Mishahara ya watumishi halmashauri yasimamishwa ................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Mishahara ya watumishi halmashauri yasimamishwa Send to a friend Tuesday, 30 November 2010 20:49 0diggsdigg

Mwanja Ibadi, Lindi
UONGOZI wa Halmashauri ya Lindi vijijini, umesimamisha kwa muda usiojulikana malipo ya mishahara ya watumishi wake zaidi ya 224 wa idara mbalimbali.
Idara ambazo zimekubwa na hatua hiyo ni utawala, elimu na afya na kwamba, inatokana na kushindwa kuwasilisha fedha na vitabu vya kukusanya mapato.
Watumishi waliokumbwa na zoezi hilo ni watendaji wa vijiji, kata, waganga wa vituo vya afya, zahanati na walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari.

Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa, baadhi ya watumishi hao walisema itendo cha kusimamisha mishahara yao kimewaathiri kwa kiwango kikubwa.
“Tulipofika benki akaunti zetu tulikuta zikiwa tupu bila kuingiziwa chochote, tulipojaribu kuona uongozi akiwamo ofisa mapato, walitueleza wamesimamisha kwa vile hatujawasilisha vitabu vya kukusanyia mapato,” alilalamika mmoja wa watumishi hao.
Hata hivyo, baadhi ya watumishi hao wakiwa na vitabu mikononi vya kukusanyia mapato vikiwa kwenye mtiririko wa namba 0063401 hadi 0063450, kilichoanza kazi Agosti 9, 2009 vinaonyesha kumalizika na kukaguliwa na mkaguzi wa hesabu wa halmashauri hiyo.

Walisema kinachowasikitisha zaidi, ni kusimamisha mishahara yao bila uongozi kuwapa taarifa.
“Kwa kawaida pale tunapochelewa kuwasilisha vitabu hivyo kwa ajili ya ukaguzi, tunapewa taarifa zikiwamo barua, lakini safari hii kitu kama hicho hakikuwepo zaidi ya kusimamishwa malipo yetu,” alisema watumishi mmoja.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Lindi vijijini, Seleman Ngaweje, alithibitisha kuzuia malipo hayo na kwamba, wapo baadhi ya watumishi hawajawasilisha makusanyo na vitabu walivyokabidhiwa kwa muda mrefu.

“Tumezuia mishahara yao kuwataka wawasilishe fedha walizokusanya na kukaguliwa kwa vitabu vyao walivyokabidhiwa, lengo la ofisi iweze kuweka vizuri kumbukumbu za hesabu zake,” alisema Ngaweje.
Ngaweje alisema lengo la kusimamisha malipo ya watumishi hao, ni kuwataka waliopewa jukumu la ukusanyaji mapato kuwasilisha fedha walizopata kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato.
 
Kaza uzi mpaka kieleweke. Wao wanaifanya Halmashauri kama shamba la bibi?
 
Back
Top Bottom