#COVID19 Misikiti mitano yafungwa Saudia baada ya waumini 7 kukutwa na Corona

tilmikha

JF-Expert Member
Feb 27, 2013
496
604
Wizara ya mambo ya kiislamu nchini Saudi Arabia,leo imeifunga misikiti mitano kwa muda kutoka mikoa mitatu tofauti baada ya kesi saba za virusi vya Corona kupatikana katika baadhi ya waumini, idadi ambayo inafikisha jumla ya misikiti iliyofungwa ndani ya siku 11 kufikia 92 ambapo 79 imeshafunguliwa baada ya kupulizwa madawa na kukamilika kwa hatua za kuhakikisha utayari wa za kiafya zipo katika hali inayotakiwa.

Chanzo: Wizara ya mambo ya kiislamu S. Arabia.
 
Hivi hawa hawaamini kwenye Mungu, sala na maombi kama jiwe? Mbona wanafunga hata nyumba za ibada?
Wizara ya mambo ya kiislamu nchini Saudi Arabia,leo imeifunga misikiti mitano kwa muda kutoka mikoa mitatu tofauti baada ya kesi saba za virusi vya Corona kupatikana katika baadhi ya waumini, idadi ambayo inafikisha jumla ya misikiti iliyofungwa ndani ya siku 11 kufikia 92 ambapo 79 imeshafunguliwa baada ya kupulizwa madawa na kukamilika kwa hatua za kuhakikisha utayari wa za kiafya zipo katika hali inayotakiwa.

Chanzo: Wizara ya mambo ya kiislamu S.Arabia.
 
Hizo dawa zinazopuliziwa na watu wanarudi miskitini zinaonekana zinauwa virusi vya corona, kwa nini zisifanyiwe modifikesheni zikawa zinatumika kwenye kunywa? 😷 🥴
 
wanasubiri Nini kumuomba Mungu was awaepushe na Hilo janga !?

Mkiambiwa dini Ni janja janja mnakataa
Dini ni zaidi ya kumuomba Mungu pale unapokuwa na shida,dini ni maisha hivyo si sehemu ya miujiza miujiza kama ambavyo labda unafikiri. Na hapo si kwamba hawamuombi Mungu,tatizo hata ukiambiwa shida fulani iliondoka kwa kumuomba Mungu utakataa utasema ni imani tu ila hapo hapo ukiona wana shida unasema mbona hawamuombi Mungu.
 
Dini ya kiislamu imefunza waumini wake kuchukua tahadhari. Panapo ibada na afya basi afya ya mtu hutangulizwa mwanzo.
Bado hai make sense wajua kwanini !?
Huwa mnasema katika Qur'an Kuna mafundisho yote mpaka sayansi Sasa Kama hivyo ndivyo inakuwaje waislam mshindwe kuja na tiba kwanini msitumie hiyo Qur'an ambayo ndani yake' Ina mafunzo ya kisayansi kuiponya dunia kutofanya hivyo hauoni kwamba inadhihirisha wazi kuwa huwa mnatudanganya
 
Back
Top Bottom