Misimamo mikali ya wenzetu kwa Viongozi wao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Misimamo mikali ya wenzetu kwa Viongozi wao

Discussion in 'International Forum' started by Sijali, Oct 22, 2012.

 1. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,054
  Likes Received: 405
  Trophy Points: 180
  Nimesoma katika forum moja: ..!! - kuwa Wamisri wamenza kumkaba koo rais wao, Mohammed Morsi, kwa kupenda kwake safari za nje.
  La kushangaza ni kuwa bw. Morsi ambaye ameingia madarakani miezi minne iliyopita, amefanya safari si zaidi ya 6 tu na zote kwa kweli zilikuwa na umuhimu mkubwa. Safari yake ya kwanza ilikuwa Saudi Arabia kwa ajili ya kutafuta fedha za bajeti ya Misri ambayo imeporomoka sana kutokana na machafuko ya 'Arab Spring' kwani utalii umekwenda chini mno. Pia huko alizungumzia kadhia maarufu la daktari mmoja wa Misri aliyefungwa huko. Halkadhalika suala la Syria. Halafu akazizuru China na Iran kwenye mkutano wa non-aligned countries, na hatimaye akaenda New York kwa mkutano wa UNGA. Hapo katikati alikwenda Uturuki juu ya masuala ya ushirikiano wa kijeshi na nchi hiyo. Uturuki pia imejitolea dola bilioni 2 kwa kuisaidia Misri.
  Katika kujitetea, bw Morsi amesema, kwa kweli ziara zake ni za lazima na kwamba ameweka sheria wakati wa safari kuwa yeye na wote wanaofuatana naye wasizidi watu 8 na kwamba kila siku per diem (matumizi ya nje ya Ofisi) ya kila mtu iwe ni dola 63 tu!
  Sasa, Misri ni nchi yenye uchumi mkubwa mara 11 ukilinganisha na Tanzania (Misri pato la taifa dola 252 bilioni kwa mwaka, Tanzania dola 23 bilioni. Pato la mtu Misri, dola 6,500 kwa mwaka, Tanzania dola 1,500). Rais wa nchi anajipa dola 63 tu kwa siku! Fikiria huyu wetu na ujumbe wake wa watu 20 wanachoma ngapi kwa saa wakiwa nje? Halafu mnapiga kelele za umaskini!
   
 2. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mtamlaumu bure huyu wa kwetu, yeye anamatatizo yake binafsi ya CD.... Ndo mana inambidi aende clinic (za nje), mara kwa mara, au mnataka awafie...
   
 3. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,054
  Likes Received: 405
  Trophy Points: 180

  Hata kama naheshimu sana maoni yako, isipokuwa naomba tujiepushe na madai yasiyo na ushahid kwani haya yanaweza kututia kwenye manza.
  Unajua JK anaweza kukushtaki (sue) aidha wewe au hata mwenye Forum hii, kwa sababu ulichosema ni Libel. Naomba moderator aondoe hiyo hapa haraka!
   
 4. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mkuu hakuna mtu aliye-mention JK, hapo juu, au kupitia quotation yako unataka watu wajue ni JK...
   
 5. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Umenikumbusha forum fulani walialikwa wajumbe 60 na barua ikasema hakuna posho wala nauli. Wajumbe waliohudhuria ni kama 8 tu. Huyu rais ameambukiza watendaji wake wote, bila posho hakuna kazi. Ingeazishwa style ya ki-UN ya ukienda safari unalipiwa full board na kupewa incidental ya 10$ for communication per day. Watu wangekimbia safari hapa.
   
 6. Sijali

  Sijali JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 2,054
  Likes Received: 405
  Trophy Points: 180
  Nadhani wenzetu wa sheria wana kitu kinaitwa 'circumstantial evidence' kwamba mpangilio wa maudhui yenyewe unaonesha waazi mlengwa ni nani. Nadhani wataanzia hapo.....
   
 7. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #7
  Oct 23, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,451
  Likes Received: 4,734
  Trophy Points: 280
  ndio maana kumbe msafara wake unafuatana na Ambukance? kwa Kamabarage, Mwinyi, Mkapa sijawahi kuliona hili............aaaahhhh hata kuanguka anguaka eh??
   
Loading...