Misiba imekuwa gharama sana

Ulimbukeni,..bushi kwetu huko bado wanakula kande,wamama hubeba huja wamebeba chakula,kindi,komon na kimpumu kwaajili ya waume zao walio msiban na pia na sisi wagen tulio toka mjini.......hakuna.mambo ya muziki MBOZI sijui wali


Anasa iliyopo n pombe za asili over
 
kinachoniumiza ni pale mgonjwa alikosa hela ya matibabu ikapelekea kifo aisee acha tu
Halafu akifa ndio ndugu wanajitokeza kukodi mziki, mpiga picha, magari, waliaji na kununua jeneza la bei kubwa achilia mbali vyakula na vinywaji. Gharama utakuta inaenda kwenye mil 3 wakati hela ya kumtibu iihitajika laki 4 tu lakini hakuna aliywkuwa tayari kutoa.
 
Halafu akifa ndio ndugu wanajitokeza kukodi mziki, mpiga picha, magari, waliaji na kununua jeneza la bei kubwa achilia mbali vyakula na vinywaji. Gharama utakuta inaenda kwenye mil 3 wakati hela ya kumtibu iihitajika laki 4 tu lakini hakuna aliywkuwa tayari kutoa.
inaumiza sana
 
Kwetu waislam hatuna mambo hayo, Usilam wa kweli mtu akishafariki tu asicheleweshwe azikwe, na atahitaji sanda , kuoshwa , kuswaliwa na kuzikwa bila mbwebwe.

Mbona wanaadam tumeghafilika? wapi ndugu zetu mnakwenda? hebu kaeni chini mjiulize mnakwenda wapi? mapambo, nguo za sare, vyakula vya kila aina vitamsaidia nini maiti?

Inasikitisha mtu anaumwa mgonjwa taabani anahitaji msaada wa dawa ama vipimo vya bei ghali, wakiendewa jamaa na ndugu watazunguka huku na kule hawatoi hata cent au watoe elfu kumi, leo mtu huyu huyu akifariki huyu katoa laki tano, mwengine laki sita tena kwa mashindano, wakati marehemu huyu anahitaji pesa ya matibabau hizi laki tano zilikuwa wapi? naandika kwa uchungu sana ! binadamu tuzinduke na tuache mambo yasio na maana.

Maiti huwa anahitaji vile vitakavomsaidia kumstiri hizo mbwembwe hazitamsaidia aslan abadan...

Kuna aya kwenye Quraan inasema "FA AINA TADHHABUUN" mnakwenda wapi? ...
 
Dunia inabadilika, maisha yanabadilika misiba sasa sio huzuni bali sherehe.
Kilichopo kitapikwa, kitafanyika na kutendeka.

Huzuni ni pale tu Marehemu alikufa kwa kukosa dawa au ghafla.
 
Tunaiga umagharibi sana.
Wenzetu mtu akifa wanazika yeye na jirani zake.
Kwa nature ya familia zao hat 50 hawafiki.
Hivyo kuwa na sare ; chakula safi na showcase watakazo kwa nature ya uchumi wao it is possible.


Ukichaa ni huku kwetu msiba unaufhuriwa na kijiji kizima.
Watu zaidi ya 500 . eti una force wote wapate chakula cha bufee
Wote wapate vinywaji
Kuwe na mziki
Ndg na jamaa wa karibu sale ya tshirt or madela.

Usawa wenyewe huu wa mwendokasi.

Tukio la masaaa 8 linaiacha familia na madeni ya vicoba na saccos.


Lazima tujifunze kutumia akiri.

Kifo sio ufahari ni kipindi cha maambolezo na kuitafakari hatima ya maisha yetu.
 
Kwa mwendo huu si ajabu mbele ya safari watu wataanza kuandaa hata kadi wanakuangalia tu! "Huyu hii wiki hapindui kachape kadi kabisa " wameongeza msiba juu ya msiba.
 
Mi naona kama wakristo ndio huwa wana mambo mengi,misiba ya waislamu haina mbwembwe na gharama, mtu akifa anazikwa haraka maisha yanaendelea.
 
Inabidi hata watu wa kulia nao uwakodi,maana siku hizi wana ndugu huwa hawalii huwa wanafikiria tu namna ya kugawana mali za marehemu.
Misiba ya siku hizi ni soo unakuta mtoto kafiwa na mzazi wake tena kijana tu eti ndio msoma risala sijui hizo nguvu wanazipataga wapi kizazi cha laana hichi
 
Misiba siku hizi Ina Kamati za Mapambo,muziki,vinywaji na vyakula,sare za wafiwa,MC,Video na Picha,Maturubai na Viti,Jeneza na gari la kubeba mwili ...n.k.
Gharama ya shughuli nzima inaweza kufikia mamilioni ya shilingi.

Ilhali misiba ya zamani ilikuwa ni mikeka,waimba kwaya,majirani kujitolea kupika,maturubai yalikuwa yanatolewa bure,jeneza hutengenezwa kwa gharama nafuu...n.k.
Kupanga ni Kuchagua.
ni kweli ila ni kwa wenye nazo km huna kitu huwezi fanya hivyo, pande hii ukifa leo unazikwa leo na ni vikombe vya chai tu vinatembea
 
Misiba siku hizi Ina Kamati za Mapambo,muziki,vinywaji na vyakula,sare za wafiwa,MC,Video na Picha,Maturubai na Viti,Jeneza na gari la kubeba mwili ...n.k.
Gharama ya shughuli nzima inaweza kufikia mamilioni ya shilingi.

Ilhali misiba ya zamani ilikuwa ni mikeka,waimba kwaya,majirani kujitolea kupika,maturubai yalikuwa yanatolewa bure,jeneza hutengenezwa kwa gharama nafuu...n.k.
Kupanga ni Kuchagua.

Mwisho wake ndio umefika sidhani kama itaendelea kwa darasa tulilomo la kusoma namba
 
MKUU HUO NI UBIDHAISHAJI, AMBAPO KILA KITU NI BIDHAA! SIYO MSIBA TUU. SIKU HIZI WATU NI MATAJIRI KWA TENDA ZA KUTOLEA KINYESI NA MKOJO MIJINI!!
 
Back
Top Bottom