Ama kweli mambo yamebadilika.Siku hizi misiba imefanana na sherehe.Ni kula kunywa na kuvaa,badala ya kuombooleza,chunguza shughuli nzima,hata kulia watu hawalii kama zamani.
Sasa hivi ndiyo nimeelewa hekima za wazee wa zamani, kijijini kwetu ilikuwa kipindi cha msiba chakula ni kande zenye mchanganyiko wa mahindi makavu yasiyo kobolewa na maharage yanachemshwa tu! Na kutiwa chumvi, ilikuwa hakuna mambo ya siku hizi vyakula lukuki na Mbwembwe nyingine huzuni ilikuwa inaonekana kabisa, lakini misiba ya siku hizi. Mimi binafsi nimewahi jichanganya nilizama kwenye harusi na kutoa pole kumbe msiba ulikuwa nyumba ya pili kote kulifungwa speakers kubwa na Mbwembwe !
Wakilia au wakicheka siku zangu zitakua zimeshaisha hapa duniani na nimeshashafutika ivyo waliobaki kazi kwao walie au wacheke hawana na sina msaada nao.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.