Mishahara ya watumishi wa umma kulipwa hazina kupitia BoT | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mishahara ya watumishi wa umma kulipwa hazina kupitia BoT

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ndokeji, May 18, 2017.

 1. Ndokeji

  Ndokeji JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2017
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Wanajamii, habari za maisha!

  Serikali imeanzisha utaratibu kuanzia julai 2017 malipo ya mishahara ya watumishi wa serikali haitalipwa na hazina kupitia mabenki wakala kama ilivyo sasa bali mishahara hiyo itakuwa inalipwa na hazina kupitia BOT.

  Kwa maana hiyo majina ya kwenye payroll ya watumishi ni lazima yafanane na yale yaliyoko kwenye akaunti namba ya benki mshahara unakopita iwapo kutakuwa na tofauti yoyote hata herufi moja mtumishi anatakiwa aende bank akabadilishe ili yaweze kufanana.

  Hazina wataanza kutumia mfumo mpya wa GSPP kushirikiana na BOT. Mtumishi atayepuuza kuweka sawa hayo majina ili yaweze kuwa sawa kuna hatari ya kukoswa mshahara kuanzia July.

  Kwa hiyo jamani mfuatilie kwa afisa utumishi ili kuhakiki majina yako
   
 2. S

  Stayfar JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2017
  Joined: Jan 11, 2016
  Messages: 535
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 180
  Mkuu Ahsante mno kwa taarifa. Mi ni mhanga wa hilo
   
 3. dibwinhe

  dibwinhe Senior Member

  #3
  May 18, 2017
  Joined: Feb 12, 2013
  Messages: 102
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mfano ktk payroll nimetumia majina mawili na kule bank nimetumia na jina la ukoo hapa itakuwaje?
   
 4. Zjilala

  Zjilala JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2017
  Joined: Jun 17, 2013
  Messages: 240
  Likes Received: 199
  Trophy Points: 60
  Inakuhusu hiyo taarifa kabadirishe
   
 5. m

  mdudu JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2017
  Joined: Feb 6, 2014
  Messages: 1,164
  Likes Received: 586
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo Bashite ataandikaje? Maana mwenyejina kapatikana na anahojiwa na Takukuru Tabora
   
 6. Ndokeji

  Ndokeji JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2017
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Mara nyingi kwenye payroll huwa ni Majina Matatu..kama umetumia mawili inabidi umuone afisa utumishi wako atakusaidia
   
 7. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2017
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,480
  Likes Received: 7,495
  Trophy Points: 280
  North Korea
   
 8. moshi vijijini

  moshi vijijini JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2017
  Joined: May 14, 2015
  Messages: 3,353
  Likes Received: 1,173
  Trophy Points: 280
  Mfumo mzuri sana
   
 9. barafu

  barafu JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2017
  Joined: Apr 28, 2013
  Messages: 6,256
  Likes Received: 25,326
  Trophy Points: 280
  I see!!In 1970's wakati huo ATC imedhaminiwa na Serikali ya Uholanzi,kupitia Royal Dutch Airlines (KLM) kwenda kusomesha vijana maswala ya Aicraft Engineering and Avionics.Vijana tulipata tabu sana katika kuandaa safari.

  Ilikuwa ni lazima kwanza documents za passport ya mtu ianze kuhakikiwa na balozi wa nyumba kumi na viongozi wengine kuanzia ngazi ya kijiji mpaka Mkoa.Pale BOT wakati wa kuondoka ndio palikuwa mahali pekee ambapo tulipewa pesa za kigeni(dola).Yaani ulikuwa huwezi kupata mahali popote dola zaidi ya bank kuu,kwa hiyo hata wakati wa kurudi likizo ilikuwa ni lazima pesa za kigeni ulizokuja nazo ukabadili pale BOT ndio uingie mtaani kula bata na warembo na kwenda kijijini kapaua nyumba toka kwenye tembe kuwa za bati.

  Serikali ilikuwa inajua nani leo kabadilisha shilingi kwenda kwenye dola,na nani kabadili dola kwenda kwenye shilingi.Kiwango cha dola kilichopo ndani ya nchi kilifahamika maana ulikuwa huwezi kupata "Bureau de change" mtaani,isipokuwa za "magendo" kwa wahindi fulani Kkoo na mitaa ya Upanga,ambao wao walienda nazo Kenya kimagendo.

  Mwaka mmoja kuna mzee karani wa BOT,ndugu wa mwanasiasa fulani,alinidhulumu karibu shilingi laki mbili za Kitanzania,ambazo kwa wakati huo...Nilikuwa nina uwezo wa kununua shamba hekali 100,kujenga nyumba mbili Dsm na mbili kijini na kuwa na "guruwe" langu toka kwa mjerumani.Anasema mimi mwanafunzi,nasomeshwa na serikali,nalipiwa kila kitu siwezi kumiliki pesa zote,ni dalili za uhujumu uchumi na ukabaila.

  Miaka miwili baadae,maafisa wa bandari walizuia "guruwe" langu moja kati ya mawili niliyoagiza toka kwa rafiki yangu Germany,wakasema kumiliki gari mbili ni uwizi na unyonyaji wa kujilimbikizia mali.

  Huu mtindo naona sasa unarudi kulekule....Mishahara BOT,na mwisho kubadili pesa itakuwa BOT...Maana halmashauri na mashirika yote ya serikali yaliyokuwa na account benk binafsi sasa wanapeleka pesa kwenye account ya serikali beki kuu.Nafikiri hii ndio ile wanaita "Centralized System of Economy".Serikali ndio anakuwa muamuzi wa shughuli zote za kifedha katika nchi.Sasa haya mabenki binafsi ambayo mishahara ilikuwa inapita kwao watafanya biashara gani?NMB kwa walimu na CRBD kwa watumishi wa umma na mashirika ya serikali......

  Nyerere aliliona hili,ndio maana akaleta ile mliita "Madaraka Mikoani".....Wanaita "D by D" yaani "Decentralization by Delegation".Ugatuaji wa madaraka!!Ukirundika kila kitu BOT,mtu akipata tatizo la mshahara akiwa Nanjilinji,tawi la BOT huko kusini ni mpaka Mbeya...Tutafika kweli??
   
 10. balimar

  balimar JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2017
  Joined: Sep 18, 2015
  Messages: 2,832
  Likes Received: 3,366
  Trophy Points: 280
  Kesho uwahi asubuhi hapa benki na picha tatu za passport barua ya mtendaji au kitambulisho na 20000 processing fees
   
 11. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2017
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,549
  Likes Received: 7,605
  Trophy Points: 280
  Hii ni changamoto ambayo Serikali imechangia. Enzi zile mtoto akiandikishwa shule ni majina mawili; lake na la baba. Hapakuwa ni kitu kama jina la ukoo au la tatu.

  Ukiingia sekondari ni lazima uendelee na majina yako. Tasisi nyingine kama mabenki wanataka majina matatu hivyo ni lazima ulitafute.
  Kwa utaratibu huo ni wachache sana ambao wana consistence ya majina mwanzo mwisho potelea mbali wale wanaofanya hivyo purposely kama vyeti feki. Wengine wakiolewa wanabadili majina shida tupu. Nchi inatakiwa kuwa na utaratibu unaoeleweka wa majina na wananchi waelimishwe umuhimu wa consistence kwenye majina na namna ya kulinda hiyo consistence anapotokea kidudu mtu kuandika jina lako anavyojisikia yeye. Wanangu nimewafundisha vitu viwili muhimu ambavyo haviruhusiwi kuchezewa - jina na tarehe ya kuzaliwa.
   
 12. rweyy

  rweyy Senior Member

  #12
  May 18, 2017
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  ina maana hao ni wa mikoani tu wilaya nyingi hazina bot
   
 13. barafu

  barafu JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2017
  Joined: Apr 28, 2013
  Messages: 6,256
  Likes Received: 25,326
  Trophy Points: 280
  Mimi pia ningefurahi kupata ufafanuzi toka kwa wahusika,kuhusiana na swali uliloliuliza
   
 14. The seer

  The seer JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2017
  Joined: Jul 31, 2015
  Messages: 202
  Likes Received: 226
  Trophy Points: 60
  Hii taarifa inatembea kwenye mitandao ya kijamii.haijulikani source ni wapi.hii Tanzania MTU tu akiwa na smart phone anajifanya afisa habari .
   
 15. U

  UCD JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2017
  Joined: Aug 17, 2012
  Messages: 3,242
  Likes Received: 2,150
  Trophy Points: 280
  Ni uelewa tu mkuu!! Mpaka sasa hivi pesa za mishahara zinalipwa kupitia BOT yaani Hazina wana akaunti BOT ila pesa zinakuwa transferred kwenda commercial banks kutoka BOT ambako mtumishi ana akaunti yake. Nafikiri wanachotaka ni verification ya majina kati ya payroll na akaunti zilizoko kwenye commercial banks. Hivyo mtumishi ataendelea kulipwa pesa zake kwenye commercial banks
   
 16. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2017
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 23,145
  Likes Received: 14,360
  Trophy Points: 280
  kupitia BOT au accaunt za halmashauri?
   
 17. C

  CHAZA JF-Expert Member

  #17
  May 18, 2017
  Joined: Dec 21, 2012
  Messages: 6,795
  Likes Received: 2,255
  Trophy Points: 280
  Hayana sana sababu kwa wakati huu. Ni kurudi kinyumenyume. Cha msingi ni kuongeza udhibiti. Sasa tupo watu 50± million,na kwa hiyo mifumo ya kisasa ya udhibiti ni muhimu,lakini isiwe mambo ya kizamani ambayo kwa wakati huo ilikua ni ya kisasa. Leo ni wakati wa digitali.
   
 18. C

  CHAZA JF-Expert Member

  #18
  May 18, 2017
  Joined: Dec 21, 2012
  Messages: 6,795
  Likes Received: 2,255
  Trophy Points: 280
  Tawi la BOT kubwa lipo Mtwara
   
 19. Ugiligili

  Ugiligili JF-Expert Member

  #19
  May 18, 2017
  Joined: Jun 20, 2014
  Messages: 1,978
  Likes Received: 1,712
  Trophy Points: 280
  Sina uelewa juu ya hili..ila kama ni zuri tuombe lilete matokeo chanya..
   
 20. T

  Tulimumu JF-Expert Member

  #20
  May 18, 2017
  Joined: Mar 11, 2013
  Messages: 8,335
  Likes Received: 4,133
  Trophy Points: 280
  Umeambiwa huyo siyo mtumishi wa serikali ila ni mwanasiasa
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...