Misiba ya kadi, make-up, nguo na magari ya kifahari

Siri Sirini

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
547
198
Kuna gazeti nimesoma yani nimeishia kucheka tu, lakini ni vinatokea kwenye jamii yetu, ni kuhusu watu waendavyo misibani, mana watu wanaenda kuonyeshana nguo, magari ya kifahari, mitindo ya nywele na jinsi ya kupaka vipodozi.
Palipo nichekesha
wengine mavazi wanayokuja nayo msibani hayana heshima, akidondosha kitu mtihani kuokota, achilia mbali viatu alivyovaa kama ngongoti anayesubiliwa kupigiwa makofi na watoto wanaomtizama, mradi atizamwe msiba mzima. Vipodozi vinavyopakwa usoni hata wengine kulia hawawezi, nyuso zimewakakamaa, mikope mirefu kama mijinamizi, huo wanja kama amefukuzwa kwenye fumanizi, mwingine hata mtandio wa kujitanda hana, mradi aonyeshe style yake ya nywele, ukija kwa wakaka, kutwa kaning'iniza funguo ya gari mkononi, suti kali hata kama kuna jua kali gani, cm ipo sikioni mda wote, mradi muione.
Jamani wapi tunaelekea? Tunawaiga wenzentu? Maana wao hata kulia cdhani kama wanalia, na kuvaa vimini kawaida yao,

dah! Nimechoka, ni hayo tu wana cc
 
Kama kuna mtu alienda kwenye msiba wa Steve Nyerere alikuwa shahidi.
Ilibaki kidogo nimtie Kofi yule msanii anaeuza nyago Uhuru Park Bar.
 
Yani umesema kweli kabisa. Yani watu ubinadamu na huzuni hawana kabisa yani.
 
Point of order:
Kuning'iniza funguo za gari sio ufahari,ni necessity,hakuna kitu kinatoboa mifuko ya suruali kama funguo.
Mengine uliyotaja nywele,kope,viatu etc i reserve my comment sitaki nigombane na ma darling wangu,na ukame huu nitakimbilia wapi.
 
shikamoo mzee Bishanga hadi na za pikipiki huwa unaning'iniza pia (funguo)
 
Last edited by a moderator:
Point of order:
Kuning'iniza funguo za gari sio ufahari,ni necessity,hakuna kitu kinatoboa mifuko ya suruali kama funguo.
Mengine uliyotaja nywele,kope,viatu etc i reserve my comment sitaki nigombane na ma darling wangu,na ukame huu nitakimbilia wapi.

wengine wanafanya sifa, mradi tumuone ana gari, kaning'iniza mifunguo kibao
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom