Mishahara ya mwezi Februari itatoka lini?serikali mbona inatudhalilisha watumishi wake?

Jana jioni mwenye dhamana ya mishahara udom, katoa barua ya kusema hajapokea fedha yoyote kutoka hazina kwa hiyo hakuna mshahara mpaka atakapo pata fedha, sio kosa lake kasema ukweli mimi nalia na mkuu wa kaya j.k.

Mbona mnatudhalilisha mjini hapa? Sijui tasisi nyingine za serikali kama wamelipwa ila hapa matangazo yameshatoka kuwa mpunga haujaingia kutoka serikalini.

Tunaishije mjini hapa?spika makinda anna anajua vizuri ugumu wa maisha dodoma ndio maana anakomalia posho,sasa tusiokuwa na posho na tunaishi dodoma miaka yote tunafanyeje?hali mbaya!!!!!!!!

SIO DUCE NA UDOM TU HATA OUT BADO hatujapata
 
Pesa zote kamaliza Vasco Dagama na anavyo zurula dah, hazina huko kwishney
 
Jana jioni mwenye dhamana ya mishahara udom, katoa barua ya kusema hajapokea fedha yoyote kutoka hazina kwa hiyo hakuna mshahara mpaka atakapo pata fedha, sio kosa lake kasema ukweli mimi nalia na mkuu wa kaya j.k.

Mbona mnatudhalilisha mjini hapa? Sijui tasisi nyingine za serikali kama wamelipwa ila hapa matangazo yameshatoka kuwa mpunga haujaingia kutoka serikalini.

Tunaishije mjini hapa?spika makinda anna anajua vizuri ugumu wa maisha dodoma ndio maana anakomalia posho,sasa tusiokuwa na posho na tunaishi dodoma miaka yote tunafanyeje?hali mbaya!!!!!!!!

he!halmashauri ya wilaya ya mufindi tumepokea mishahara toka tr 24 feb,polen sn
 
ani ngojeni wakusanye kwanza Makadiro ya kodi za Mapato ya biashara za makabwela.

Yaani mkuu hakuna kitu kinanikera kama hicho. Utaona TRA wanazunguka kwenye viduka vidogo vidogo na kukamata magari kwa ajili ya road license wakati wanasamehe kodi kubwa kwa wawekezaji wanaokwapua rasilimali zetu. Hivi nchi hii ni lini itakombolewa?
 
Jana jioni mwenye dhamana ya mishahara udom, katoa barua ya kusema hajapokea fedha yoyote kutoka hazina kwa hiyo hakuna mshahara mpaka atakapo pata fedha, sio kosa lake kasema ukweli mimi nalia na mkuu wa kaya j.k.

Mbona mnatudhalilisha mjini hapa? Sijui tasisi nyingine za serikali kama wamelipwa ila hapa matangazo yameshatoka kuwa mpunga haujaingia kutoka serikalini.

Tunaishije mjini hapa?spika makinda anna anajua vizuri ugumu wa maisha dodoma ndio maana anakomalia posho,sasa tusiokuwa na posho na tunaishi dodoma miaka yote tunafanyeje?hali mbaya!!!!!!!!

Mkuu Tangazo kama hilo nilikuta UDSM wakati napita zangu kwa hiyo kilio ni cha wengi.
 
kama ni udom na niliwahi kusikia kuna mtu anaukoo na smiling killer jk anaitwa mlacha. ukichanganya hao wawili basi nyie mtapata salary trh 15
 
mwezi huu wamejitahidi kuwalipa madaktari kwanza nyie wengine mtasubiri kwanza hadi zipatikane, c umeona hata wabunge wamegomewa nyongeza? tuvumilie hali serikali nimbaya kifedha
ACHA UONGO WE *****! Hakuna daktari aliyelipwa, subiri tarehe tatu kitanuka tena.
KAMA WEWE NI DAKTARI WAMEFUGO NDO UMELIPWA HONGERA. ILA WA BINADAMU BADO
 
Kuliko Serikali kuwa na idadi kubwa ya wafanyakazi isiyoweza kuwalipa kwanini wasifanye uchambuzi yakinifu kujua mahitaji halisi kwa kazi zilizopo na wengine waje huku sekta binafsi? Sera ya "full employment" haifanyi kazi kwenye uchumi huria kwanza inakandamiza ukuaji wa sekta binafsi.

Ukifuatilia sana serikalini wamejaza wasomi na hawana kazi zinazoendana na visomo vyao hivyo wangewekwa kando (jobless) wangejitambua na kutumia visomo vyao kuinua pato la taifa.
Mkuu, kwa taarifa yako waliojaa ni wafanyakazi hewa... kama serikali ikiweza kudhibiti idadi ya wafanyakazi halali si kubwa sana kuimudu
 
Picture1.png
431182_321862354528766_100001150132848_818925_18544395_n.jpg

:shock:
 
Jana jioni mwenye dhamana ya mishahara udom, katoa barua ya kusema hajapokea fedha yoyote kutoka hazina kwa hiyo hakuna mshahara mpaka atakapo pata fedha, sio kosa lake kasema ukweli mimi nalia na mkuu wa kaya j.k.

Mbona mnatudhalilisha mjini hapa? Sijui tasisi nyingine za serikali kama wamelipwa ila hapa matangazo yameshatoka kuwa mpunga haujaingia kutoka serikalini.

Tunaishije mjini hapa?spika makinda anna anajua vizuri ugumu wa maisha dodoma ndio maana anakomalia posho,sasa tusiokuwa na posho na tunaishi dodoma miaka yote tunafanyeje?hali mbaya!!!!!!!!

Uzeni ''paper'' hii nchi unatakiwa uifisadi kutegemea mahali ulipo.

Utajiri mnao ila mmeukalia halafu mwalalamika kwani hamjui huu mwezi umewahi kuisha kabla wakubwa hawajamaliza kuuza zile karatasi zinazoitwa T-bonds pale BOT ili mlipwe.?

Tahadhari: Akili za mbayu wayu changanya na zako
 
Walimu wapya waonja joto ya jiwe

• WANYIMWA FEDHA ZA KUJIKIMU, WAGOMA KUFUNDISHA

na Mwandishi wetu

MAISHA ya walimu wapya walioajiriwa hivi karibuni na kupangiwa vituo vya kazi sehemu mbalimbali nchini, yanaendelea kuwa magumu baada ya serikali kushindwa kuwalipa fedha zao za kujikimu tangu waliporipoti.

Malalamiko ya walimu hao yamekuwa yakisikika takriban kutoka mikoa yote nchini, ambapo mbali na fedha za kujikimu, hawajalipwa pia mshahara wa Februari mwaka huu na fedha za kusafirisha mizigo.

Taarifa zilizokusanywa na Tanzania Daima kutoka jijini Mwanza, Bunda, mkoani Mara na Bariadi, mkoani Shinyanga, jana, zilionyesha kuwa walimu wapya hawakufanya kazi na badala yake waliendesha mgomo baridi wa kutoingia madarasani na wengine waliandamana kushinikiza kulipwa fedha hizo.

Kutoka mkoani Mwanza, Sitta Tuma, anaripoti kuwa walimu hao wa shule za sekondari, walilazimika kuacha kufundisha kwa siku nzima, kisha kwenda kupiga kambi katika ofisi za jiji kwa lengo la kushinikiza kulipwa mishahara yao ya Februari mwaka huu.

Walimu hao walifika kwenye ofisi hizo wakilalamikia kitendo walichodai ni kupigwa danadana na maofisa wa jiji hilo juu ya kulipwa haki zao, na hivyo kukataa kuondoka hadi walipwe.

Wakizungumza kwa jazba, walilalamikia manyanyaso waliyodai kufanyiwa na ofisi ya Utumishi na Idara ya Sekondari ya Jiji, wakisema kuwa mishahara iliyoidhinishwa kwa ajili ya walimu wenye digrii na diploma imekatwa tofauti na maelekezo ya serikali.

Walimu wa ngazi ya diploma nao waliungana na wenzao kulalamikia kukatwa mishahara yao kinyume na utaratibu, wakisema kuwa walipaswa kupewa mshahara wa sh 325,700 lakini walilipwa sh 290,600, hivyo sh 35,100 walikuwa wakikatwa.

Hata hivyo, walimu hao walisema tangu waanze kazi Januari Mosi mwaka huu, serikali ya jiji hilo haijawalipa fedha zao za nauli na mizigo, tofauti na ilivyoelezwa na serikali kuu kuwa sh bilioni 6.2 zilishapelekwa Mwanza kwa lengo la kulipa nauli na mizigo wakati wakienda kuripoti.

Wakati hali ikiwa hivyo, jijini Mwanza, Ahmed Makongo anaripoti kutoka Bunda mkoani Mara akisema kuwa walimu zaidi ya 100 walioajiriwa hivi karibuni jana waliandamana hadi makao makuu ya halmashauri hiyo, wakidai madai yao mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kucheleweshewa mishahara yao.

Wakizungumza na Tanzania Daima, walisema kuwa wameamua kuandamana kwenda kumuona mkurugenzi wa halmashauri hiyo, ili aweze kuwalipa madai yao yote kwani kwa sasa wanaishi maisha ya kubahatisha kutokana na ukata walionao.

Walisema kuwa wakati wanaajiriwa Januari mwaka huu na kupangiwa vituo vya kazi, serikali iliwaambia kuwa watalipwa haki zao zote, ikiwa ni pamoja na posho za kujikimu, fedha za nauli na mizigo yao.

"Tumefika kazini, hakuna nyumba za walimu na hivyo tunalazimika kuishi kwenye nyumba za kulala wageni, na sasa tunadaiwa fedha nyingi, mizigo yetu imeshikiliwa na wenye nyumba," alisema mmoja wao akiungwa mkono na wenzake.

Naye, Samwel Mwanga kutoka Bariadi mkoani Shinyanga, anasema kuwa walimu wa shule za msingi na sekondari wameanza mgomo baridi wa kutofundisha licha ya kauli za kejeli dhidi yao zilizotolewa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Deogratius Hella.

Wakizungumza na Tanzania Daima jana katika ofisi ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wilayani hapa, walimu hao walisema kuwa wataendelea na mgomo huo hadi hapo serikali itakapokubali kuyalipa madeni yao licha ya kutoa vitisho vya kumkamata kiongozi wao, Ponsia Gervas.

Walisema kuwa wao wataendelea kufika katika eneo la kazi lakini hawatafundisha hadi hapo serikali itakapokubali kulipa madeni ya malimbikizo ya fedha zao bila vitisho.

‘Sisi tutaendelea kufika katika maeneo yetu ya vituo vya kazi lakini hatuwezi kuingia madarasani hadi hapo serikali itakapotulipa madeni yetu kwani tumechoka kunyanyaswa," alisema Emanuel Paul.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika shule za msingi Kidinda, Somanda(A), Somanda (B), Sima, Bariadi na sekondari za Bariadi na Kidinda, ulibaini walimu kutoingia madarasani na badala yake wanafunzi walikuwa wakiendelea na michezo viwanjani.

Katibu wa CWT, Gervas, alisema kuwa kitendo cha serikali kushindwa kulipa madeni ya walimu huku baadhi ya viongozi kuwabeza kwa kutoa kauli za kejeli kitaleta athari kubwa.

Naye, mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi, Hella, alisema kuwa hana fedha za kuwalipa walimu hao hadi hapo atakapopata fedha kutoka hazina.
TZ Daima
 
Ina maana we unaishi kwa kutegemea mshahara tu? imeandikwa mtu hataishi kwa mkate tu mkuu!

Sasa niishi kwa kutegemea nini kingine? Yaani mtu asome na kufaulu kwa daraja la juu ktk kila ngazi ya elimu, lakini bado asiweze kuendesha maisha yake kwa mshahara? Hapa la msingi ni kwa serikali kuthamini wasomi na wataalam wake. Ni bahati mbaya sana kwamba wenye elimu na wataalamu hawapewi kipaumbele ktk nchi zinazoendelea, badala yake wanasiasa ndo wanapeta.

Vilevile, kuna wafanyakazi wengine wa serikali (e.g. BOT) wanaoishi kwa staha bila kulazimika "kufuga kuku au ngómbe"! Iweje tutegemee wasomi wetu waache shughuli zinazoendana na taaluma zao ili waweze kufungua duka na kufuga mbuzi ndipo waishi kwa staha (sio maisha ya anasa)? Ni wakati wa kuishinikiza serikali kuwalipa wafanyakazi wake pesa inayoendana na hali halisi ya maisha na taaluma zao.
 
Back
Top Bottom