John Mnyika
JF-Expert Member
- Jun 16, 2006
- 713
- 1,241
XXV. ENEZA TAARIFA NA ELIMU YA URAIA: Ukichambua kwa makini utagundua kuwa chanzo kikuu cha matatizo mengi miongoni mwa wananchi ni kukosa taarifa ama elimu ya uraia. Wapo wananchi wanaonyanyashwa kwa kushindwa tu kujua haki zao, wapo wanaokosa fursa za kielimu kwa kushindwa kujua wapitie hatua zipi, wapo wajane wanaonyanganywa mirathi kwa kushindwa tu kujua jinsi ya kusimamia stahili zao, wapo waopoteza maisha kwa magonjwa kutokana na kukosa tu taarifa za msingi nakadhalika. Hivyo yapo maendeleo ambayo Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo anaweza kuyaleta kwa kuwezesha tu taarifa za msingi na elimu ya uraia kuenea kwa wananchi wengine. Hivyo Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo aweke mkazo kwa namna ya pekee sana kuhakikisha taarifa zinaenea na elimu ya uraia inatolewa. Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo awe mstari wa mbele katika kufanikisha msingi huu kupitia mikutano ya jumuia, vipeperushi na njia nyinginezo. Kwa upande mwingine Kiongozi ama mwananchi wa jimbo la Ubungo ahakikishe wadau wengine ikiwemo serikali wanatoa taarifa muhimu na kueneza elimu ya uraia kuhusu fursa na michakato mbalimbali ya kimaendeleo.
Kwa misingi mingine 24, tembelea:http://ubungo.blogspot.com/2008/04/mjadala-wa-maendeleo-ubungo-12-april.html
JJ
Kwa misingi mingine 24, tembelea:http://ubungo.blogspot.com/2008/04/mjadala-wa-maendeleo-ubungo-12-april.html
JJ