Misimamo ya Rais Magufuli itakuwa ile ile mkimchagua jiandaeni kuendelea kusota

kagoshima

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
2,631
5,137
Ukimsikiliza kwenye kampeni zake Magufuli haonyeshi dalili ya kubadilika.

Anaongea Yale Yale na haonyeshi angalau kutoa matumaini ya namna gani ataongeza ajira, je haki za wafanyakazi zitaboreshwa? Haki za kiraia zitalindwa? Wakulima watawezeshwa vipi kimitaji na kimasoko?

Je, atapunguza makato bodi ya mikopo?

Je, kundi la watoto wanaotaabika na kuacha vyuo kwa kukosa mikopo atatatua vipi hilo tatizo ? Na mengine mengi.

Anatajataja tu madaraja, ndege, Barabara.

Kwa uelewa wangu ni kwenye ukishapewa kuunda serikali ujenzi wa miundo mbinu nilazima uufanye wakati huohuo uchumi na afya za watu lazima uziboreshe, ajira ziongezeke, mishahara ipande proportionary

Hakuna excuse ukishindwa kufanya hayo yote kwa pamoja pisha office umeshindwa kazi.

Sasa mgombea wa CCM ni dhahiri akichaguliwa tena mambo mengine yatendelea kuwekwa benchi. Vijana wataendelea kukosa ajira.

Wafanyakazi wataendelea kusoteshwa. Wafanyakazi waendelee kusubiri maumivu. Wananchi waendelee kusubiri lugha za kejeli
 
Nimegundua pia, mambo ya ajabu yote aliyowahi kuyafanya hamna mtu aliwahi kumuambia kua umekosea na kumkosoa ndani ya chama chake, anapewa tu praise.

Ndani ya miaka 5 amepata criticism kutoka kwa TL tu pekee, ndio maana kila ikifika jioni lazima asikilize 'Reo kaongea nini Risu"
 
Yanaanza na wewe kwa kumpa Magufuli, mbunge na madiwani. Tanzania mpya, inakuja.
Kama baada ya miaka 5 bado hatujamuelewa Meko anahakikisha kwenye Kampeni za mwaka huu anaweka wazi HULKA yake.

Tusijekulalamika akichukuwa Urais 2020-2025.

*Ukimpigia Kura mpinzani utalipa kodi kama kawaida lakini usitengeme huduma za Serikali*

28/10/2020 Kazi kwetu!
 
Ukimsikiliza kwenye kampeni zake Magufuli haonyeshi dalili ya kubadilika.

Anaongea Yale Yale na haonyeshi angalau kutoa matumaini ya namna gani ataongeza ajira , je haki za wafanyakazi zitaboreshwa? Haki za kiraia zitalindwa ? Wakulima watawezeshwa vipi kimitaji na kimasoko ?
Je atapunguza makato bodi ya mikopo?
Je kundi LA watoto wanaotaabika na kuacha vyuo kwa kukosa mikopo atatatua vipi hilo tatizo ? Na mengine mengi.

Anatajataja tu madaraja, ndege , Barabara.
Kwa uelewa wangu ni kwenye ukishapewa kuunda serikali ujenzi wa miundo mbinu nilazima uufanye wakati huohuo uchumi na afya za watu lazima uziboreshe, ajira ziongezeke, mishahara ipande proportionary .
Hakuna excuse ukishindwa kufanya hayo yote kwa pamoja pisha office umeshindwa kazi.

Sasa mgombea wa CCM ni dhahiri akichaguliwa tena mambo mengine yatendelea kuwekwa benchi. Vijana wataendelea kukosa ajira. Wafanyakazi wataendelea kusoteshwa. Wafanyakazi waendelee kusubiri maumivu. Wananchi waendelee kusubiri rugha za kejeli
Tatizo Ni watanzania tupo very hopeless na safari hi atatutia mpaka madole ya pua
 
Madaraja oyeee!! Nilimsikia jiwe akisema...kwa hiyo hana jipya na IQ yake inatia mashaka
 
Sasa kama tunachagua wabunge na madiwani ambao hawawasilishi matatizo ya wananchi kunakotakiwa, badala yake tunasubiri rais apite mtaani kwetu ndio tuanze kumweleza si lazima tusote?
Wenzetu wanawakilisha watu wao, sisi tunatukana na tunatoka nje ya bunge.... kama mpinzani baada ya kukosa dola hamna haja ya kususa, ni bora kuwadai chama tawala watekeleze kile walichoahidi
 
Ilani ya msimu huu ni kubwa mara 3 ya ile ya msimu uliopita na yote imesheheni madaraja, madege, sijui mastiglaz joji, kazi kwenu!
 
Back
Top Bottom