Misimamo rahisi iliyonisaidia mpaka leo napumua

mtoto mdogo sana

JF-Expert Member
Apr 16, 2020
460
1,337
Habari zenu ndugu zangu.

Leo ikiwa ni mwishoni kabisa mwa wiki basi niwape pole kwa mihangaiko ya kila siku. Aidha kazi na majukumu sio mateso, ni kipimo na thamani ya mchango wa kila mmoja kuleta tofauti fulani yenye matumaini kwenye maisha.

Pasipo kupoteza muda zaidi naomba nianze na mada yangu moja kwa moja.

Kwa haraka haraka naweza kuyatafsiri maisha yangu kwa ujumla kama mfululizo Assignments. Mara nyingi nimekuwa nikiishi maisha yenye changamoto zisizonipa nafasi ya kuchagua mbadala wa maamuzi. Yaani nimekuwa kama ng'ombe kwnye josho. Huenda tu mbele na hata akiamua ageuze nyuma kuepuka kupita kwenye maji yenye dawa basi hataweza kwa sababu ya ufinyu wa njia.

Ila ninachoshukuru zaidi ni kuwa Mungu hakuwahi kuniacha peke yangu katika yote haya. Yaani naweza kusema mimi ni kati ya watu wenye bahati sana. Kuna namna huwa nafika kipengele ambacho siwezi kujinasua ila ghafla, na wakati mwingine bila juhudi zangu binafsi nashangaa mtu anajitokeza kuazimia kunivusha. Asante Mungu kwa hili.

Kwa kuwa nimeishi maisha ya kienyeji sana tangu utotoni, basi **** misimamo niliyojiwekea, ambayo kila siku imekuwa kama katiba kwangu niifuate ili niendelee kuishi. Tena niishi kwa amani.

1. Kwangu, ahadi sio deni. Yaani ukiniahidi jambo lolote mimi nachukulia kama sehemu ya stori zetu mpaka utakapofanikiwa kutimiza ahadi yako. Awali niliwahi kuwa nadai ahadi... Badala ya kutimiziwa nilionekana ni msumbufu na hapo nikajiambia kuwa Ahadi sio deni. Naamini kuwa kuna wakati mtu anaweza kuniahidi jambo kutokana na mood aliyonayo. Ila hali inapobadilika, haipi tena nguvu wala nia ile ahadi aliyonipatia. Msimamo huu umekuwa ni chachu ya mafanikio yangu. Na kimsingi mimi sidai ahadi asirani.

2. Sikasiriki kisa nimetukanwa wala kudhalilishwa, tena najitahidi nisirudishe nono lolote. Kwanza ni kutokana na kuwa, kwa maisha yangu ya mtaani, matusi magumu na mazito sana ndio ilikuwa lugha nilizokutana nazo siku zote. Nadhani unaelewa asili yetu binadamu, tunapokutana na jambo zito au gumu, faraja ya kwanza ni kutukana sana. Bila kujalisha unamtukana mtu au unatukana mwenyewe.

Zamani nilipokuwa sijaanza kuishi msimamo huu, nilikuwa mgomvi sana. Tena nilikuwa nikipigana na mtu namuumiza vibaya sana.. (nina asili ya hasira sana. Hasa kabla sijaweza kuzimudu) zamani kama mtu akinikasirisha sawasawa, nilikuw nampiga mtu mpaka pale hawez tena kurudishia wala kuongea. Mara ya kwanza nikiwa na miaka 12 nililala lock up siku 3 (nilifungiwa ofisi ya mtendaji wa kijiji kwa kuogopa kunifunga lockup ya wakubwa) na sababu ya kuachiliwa sio kwamba sikuwa na hatia. No. Isipokuwa sikuwa na mtu wa kunihudumia kwa msosi nikiwa pale kizuizini. Wakaona wanikanye waniache. Anyway niliwahi kuwa na mfululizo wa magukio ya kuwavunja watoto wenzangu mikono, vidole na miguu nikipigana nao mpaka nikaonekana pepo fulani.. ila baadae, ilifika kipindi nikaweza kabisa kuzimudu hasira zangu kwa njia hii.

3. Mimi situmii maneno mengi sana kujitetea na inapofika wakati nakazaniwa, nakaa kimya kuepusha ubishi. Hii usiitafsiri kama kiburi, hapana... Mimi nakuwa mwepesi wa kuomba samahani na kukubali kuwajibjka hata kama nina uhakika kosa sijalifanya. Mara nyingine watu tuna perspective tofauti. Unavyozidi kujitetea, ndio unavyozidi kumkesa uliyemkosea. Hii imenisaidia kuokoa baadhi ya urafiki ambao ungevunjika. Pia imenifanya kuaminika kwa haraka ninapokutana na yeyote. Kwa asiki ya kabila langu inasemekana sisi ni wabishi na hatukubali kutajiwa au kutajwa isivyo. Ila nadhani mimi nimekuwa mmoja kati ya waliofanikiwa kwenda tofauti na asili ya kabila.

4. Situmii shida yangu kama excuse kuiba au kuvunja sheria au taratibu zozote za kijamii. Kwenye maisha yangu yote mimi shida yangu kubwa sana ambayo imekuwa ikinisumbua ni njaa. Njaa ndio adui yangu namba moja. Na hii imepelekea mimi kuwa msomi asiyekuwa na future. Nimekuwa kila siku natafuta namna ya kushibisha tumbo tu. Nikishiba naridhika nangoja jua lizame nilale.

Sijui kama naeleweka, ila namaanisha, huwa najizuia kuiba, kutapeli na kudanganya ili nipate mahitaj yangu. Aidha jambo jingine nisiloweza kufanya najitahidi kutotumia shida zangu kama mtaji. Mimi ninao uwezo mkubwa sana wa kuzisoma saikolojia za watu mbali mbali. Huwa nina uwezo wa kubashiri matokeo ya kauli zangu kwa watu na nina uwezo mkubwa sana wa ku-manipulate mtu apate wazo fulani bila mimi kulitaja kwa uwazi. Lakini nilijipa msimamo kuwa njia ya mwongo na mwovu siku zote ni fupi. Siombi msaada kwa chambo cha shida zangu. Labda mtu ajisikie kusaidia mwenyewe.

5. Subira. Nikiwa na shida hata iwe ya haraka vipi, ila mtu mwenye mamlaka husika aka suggest jambo la mimi kubuta muda, huwa napitisha wazo hilo haraka sana. Yaani sipingi. Najua nyakati nyingine huwa inanicost ila trust me. Hiyo imenijengea uaminifu na hali ya kuonekana mnyenyekevu kwa watu wengi.

Nitaendelea baadae nikitulia.
View attachment 1647395
View attachment 1647396
 
................................Hoja #1 nimeipenda sana,ila nimefikiriaa sijakumbuka kama kuna mtu aliniahidi au labda tayari nipo kama wewe sifuatilii sana mambo ya ahadi sijui.

Hiyo #4 hasa paragraph ya kwanza ukiisoma kwa utulivu inaumiza sana japo kimaisha sipo ktk stage hiyo,siyo wewe tu hayo maisha ni wengi wanayaishi baada ya kupoteza muda wao mwingi ndani ya kuta nne wakitegemea neema wakimaliza ila hola.

Mungu awape nyote hitaji la mioyo yenu.
 
................................Hoja #1 nimeipenda sana,ila nimefikiriaa sijakumbuka kama kuna mtu aliniahidi au labda tayari nipo kama wewe sifuatilii sana mambo ya ahadi sijui.

Hiyo #4 hasa paragraph ya kwanza ukiisoma kwa utulivu inaumiza sana japo kimaisha sipo ktk stage hiyo,siyo wewe tu hayo maisha ni wengi wanayaishi baada ya kupoteza muda wao mwingi ndani ya kuta nne wakitegemea neema wakimaliza ila hola.

Mungu awape nyote hitaji la mioyo yenu.
Asante sana mkuu. Ubarikiwe

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Mi nitajuaje sasa, it is your life, go on with your life

Tutajuaje mwenzetu kama hutaki mafarakano ndio ukaamua kujiwekea misimamo?

Nasubiri muendelezo
 
Back
Top Bottom