physical appearance,ukasema huyu ndo MPENZI wangu licha ya hili na hili lkn huyu ndo ananifaa na ndo best choice yangu na yy mwenyewe anatakiwa ajue jinsi gani unamkubali.Je unamkubali ye ni mtu bora?Au unamchukulia kawaida tu.?Na ukimkubali naamn hutaacha kumpa sifa ambazo unazoziona toka kwake.

2.TRUST.

Trusting someone means that you think they are reliable, you have confidence in them and you feel safe with them physically and emotionally.emotionally, it is where you expose your vulnerabilities to people, but believing they will not take advantage of your openness.

Naweza sema ile hali ya mtu kukuamini.Mambo yake ambayo ni more confidential anaweza kukushirikisha na anaamn kwako itakua ni salama na unaweza kuwa msaada kwake. Mpenz wako anaweza kukushirikisha jambo nyeti mno ambalo linahusu family yao,yeye binafsi au chochote kile ambacho anaamn asingeweza kumwambia mtu yyt Yule.

Ktk mahusiano kila mtu akiwa na imani na mwenzie ni rahisi sana kuishi muda mrefu coz mioyo yenu inakua free kueleza chochote kwa mwenzie na ka ni tatizo ni rahisi kutatua,lkn ka hakuna kuaminiana kila mtu anawaza HILI JAMBO AKILIJUA MPENZI WANGU mmmh ANAWEZA AKAHARIBU au KUKWAMISHA .

Yani mazingira flani hivi ya kuonana kila mtu anaweza asiwe salama kwa mwenzie. Na ktk mahusiano kudevelop hiki kitu ni kazi mno lkn kuharibu ni dakika sifuri.Ukishapoteza imani kwa mwenzi wako kuirudisha ni HAIWEZEKANI HATA KIDOGO. ni sawa na kuvunja glasi na kutaka kuirudisha ka mwanzo. NI KITU CHA KUKITUNZA MNO KATIKA MAHUSIANO.

Kama mpenz wako kapunguza imani na wewe utamwona tu,taratibu anaanza kuskip kukupa baadhi ya taarifa au vitu ambavyo mwanzo ilikua kawaida kukupa. Na ikishakuwa hivo tayar mahusiano hayawezi kuwa strong.

3. HESHIMA

Hiki ni kitu muhim sana katika mahusiano. Lazima muheshimiane kila mtu katika kile anachokifanya. Kila mmoja lazima ajue mipaka yake. Mwanaume mipaka yake ni hii na mwanamke ni hii.

Usipojua mipaka yako kama mwanaume au mwanamke ni rahisi sana kufanya kitu ambacho kinaweza kuleta tafsiri mbaya ambayo ni DHARAU. Katika kuonesha unaheshimu nini mwenzio lazima kuwe na acknowledgement, appreciation na positive acceptance kwa jitihada ambazo mmoja wenu anafanya katika kukabiliana na hali flani.

Lazima umweshimu mwenzio sehem yyt Ile. Usifanye vitu vya kumfanya mwenzio aonekane mtu wa ovyo mbele za watu.Lazima kuwe na tofaut kati ya mke au mme wa mtu na watu wengine wa kawaida.MAHUSIANO YENYE HESHIMA HUDUMU MDA MREFU SANA kuliko mahusiano yasiyo na heshima.

4. KUELEWANA.

Katika mahusiano lazima kila mmoja amsome mwenzie. Kama huelew mwenzio yuko vipi ni vigumu sana kuishi pamoja.Lazima ujue akiwa ktk mood flani anabehave vipi.

Lazima uwe na uwezo wa kusoma mazingira haraka sana.Mwenzangu saiz yuko hivi, na yuko hivi kwasababu ya kitu flan so ngoja nifanye hivi. Sio kila kitu unaforce tu. Unaambiwa kuna hili na hili so tufanye hivi, We huelewi. Katika mahusiano maelewano yakikoseka jua mda wowote uhusiano unaweza kuvunjika. Lazima uelewe kuwa kuna kitu MAPUNGUFU, ukielewa mapungufu ya mwenzio na ukaelewa binadam lazima awe na mapungufu basi ni rahisi kuyahandle mapungufu yake.

Lazima uelewe mipango ya mwenzio iko vipi na mkakaa kwa pamoja kuangalia mnafanyaje,sio wewe unawaza hili mwenzio lile na kila mmoja anataka kufanya lake,lkn ka mkaelewana kuna hili na hili na tufanye hivi HAKIKA UHUSIANO UTADUMU MUDA MREFU.

Yako mengi ya kueleza lakini Niseme tu Hizo NGUZO nne ni kama KITI CHENYE MIGUU MINNE .ukivunjika mguu mmoja kinaweza kuwa kiti bado lkn sio kiti ambacho unaweza kukaa kwa kujiachia. TUNZA SANA HIZO NGUZO NNE.

AHSANTENI.
 
Back
Top Bottom