Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,459
- 29,153
VyetifekiMkuu umenikumbusha kadhia iliyonikuta enzi hizo namaliza darasa la saba tunajaza zile form nikaandika majina yote matatu yani First Name(Langu), Middle Name(Baba), na Surname (Ukoo) basi mwalimu mmoja wa kike akanizuia hilo jina la kati. Nimeenda elimu za mbele hadi ya juu kote nadaiwa majina matatu, cheti cha kuzaliwa, kupiga kura, kitambulisho cha taifa, na hati ya kusafiria kote wanataka majina matatu. Mimi nimeamua kuongeza hilo la kati kama inavyoonesha ktk hizo nyaraka muhimu kama cheti cha kuzaliwa. Namchukia sana yyule mwalimu, nashangaa kwanini alikuwa mjinga wakati alifika kidato cha nne na alikuwa mke wa afisa uhamiaji nilitegemea angejua umuhimu wa middle name.