Mishahara ya wabunge, mawaziri na majaji juu!

Ngoja nianze kulia kama dakika mbili hivi. uwi, uwi, eeeh, eeeeeeeeeeeh. uuuuuh.

GM7 nyamaza kulia naona machungu mpaka yamepitiliza sijui lini sie watoto wa wakulima tutakuja fanikiwa kimaisha.
 
mshahara wa rais ni shilingi ngapi?..........
naomba msaada...
 
wakati kuna nchi nyingi wamefreeze malipo ya watu wao wa serikali kutokana na uchumi kuwa mbovu nchi yetu yenye viongozi waliojaa ubinafsi wanaona huu ndio wakati muafaka kuongeza mishahara yao maradufu.
 
Jamani kweli serikali yetu haina priorities! Mahospitali hakuna dawa na watu wa chini wanazidi kupigika wao ndio kwaaaanza wanagawana jasho letu!
 
as far as i know,''A HUMAN IS A SELFISH-BEING''.any human!sitashangaa hata mimi ninaelalamika hapa kesho nikiingia kwenye system i become the worst person
 
hiyo mishahara wanayo ongezeana ama kupeana ingetosha kuweka umeme katika Zahanani ngapi vijini, madawa kiasi gani yangenunuliwa kwenye mahospitali yetu, vitanda vya wagonjwa vingenunuliwa watu waache kulala chini ama sakafuni, madawati mangapi yangenunuliwa watoto wetu walala hoi waache kukalia matofali au kukaa sakafuni.
 
Sioni mantiki ya post hii kutolewa na gazeti la mwananchi kwani gazeti hili ni moja ya vyombo vya habari visibyolipa mishahara ya wafanyakazi wao.

ebu fikiria gazeti linaingiza mapato ya shj milini 11 kwa siku kisha mwandishi wao analipwa sh 60,000 kwa mwezi kisha wanaandika habari kama hiyo ufisadi na matumizi mabaya ya fedha ni kwa serikali tu?
 
Kwani ni kigezo kipi kimetumika kuwaongezea hao hiyo mishahara??? Ni kazi ipi walioifanya hadi JK na serikali yake waongeze mishahara?
1. Kukaa bungeni na kulala
2. Kukaa bungeni na kuongea pointless
3. kukaa bungeni na kuwapongeza mafisadi.

Nina machungu makubwa sijui nifanyeje kweli nashindwa kuvumilia ningekuwa na uwezo ningepinga hilo ongezeko lao la mishahara. Wabunge wote wanakaa mijini matatizo ya jimboni mwao hawayajui ukifanya sensa ya mbunge anaye kwenda jimboni kwake( maisha yake shughuli zake ni huko jimboni kwake tena kijijini hasa sio mjini) na kukaa huko hadi kipindi cha bunge kinapofikia sijui kama watapatikana. Wabunge wote wako mjini kuponda raha tu.

Nadhani kuna haja ya sheria ipitishwe wabunge wote lazima wakae jimboni kwake kama mabwana shamba tumewachoka kuwaona mijini
 
hawa watu wanastahili kulipwa huu mshahara basi,sasa marupurupu yanini tena?hawafanyi kazi kustahili hela yote lita 100 za fuel par week?simu?house?mavazi?ndo sababu wapo radhi hata kupindisha mambo waendelee kuwepo,wangekuwa wanafanya kazi yao kama sisi huku chini tungekuwa mbali.wao wanahangaikia maslahi yao zaidi,then watamkumbuka mnyonge saa ngapi? Na huyu JK kuchagua majaji wa mahakama kuu wengi namna hiyo ni wa nini?au watanzania wahalifu wengi sana?sipati picha kujiongezea mzigo nakatwa PAYE,VAT kila ukifanya urchase unanyongwa then mwingine anapewa ni marupurupu,why kusiwe na salary tu then basi?sisi wengine tunaishi vipi kwani?thats why hawana uchungu na NCHI
 
Mishahara ya wabunge,mawaziri na majaji imepandisha huku wa spika wa bunge ukipanda mara dufu.
Kwa kifupi tu;

Spika na Jaji mkuu Tshs 2,760,000/= mpaka 4,850,000/=
Naibu spika Tshs 2,080,000/= mpaka 2,172,000/=
Mbunge Tshs 1,840,000/= Mpaka 1,921,000/=
jaji wa mahaka kuu tshs 2,160,000/= mpaka 3,645,000/=
jaji Mahakam ya rufaa Tshs 2,310,000 mpaka 4,250,000/=

Wakuu ninchoomba kuelewesha inamaana kwa kuwa spika ni mbunge kwa hiyo anakula na mishahara mingine ya ubunge au?

Kwa hali hii kweli tutapona?
Source:Mwananchi news paper la leo

Serikali ya kifisadi hii. Wakati wanadai nchi imeathirika kwa hali mbaya ya uchumi duniani na hivyo kushindwa kuongeza kima cha chini cha mishahara, lakini kwa wengine mishahara inaongezwa kama kazi.

Vipi kuhusu mishahara ya Walimu wa shule za msingi, vyuo vyetu vikuu, manesi, madaktari, polisi na umma wa Wafanyakazi wa Tanzania mbao mishahara wanayoipata haiendani na hali halisi ya gharama za maisha ya kila siku? Kulikuwa na sababu yoyote ya msingi kuwaongezea wahusika mishahara ambapo tayari wana mishahara ya juu badala ya watu muhimu sana katika Tanzania ambao wanalalamika kuhusu mishahara midogo?
 
Sioni mantiki ya post hii kutolewa na gazeti la mwananchi kwani gazeti hili ni moja ya vyombo vya habari visibyolipa mishahara ya wafanyakazi wao.

ebu fikiria gazeti linaingiza mapato ya shj milini 11 kwa siku kisha mwandishi wao analipwa sh 60,000 kwa mwezi kisha wanaandika habari kama hiyo ufisadi na matumizi mabaya ya fedha ni kwa serikali tu?

Bw.Ukoko,

Anzisha thread mpya tafadhali!

Ahsante kwa uzalendo na ujasiri wako!
 
Sioni kosa la nyongeza za mshahara kwa wafanyakazi wa serikali.
Shida yangu inaanzia pale ambapo kila mwaka baada ya mwaka anaongezewa mwanasiasa tu. Wengine wanabaki kilio tu, na ngoja ufike uchaguzi usikie, hao haowanaodhulumiwa ndio wa kwanza kushirikiana na wezi hawa kuiba kura za wananchi, na hawa hawa utaona wana kimbia wamevaa fulana na kofia za kidumu chama cha manyanyaso na ufisadi!
Kazi kweli kweli!
 
mnasema walimu wa sekondari na msingi tu,mimi naomba kuuliza lecturer msaidizi analipwa kiasi gani?
 
Wakuu inawezekana walisahau kuongeza mishahara ya Raisi, Makamu wake pamoja na Waziri Mkuu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom