Mishahara ya watumishi wa umma kulipwa hazina kupitia BoT

I see!!In 1970's wakati huo ATC imedhaminiwa na Serikali ya Uholanzi,kupitia Royal Dutch Airlines (KLM) kwenda kusomesha vijana maswala ya Aicraft Engineering and Avionics.Vijana tulipata tabu sana katika kuandaa safari.

Ilikuwa ni lazima kwanza documents za passport ya mtu ianze kuhakikiwa na balozi wa nyumba kumi na viongozi wengine kuanzia ngazi ya kijiji mpaka Mkoa.Pale BOT wakati wa kuondoka ndio palikuwa mahali pekee ambapo tulipewa pesa za kigeni(dola).Yaani ulikuwa huwezi kupata mahali popote dola zaidi ya bank kuu,kwa hiyo hata wakati wa kurudi likizo ilikuwa ni lazima pesa za kigeni ulizokuja nazo ukabadili pale BOT ndio uingie mtaani kula bata na warembo na kwenda kijijini kapaua nyumba toka kwenye tembe kuwa za bati.

Serikali ilikuwa inajua nani leo kabadilisha shilingi kwenda kwenye dola,na nani kabadili dola kwenda kwenye shilingi.Kiwango cha dola kilichopo ndani ya nchi kilifahamika maana ulikuwa huwezi kupata "Bureau de change" mtaani,isipokuwa za "magendo" kwa wahindi fulani Kkoo na mitaa ya Upanga,ambao wao walienda nazo Kenya kimagendo.

Mwaka mmoja kuna mzee karani wa BOT,ndugu wa mwanasiasa fulani,alinidhulumu karibu shilingi laki mbili za Kitanzania,ambazo kwa wakati huo...Nilikuwa nina uwezo wa kununua shamba hekali 100,kujenga nyumba mbili Dsm na mbili kijini na kuwa na "guruwe" langu toka kwa mjerumani.Anasema mimi mwanafunzi,nasomeshwa na serikali,nalipiwa kila kitu siwezi kumiliki pesa zote,ni dalili za uhujumu uchumi na ukabaila.

Miaka miwili baadae,maafisa wa bandari walizuia "guruwe" langu moja kati ya mawili niliyoagiza toka kwa rafiki yangu Germany,wakasema kumiliki gari mbili ni uwizi na unyonyaji wa kujilimbikizia mali.

Huu mtindo naona sasa unarudi kulekule....Mishahara BOT,na mwisho kubadili pesa itakuwa BOT...Maana halmashauri na mashirika yote ya serikali yaliyokuwa na account benk binafsi sasa wanapeleka pesa kwenye account ya serikali beki kuu.Nafikiri hii ndio ile wanaita "Centralized System of Economy".Serikali ndio anakuwa muamuzi wa shughuli zote za kifedha katika nchi.Sasa haya mabenki binafsi ambayo mishahara ilikuwa inapita kwao watafanya biashara gani?NMB kwa walimu na CRBD kwa watumishi wa umma na mashirika ya serikali......

Nyerere aliliona hili,ndio maana akaleta ile mliita "Madaraka Mikoani".....Wanaita "D by D" yaani "Decentralization by Delegation".Ugatuaji wa madaraka!!Ukirundika kila kitu BOT,mtu akipata tatizo la mshahara akiwa Nanjilinji,tawi la BOT huko kusini ni mpaka Mbeya...Tutafika kweli??
Mkuu umeturudisha nyuma sana enzi hizo bia sh 200 soda sh 10 baikeli sh 500 na gari sh... Nimekumbuka mbali sana! RTD idhaa ya taifa na idhaa ya biashara kule yuko anko J Nyaisanga...
 
Kwa hiyo Bashite ataandikaje? Maana mwenyejina kapatikana na anahojiwa na Takukuru Tabora
Bashitw sio mtumish wa umma.
Jamani ushasahau ile hotuba ya UDOM kwenye kukabidhiana orodha ya majina 9000+??
 
Mkuu umeturudisha nyuma sana enzi hizo bia sh 200 soda sh 10 baikeli sh 500 na gari sh... Nimekumbuka mbali sana! RTD idhaa ya taifa na idhaa ya biashara kule yuko anko J Nyaisanga...
Duh!baisikeli ilikuwa sawa na biambili nanusu ,.
 
Ni uelewa tu mkuu!! Mpaka sasa hivi pesa za mishahara zinalipwa kupitia BOT yaani Hazina wana akaunti BOT ila pesa zinakuwa transferred kwenda commercial banks kutoka BOT ambako mtumishi ana akaunti yake. Nafikiri wanachotaka ni verification ya majina kati ya payroll na akaunti zilizoko kwenye commercial banks. Hivyo mtumishi ataendelea kulipwa pesa zake kwenye commercial banks
Asante sana mkuu kwa kunielewesha!!Nitasubiri ufafanuzi mwingine toka mahali kwingine,huu wako umenifungua macho
 
Mfano ktk payroll nimetumia majina mawili na kule bank nimetumia na jina la ukoo hapa itakuwaje?

Nenda kayaunganishe yafanane acha ubishi ni lazima yawe matatu mfano John Albert Mapunda na sio John Albert wala john Mapunda.maana john Albert ni mtu mwingine, John Mapunda ni mwingine na John Albert Mapunda ni mtu mwingine ok wahi sasa
 
Taarifa sio rasmi. We need verified information. Hata sihangaiki coz cjapata taarifa yoyote toka kwa mwajiri wangu

Mwajiri wangu leo mapema sana asubuhi kanisogezea form ili nijaze taarifa zangu kuhusu hii ishu na inataka uwe na uhakika wa usahihi wa majina ya kwenye payroll na bank nadhania itawafikia tu kwa kua zoezi litaanza kufanyika mwisho wa julai kama sikosei.
 
I see!!In 1970's wakati huo ATC imedhaminiwa na Serikali ya Uholanzi,kupitia Royal Dutch Airlines (KLM) kwenda kusomesha vijana maswala ya Aicraft Engineering and Avionics.Vijana tulipata tabu sana katika kuandaa safari.

Ilikuwa ni lazima kwanza documents za passport ya mtu ianze kuhakikiwa na balozi wa nyumba kumi na viongozi wengine kuanzia ngazi ya kijiji mpaka Mkoa.Pale BOT wakati wa kuondoka ndio palikuwa mahali pekee ambapo tulipewa pesa za kigeni(dola).Yaani ulikuwa huwezi kupata mahali popote dola zaidi ya bank kuu,kwa hiyo hata wakati wa kurudi likizo ilikuwa ni lazima pesa za kigeni ulizokuja nazo ukabadili pale BOT ndio uingie mtaani kula bata na warembo na kwenda kijijini kapaua nyumba toka kwenye tembe kuwa za bati.

Serikali ilikuwa inajua nani leo kabadilisha shilingi kwenda kwenye dola,na nani kabadili dola kwenda kwenye shilingi.Kiwango cha dola kilichopo ndani ya nchi kilifahamika maana ulikuwa huwezi kupata "Bureau de change" mtaani,isipokuwa za "magendo" kwa wahindi fulani Kkoo na mitaa ya Upanga,ambao wao walienda nazo Kenya kimagendo.

Mwaka mmoja kuna mzee karani wa BOT,ndugu wa mwanasiasa fulani,alinidhulumu karibu shilingi laki mbili za Kitanzania,ambazo kwa wakati huo...Nilikuwa nina uwezo wa kununua shamba hekali 100,kujenga nyumba mbili Dsm na mbili kijini na kuwa na "guruwe" langu toka kwa mjerumani.Anasema mimi mwanafunzi,nasomeshwa na serikali,nalipiwa kila kitu siwezi kumiliki pesa zote,ni dalili za uhujumu uchumi na ukabaila.

Miaka miwili baadae,maafisa wa bandari walizuia "guruwe" langu moja kati ya mawili niliyoagiza toka kwa rafiki yangu Germany,wakasema kumiliki gari mbili ni uwizi na unyonyaji wa kujilimbikizia mali.

Huu mtindo naona sasa unarudi kulekule....Mishahara BOT,na mwisho kubadili pesa itakuwa BOT...Maana halmashauri na mashirika yote ya serikali yaliyokuwa na account benk binafsi sasa wanapeleka pesa kwenye account ya serikali beki kuu.Nafikiri hii ndio ile wanaita "Centralized System of Economy".Serikali ndio anakuwa muamuzi wa shughuli zote za kifedha katika nchi.Sasa haya mabenki binafsi ambayo mishahara ilikuwa inapita kwao watafanya biashara gani?NMB kwa walimu na CRBD kwa watumishi wa umma na mashirika ya serikali......

Nyerere aliliona hili,ndio maana akaleta ile mliita "Madaraka Mikoani".....Wanaita "D by D" yaani "Decentralization by Delegation".Ugatuaji wa madaraka!!Ukirundika kila kitu BOT,mtu akipata tatizo la mshahara akiwa Nanjilinji,tawi la BOT huko kusini ni mpaka Mbeya...Tutafika kweli??
Nadhani huu ni uhakiki wa namna nyingine kama sikosei
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom