Mishahara ya mwezi Dec kuna hatihati isilipwe. Huenda ikaunganishwa na ile ya mwezi January.

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Amenaswa kiongozi mmoja kijana wa ngazi za juu hazina akiongea kwa simu na mtu ambaye hakufahamika mara moja. "Kuna tatizo hapa, pesa hakuna. Hata mishahara ya mwezi huu ni kizunguzungu, Juhudi zinafanyika ili pesa ipatikane mapema kwa ajili ya mishahara ya mwezi dec. Kuna baadhi ya idara nyeti watalipwa mapema mshahara wa dec, wapo pia watakaolipwa mishahara nusu. Isipokuwa kwa idara ya elimu hali itakuwa ngumu kidogo. Pengine mishahara yao ya mwezi dec wakalipwa tarehe za kati kati ya mwezi january....Akaingia ofisini na kujifungia huku akiendelea kuongea. Haya, wale wenye visanduku vya uvunguni wajiandae kuvibomoa.
 
mmmmmmmmmmmm!
Hata mie nilishanga kuona wanajeshi wamecheleweshewa sana mshahara japo mpaka sasa wamelipwa.maskini kikwete aibu hii utaipata wapi na mtu ambaye unge mkimbilia haraka wameshamuua(gadaff)kazi unayo najiua utakimbilia kulipa majeshi yako amabyo hutawanya maandamano ya wadai haki
 
Msiwe na wasi wasi ni kipindi tu cha mpito wakati serikali inajiandaa kulipa denila DOWANS, once likilipwa, mambo yatakuwa mazuri kama zamani: namaanisha maziwa na asali. Ila polisi tutawalipa kwanza ili nao wasije wakaandamana.,tehe tehe tehe!
 
si mkulo alikana kuwa serikali haijafilisika atashangaa sasa....jk alidhani ni rahisi kuwa rais wa nchi...
 
amenaswa kiongozi mmoja kijana wa ngazi za juu hazina akiongea kwa simu na mtu ambaye hakufahamika mara moja. "kuna tatizo hapa, pesa hakuna. Hata mishahara ya mwezi huu ni kizunguzungu, juhudi zinafanyika ili pesa ipatikane mapema kwa ajili ya mishahara ya mwezi dec. Kuna baadhi ya idara nyeti watalipwa mapema mshahara wa dec, wapo pia watakaolipwa mishahara nusu. Isipokuwa kwa idara ya elimu hali itakuwa ngumu kidogo. Pengine mishahara yao ya mwezi dec wakalipwa tarehe za kati kati ya mwezi january....akaingia ofisini na kujifungia huku akiendelea kuongea. Haya, wale wenye visanduku vya uvunguni wajiandae kuvibomoa.

pole mkuu bado uko serikwanini???komaeni muandamane
 
NGOJA MI NIFANYE MIKATABA MIBOVU ILI NIJE NIWAKOPESHE HAO JAMAA mtapata mishahara tena $DOLA na mkopo wa us dola.
 
Mungu apishe mbali na iishie kuwa uvumi kwani katika masuala tata ndani ya hii nchi ni mishahara, mishahara yenyewe haitoshi halafu icheleweshwe mpaka December hii kwa vyovyote itaweza kumfanya bubu yeyote atake kuongea.
 
NGOJA MI NIFANYE MIKATABA MIBOVU ILI NIJE NIWAKOPESHE HAO JAMAA mtapata mishahara tena $DOLA na mkopo wa us dola.


mkuu kisesa umenichekesha sana
jana nilikuwa napeleka gari kurekebisha a/c nkakuta magari mazuri aisee yamepangana ilala kama yanauzwa nikauliza ya nani nikaambiwa kuna kijana wa kichga anafanya kazi ya kukopesha aisee hayo unayoyaona ni madogo ana magari kama 10 na amana zake ni gari tu akiridhika na hela anayokupa ukishindwa siku moja imetoka mpwa yaani nikaogopa
 
Chanzo chako sikiamini ni kama uzushi fulani, lakini ukweli ni huu. TPDF wameshalipwa, Police mkoa wa Dar -Es - Salaam wameshalipwa, Magereza bado wote, Uhamiaji nao bado hawajalipwa. Tatizo mpaka sasa hundi toka hazina ilikuwa bado haijapelekwa idara husika ili mishahara ipelekwe banki kwani watumishi wengi wanapokelea bank.
Idara nyingine bado nazifuatilia lakini bila ya shaka nazo hazijalipwa.
 
Back
Top Bottom