Mishahara ya madaktari!

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
WATUMISHI wa sekta ya afya wataka mshahara wa madaktari kuwa Sh 2milioni
Na Nora Damian

WATUMISHI wa sekta ya afya nchini wamependekeza kima cha chini cha mshahara kuwa Sh500,000 na cha juu kuwa Sh2,500,000 kwa kada ya udaktari wakati wauguzi wametaka kuwa kati ya Sh400,000 na Sh800,000 kwa mwezi.

Hayo yalisemwa jana jijini na Mkurugenzi wa Umoja wa Vyama vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karsan baada ya umoja huo kufanya uchunguzi wa kihabari na watumishi hao kupendekeza kiasi hicho.

Karsan alisema uchunguzi huo, ulifanyika Oktoba mwaka jana hadi Januari mwaka huu na watumishi hao kupendekeza kuwa walipwe kiasi hicho kwa kuwa maisha ni magumu na hivyo wanataka walipwe kiasi hicho.

Mkurugenzi huyo alisema, jumla ya wafanyakazi 230 wa sekta hiyo katika mikoa husika walihojiwa na kusema kuwa kutokana na gharama za maisha kupanda, wanalazimika kutumia asilimia 60 ya muda wao kufanya kazi katika hospitali binafsi, biashara, kilimo na kulisha mifugo ili kukabiliana na hali hiyo.

Alisema wafanyakazi walioajiriwa na serikali au na taasisi binafsi walilalamika kulipwa mishahara midogo na kwamba asilimia 70 kwa nyakati tofauti, walisema hawalipwi marupurupu yoyote kama vile posho ya usafiri, malipo ya ziada, posho ya mazingira magumu na posho ya matibabu.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, wafanyakazi walioajiriwa walilalamika kuwa hawapati nafasi za masomo ya kujiendeleza bila kutoa rushwa ya ngono kwa wanawake na kutoa fedha kama rushwa.

Katika uchunguzi huo pia, asilimia 90 ya wafanyakazi waliohojiwa walisema kuwa hawapewi nyumba na waajiri wao wakati wafanyakazi wa Zahanati ya Endasaki wilayani Babati, walisema wanalazimika kulala kazini kutokana na hofu ya kuliwa na simba wanapokuwa zamu za usiku.


Uchunguzi huo, ulifanywa katika mikoa ya Mtwara, Kigoma, Shinyanga, Ruvuma, Manyara, Rukwa, Arusha na Dodoma.
 
Sawa,
1. Wafanyakazi Afya walipwe 2.4m hata zaidi.... haina neno! Kwani hayo mashangingi na gharama la kuyaendesha ni kiasi gani?
Kama Mshahara wa daktari mmoja ni 2.4m *12 = 28.8 m. (Kwa mwaka). Kununua shangingi 1 analotumia Mkurugenzi wa Kawaida tu Wizarani utalipa madaktari watatu! Achilia mbali gharama ya uendeshaji wa hilo shangingi!

2. Sii kweli serikali haina pesa- ni matumizi tu makubwa ya kifahari na kuwasahau walalahoi! Kama serikali ikiamua kudhiditi matumizi na kuachanana na ufahari- then itapatikana pesa kuwalipa vizuri tu wafanyakazi!
 
Naomba wanaJF mnisaidie katika mjadala huu, maana nahisi labda mwandishi wa habari kakosea hii figure, labda kafuta sifuri moja mwishoni! Hasa Ndugu Dotori naomba mchango wako maana ni wewe pekee ninayekumbuka katika forum hii ambaye umejitambulisha ni daktari. Na wengine pia tafadhali.

Ati ni kweli daktari bingwa huko Zanzibar baada ya kupandishwa mshahara mwaka huu ndo sasa analipwa sh laki na nusu (150,000) kwa mwezi?
Gazeti la Majira la leo lina habari kuwa wamegomea mishahara hiyo, kama nilivyobandika hapa chini.

Madaktari Zanzibar wagomea mishahara


Na Ali Suleiman, Zanzibar

WAFANYAKAZI wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakiwamo madaktari bingwa, wamegomea mishahara mipya iliyotolewa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kwa madai kwamba ni midogo kulingana na taaluma zao.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Bw. Sultani Mungheiry, alikiri jana kuwapo tatizo hilo na kusema wizara yake inafanya marekebisho ya viwango vipya vya mishahara.

"Ni kweli tatizo lipo tunalifanyia kazi, kuona viwango vipya vilivyotangazwa na Serikali vinawanufaisha wafanyakazi wa Wizara ya Afya, wakiwamo madaktari," alisema.

Yamejitokeza malalamiko kwa watumishi wa SMZ baada ya kutangazwa kwa viwango vipya vya mishahara na Serikali.

Ofisa wa Idara ya Utumishi, alikiri kuwapo kwa tatizo hilo na idara hiyo kutoa tamko la wafanyakazi kuchukua mishahara hiyo hadi itakapofanyiwa marekebisho.

Kasoro kubwa zilizojitokeza katika mishahara mipya ni kwamba baadhi ya watendaji wakuu wa Serikali, wakiwamo wakurugenzi wa Serikali kupata mishahara midogo, tofauti na watumishi wao.

Hatua hiyo imefanya baadhi ya wakurugenzi kutishia kugoma kupokea mishahara mipya, iliyotangazwa na SMZ.

Hivi karibuni, Rais Amani Abeid Karume, aliwataka watumishi wa SMZ kuvuta subira huku marekebisho ya mishahara mipya yakifanywa.

Daktari bingwa katika Wizara ya Afya ambaye hakutaka jina lake litajwe, iliitaka wizara hiyo kurekebisha mishahara haraka au vinginevyo wahame na kutafuta maslahi bora sehemu nyingine.

Madaktari bingwa Visiwani hapa, hulipwa kati ya sh.150,000 kwa mwezi, kiwango ambacho kinalalamikiwa na wataalamu hao kulinganisha na wenzao wanavyopata Bara.
 
Naomba kuuliza hivi, kwani waheshimiwa wawakilishi na wabunge wetu wanalipwaje kwa mwezi?

Unaulizia kwa mwezi? Uliza kwanza posho ya kikao kwa siku, utakapogundua ni sawa na huo mshahara wa mwezi wa huyo daktari wa Zanzibar usishangae! Hata mshahara ukiwa mdogo hapo hakuna mbunge atakayeulalamikia! Ukweli ni kuwa wafanyakazi wengi wa serikali huwa wana mishahara midogo, lakini wale wenye nafasi wanaridhika kutokana na hizo wanazoita "posho". Nilipokuwa mwalimu huko nilikuwa nashangaa sana, nilikuwa nalipwa kwa mwezi mshahara ambao nikiitwa semina Dar ya siku 3 tu nalipwa posho ambayo ni sawa na mshahara wa mwezi! Maana yake ni kwamba mshahara ulikuwa mdogo sana, kwani hata hiyo posho ya siku 3 nikijibana sana na kukaa kwenye hoteli "choka mbaya" nilikuwa nasevu pungufu kidogo ya nusu! Yaani ni kwamba nikiondoka mwenyewe na mshahara wangu wa mwezi kwenda kupumzika kwenye hoteli iliyochoka ya huko Sinza, huo mshahara ungenitosha (kula na kulala) siku 4 tu! Kwenye hoteli ya kati katikati ya Jiji(sio ya kitalii), ungenitosha siku 2, na kwenye zile hoteli za beach kule Bagamoyo (vile vyumba vya bei ya chini kabisa) mshahara wangu wa mwezi ungetosha tu bed and breakfast kwa usiku mmoja tu! Sasa ulipaji wa hivyo kwa kweli ni masikhara kabisa! Wale wenzangu waliokuwa walimu wenye bidii sana na ufundishaji ambao hawakuwa na mradi wowote nyumbani, muda wote wako na wanafunzi, kumalizia syllabus, kupanga lesson plans nzuri, wanatoa assignments na tests kibao (maana yake pia wana kazi nyingi za kusahihisha kazi za wanafunzi), walikuwa na matokeo mazuri sana ya mitihani ya kitaifa katika masomo yao, lakini wenyewe walikuwa "choka mbaya"! Walikuwa hawafundishi tuisheni (isipokuwa tu wakati wa likizo, tena kama wiki 2 tu maana muda mwingine waliutumia kusahihisha terminal exams kwa "makini"). Hawakuwa na "kitu" mfukoni, hata wanafunzi walikuwa wanawatania! Lakini majuzi (June) nilikwenda nyumbani nikawaona wawili, nilishangaa, wameacha kufundisha! Unajua wanafanya nini? Wameingia kwenye siasa za "chama cha walimu", wananiambia wameajiriwa huko, huyo mmoja alinipa lifti kwenye gari ya chama cha walimu akanipeleka hadi kijijini Muriet kuona ndugu na jamaa, kaniambia sasa hivi mambo "mswano", kwani naye anapata "posho" za vikao, na amejenga nyumba na kuanzisha mradi wa baa! Yule aliyekuwa bingwa wa hesabu kajiunga na idara ya takwimu naye mambo yake ni "bomba", ualimu ameacha. Yuko mmoja wanafunzi wa A level Biology walikuwa wanamwita "Vines", alikuwa "amemeza" yale mabuku makubwa mawili ya A'Level biology (nadhani ndio yanaitwa Vines), alikuwa anapendwa huyo! Alikuwa anaongea kwa sauti ndogo sana na hachapi mtu, lakini akiwa zamu, utashangaa wanafunzi wanavyomtii na kumsikiliza. Walikuwa wanadai yeye ndio "biology" yenyewe, maana alikuwa anaitoa neno kwa neno kinywani mwake bila kutumia kitabu wala notes, anaingia darasani na chaki tu, na soksi iliyochakaa ya kufutia ubao! Lakini naye alikuwa ameyumba sana kiuchumi, kila siku yuko na suruali yake ya khaki, shati la bluu na safari buti (vijana walikuwa wanaziita "mbwa"), na nadhani zilikuwa hazifuliwi, maana ni kila siku ziko mwilini. Lakini vijana walikuwa wanafaulu sana somo lake, na wako wengi ninaowafahamu ni madaktari. Sasa huyu nilikutana naye, nilimsahau kabisa! Amekuwa "sopsop", anang'ara, anaendesha "Range-Rover", nikamwambia "mwalimu naona sasa mambo yamekuwa matamu, kumbe mie naondoka na nyie ndio mambo yanawanyookea". Akacheka sana, kisha akaniambia ningepata utamu huu kwenye ualimu nisingeacha. "Kumbe umeacha?" nikamwuliza. Akajibu ameacha zamani, na amejiunga na shirika linalojihusisha na utafiti katika masuala ya wanyama pori, na ameajiriwa kwenye mradi ambao anasema akienda field porini kwa wiki 3 tu anapata malipo ambayo ni sawa na mshahara wake wa mwaka mzima alipokuwa mwalimu!

Kwa nini nimeyasema yote haya? Ni kwamba mfumo wa utawala uliopo unawakatisha tamaa wataalamu, na unawafanya wale wenye bidii na uaminifu kujuta kwa nini wanafanya kazi kwa kujituma, kwani haiwalipi! Matokeo yake ni kwamba wale walio wazuri wanakata tamaa na kuacha kazi na kutafuta njia nyingine au sehemu nyingine ambako utaalamu wao unaheshimika na kulipwa ipasavyo. Wale wanaobaki kazini wanaendeleza "usanii", wanakuwa "pretenders", kwa hiyo while the government pretends to pay, the employees pretend to work! Hakifanyiki kitu hapo! Na ninasema tatizo si la madaktari peke yao, ni kila mtu anayefanya kazi serikalini (isipokuwa wateule wachache wa huko BoT, TRA, PCB, TANROADS). Bahati mbaya kwetu ni kwamba madaktari "wametushika pabaya", wakigoma athari zinaonekana haraka na zinatisha, kwa hiyo wanasikilizwa haraka pia. Lakini wengine pia wana hali mbaya hivyohivyo!
 
Naomba kuuliza hivi, kwani waheshimiwa wawakilishi na wabunge wetu wanalipwaje kwa mwezi?

Kama sijakosea, Mh Zitto alipo simamishwa, wabunge wa upinzani walisema wataendeleea mchangia nusu malipo yake ambayo ni 1.5mil. kwa mwezi, kwani alikuwa akiendelea pata nusu malipo.

Kwa mtaji huu manake Mbunge analamba 3 mil. kwa mwezi. achilia mbali vikao, ambapo hupata 120,000 kwa siku.

Kwa nyongeza zaidi, wanapata pia kinua mgongo cha milioni 60 baada ya miaka mitano, bila kusahau, mkopo wa milioni 40 wa shangingi la ubunge, na kwa sasa kuna hii habari ya milioni 200 za mfuko wa jimbo, hizi sijajua zitakuwa ni kwa mwaka? ama kwa myaka yote mitano!
 
Yaani mwalimu Kithuku naisoma post yako kwa uchungu wa hali ya juu kutokana na ulivyo-relate personal experience very vividly kama movie vile.On the one hand nasikitika walimu wazuri wanaacha kufundisha kutokana na masuala ya maslahi, na upande mwingine, kama mfanyakazi mzuri anapoondoka kwa kupata "greener pastures" ninafurahi kwa mafanikio yao, everybody has to eat and pay bills.In a free market economy no matter how patriotic you are at the end of the day you have to look out for yourself because nobody else will.

At the end of the day anayeumia ni mwanafunzi ambaye atakuwa hapati walimu wenye uwezo/dedication.
 
Kwa nini nimeyasema yote haya? Ni kwamba mfumo wa utawala uliopo unawakatisha tamaa wataalamu, na unawafanya wale wenye bidii na uaminifu kujuta kwa nini wanafanya kazi kwa kujituma, kwani haiwalipi! Matokeo yake ni kwamba wale walio wazuri wanakata tamaa na kuacha kazi na kutafuta njia nyingine au sehemu nyingine ambako utaalamu wao unaheshimika na kulipwa ipasavyo. Wale wanaobaki kazini wanaendeleza "usanii", wanakuwa "pretenders", kwa hiyo while the government pretends to pay, the employees pretend to work! !

Kithuku,
Hakuna mbegu mbaya kama wafanyakzi waliokata tamaa- you can not talk of productivity- na Watz wengi wanafanya tu kazi za serikali bora liende tu- hii iko ktk sector zote- in the long run taifa linakosa mwelekeo!

Hata huko BoT sasa kama wewe unafanya kwa bidii na uliajiriwa based on merit halafu unashangaa analetwa mtoto wa mkubwa kwa kimemo na hana merit yoyote-na anapewa mshahara sawa au kukuzidi wewe- unadhani huyu moyo wa kazi bado utaendelea kuwepo? Let alone promotion za vichupi, safari za upendeleo, n.k yaani walioko serikalini wapo tu bora liende- wewe waalimu, madaktari, manesi, polisi n.k

I am trying to be a realist! The big problem- once a society loses morals and ethics ktk kazi- it is so difficult to restore good values (sanity) later- na ndoo inayotokea Tz kwa sasa. Nchi kama Nigeria baada ya haya mambo kukuwa sana- ndo maana Wanigeria wanaogopwa sana duniani kuwa ni matapeli- yalianza hivi kama hapa Tanzania!

The question is- who is responsible in the restoration of work ethics so as to improve productivity? Je hii tuwaachie tu wanasiasa? Any suggestions?
 
Mzalendohalisi unaingiza point muhimu sana.

Mara nyingi tunakuwa tukiwaweka mbele madaktari na wanasheria kwamba wao ndio watu muhimu kabisa lakini "ukweli" huu unaweza kuwa challenged.

Ukweli ni kwamba Tanzania kuna inequity kubwa katika mishahara kiasi cha kusikitisha.Wakati watu wengine mishahara yao ya mwezi ni sawa na bei ya lunch moja katika hoteli kubwa, wengine wanaongelea kupata "posho" maradufu ya mshahara huo kwa siku moja tu na mshahara ulio mnono isivyomithilika.

Ingekuwa afadhali kama mishahara midogo kabisa ingeweza kukidhi mahitaji ya msingi kabisa kama chakula, nishati, malazi na usafiri.Matokeo ya inequity hii ni kwamba hata katika pricing system vitu vinakuwa confused kwa sababu watu wanaweka bei ambazo wachache wanaweza ku-afford, hence driving prices up for the rest of the population and creating a vicious cycle of poverty kwa wanaolipwa mishahara ya chini.

Kuna haja ya ku-review system nzima ya mishahara.Lakini kitu cha maana zaidi ya ku-review mishahara kama anavyotaka kufanya Kikwete, ni kukuza uchumi ili kusudi mishahara yenyewe iweze kujisustain katika market system, na isiwe artificially enforced by the government.Kama Kikwete yuko serious anatakiwa kuianzia hii issue bottom up na wala siyo top down.

Tayari tumeona ni jinsi gani reforms za kima cha chini za maagizo ya serikali zinavyoanza kutishia unemployment kwa sababu employers wanadai hawawezi ku-afford kulipa mishahara mipya come January, which is only a week away!
 
Kuna haja ya ku-review system nzima ya mishahara. Lakini kitu cha maana zaidi ya ku-review mishahara kama anavyotaka kufanya Kikwete, ni kukuza uchumi ili kusudi mishahara yenyewe iweze kujisustain katika market system, na isiwe artificially enforced by the government.Kama Kikwete yuko serious anatakiwa kuianzia hii issue bottom up na wala siyo top down.

Tayari tumeona ni jinsi gani reforms za kima cha chini za maagizo ya serikali zinavyoanza kutishia unemployment kwa sababu employers wanadai hawawezi ku-afford kulipa mishahara mipya come January, which is only a week away!

Hii ni muhumu sana ndugu Pundit.

Labda katika suala la uchumi mkuu na wenzie huko waangalie pia suala la inflation, ili hata wanapo-review mishahara, ongezeko linalofanyika liweze kweli kuinua hali ya maisha. Nimeona practical example Zimbabwe, ambako uchumi umeyumba sana. Mwezi huu wametoa noti mpya ya ZD (Zim Dollar) 750,000. Hapo kabla noti kubwa kabisa ilikuwa ZD 100,000, ambayo nilipokwenda Zimbabwe 2005 ilikuwa inatosha kununua kilo moja ya sukari! Nilimtembelea "shemeji" yangu mmoja mzimbabwe (alikuwa "anamchukua" msichana mmoja wa kwetu tulipokuwa naye Chuo), akaniambia analipwa milioni 20 kwa mwezi. Nikampongeza sana kwa "umilionea", mbona alicheka! Wakati huo ilikuwa USD 1 kwa ZD 250,000, kwa hiyo mshahara wake wa milioni 20 ulikuwa sawa na USD 80 kwa mwezi! Ndipo mwishoni mwa 2006, Gavana wa benki kuu ya Zimbabwe akatangaza "mbinu" ya kupambana na inflation (wakati huo ilikuwa kama 1800%), kwa kufuta zero 3 kwenye currency ya Zimbabwe, akaanzisha new ZD, ambayo unarudisha benki ZD 100,000 unapewa ZD 100 (pia ili kupunguza bulkiness), hapo ikawa new ZD 250 kwa USD 1. Na mishahara ikarekebishwa kuendana na currency mpya. Leo hii wanabadilisha tena pesa, na USD 1 imefikia sawa na ZD 30,000 kwa kipindi cha mwaka 1 tu tangu ibadilishwe. Na inflation ni zaidi ya 4,500%. Sasa katika hali chaotic kama hii, sijui mtu anawezaje kufanya salary reforms.

Kwa hiyo ndugu Pundit nakubaliana nawe kuhusu kukuza uchumi na kuwa na self-sustaining system, lakini swali langu ama wasiwasi wangu ni: je mwelekeo wa kiuchumi wa serikali tuliyonayo waweza kutufikisha kwenye matumaini hayo? Tutasubiri hadi lini kuona hayo yakitokea? Hatua ipi ni feasible zaidi, kubadilisha serikali kwa matumaini kwamba mifumo itabadilika kuelekea kwenye uchumi sustainable zaidi, ama kujitahidi kuleta mabadiliko hayo ndani ya mfumo uliopo ? In other words, which is more feasible: fighting "them" or joining "them"? And either way, what are the chances of success?

Hayo ndio mashaka yangu.
 
Kwa hiyo ndugu Pundit nakubaliana nawe kuhusu kukuza uchumi na kuwa na self-sustaining system, lakini swali langu ama wasiwasi wangu ni: je mwelekeo wa kiuchumi wa serikali tuliyonayo waweza kutufikisha kwenye matumaini hayo? Tutasubiri hadi lini kuona hayo yakitokea? Hatua ipi ni feasible zaidi, kubadilisha serikali kwa matumaini kwamba mifumo itabadilika kuelekea kwenye uchumi sustainable zaidi, ama kujitahidi kuleta mabadiliko hayo ndani ya mfumo uliopo ? In other words, which is more feasible: fighting "them" or joining "them"? And either way, what are the chances of success?

You already know Kikwete and CCM are jokers who should not be entrusted to run a district let alone a country. we need a regime change, tatizo ni sasa with the bickering kama hizi za Wangwe na Zitto upinzani you seriously begin to wonder about the alternative tusije tukaleta the Chiluba effect hapa ikawa taabu juu ya taabu.

Lakini Kikwete has to go, especially kwa sababu hana excuse, amesomea uchumi, ana mandate ya watu na alikuja na gimmick ya "Ari Mpya,Nguvu Mpya" kumbe its is more like "old wine in new bottle" na "nguvu ya soda" if anything.
 
tatizo ni kwamba tunaishi katika taifa lisilojali na lisilothamini elimu na wataalamu.kama ni taifa linalojali lingekuwa tayari limejirekebisha.kwani tukiiangalia zanzibar(ambayo ndiyo kiini cha hii habari) tayari wataalamu wengi wameikimbia nchi kukimbilia ulaya magharibi na marekani kwa kutafuta mishahara yenye maslahi,huku nyuma wakiacha pengo ambalo hakuna wa kuliziba.lakini serikali haijaona hili kama ni tatizo hivyo mpaka leo inaonekana kwamba imeridhika na hali hii.matokeo yake watoto wasio na hatia wananyimwa elimu na wagonjwa mahututi wanafariki kwa maradhi ambayo yangetibika kutokana na uzembe mdogo tu wa serikali.kuthibitisha kwamba hawajali,ni juzi tu kulikuwa hakuna huduma ya xray katika hospitali ya mnazi mmoja kwa muda wa miezi 2 au 3, just kwasababu kuna kifaa kimeungua na nilipohabarishwa kifaa hicho kinagharimu shilingi milioni tatu za kitanzania nilibaki mdomo wazi. milioni tatu za kitanzania zichukue miezi.hili ndio taifa tunaloishi.tunaishi kwa nguvu za mola.damu zetu zimo mikononi mwa serikali zetu.tunawasubiri wasataafu waje kutuomba radhi.tushaizoea hii hali.
 
Kumekuwa na mgomo wa madaktari interns tangu alhamisi iliyopita baada ya kuona wanaendelea na manyanyaso yasiyi na mwisho na ahadi kedekede za maslahi bora za serikali ya JK. Leo tulisikia kwamba wauguzi na kada zingine zote zilizopo watajiunga na kuongeza nguvu. Kwa taarifa za vyombo vya habari ni kwamba serikali inasubiri ipelekewe taarifa rasmi sijui kwa njia gani?

Tujuavyo jinsi hii hopsitali ilivyo muhimu kwa watu maskini wa nchi hii napata woga wa kuona jinsi watu watakavyooza hapo mawodini na wazazi watakavyokufa. Jana kilikuwa na madaktari wawili tu pale wodi ya wazazi na wagonjwa zaidi ya 60 wakihitaji huduma zao ikiwemo ya upasuaji kwa walioshindwa kujifungua kwa njia ya kawaida. Mmoja akiwa theatre na mwingine wodini hali ilikuwa mbaya sana sijui leo

WanaJF tujadili hii hali, serikali iliahidi mishahara mipya kuanzia Jan 08 na ikatoa waraka unaoonyesha viwango vitakavyotumika na nyongeza. Ikaahidi mshahara mpya kuanzia July 08 ikiwa ni pamoja na malimbikizo ya miezi yote. Ilitegemewa Aug 08 mshahara mpya na malimbikizo yatoke lakini badala yake wakataka kutoa wa zamani, kukawa na fununu za mgomo. Ikatangazwa mshahara utachelewa hadi Aug 06 ili utoke mpya na malimbikizo majuzi wakatoa wa zamani kinyemela kupitia benki. Mara mkubwa mmoja akasema mshahara mpya utatolewa na hakuna malimbikizo kwa walio na mshahara wa zaidi ya Tsh 100,000/= (kima cha chini afya ni 135,000/=) hapo ndo moto ukaanzia na mgomo ukaanza hadi leo.

Aliye na taarifa na hali ilivyo leo atuhabarishe tujue huu usanii utaendelea hadi lini na watu wanaoumia ni maskini??? Wao wanatibiwa mafua tu India (Kumbuka Makamba alienda kucheck malaria India) na wana msacrifice Dr Masau ili mradi huu uendelee.

Serikali haina pesa za kulipa staff wake kwa vile wafadhili wamegoma hadi mafisadi wa EPA washughulikiwe???? Kwa nini JK haoni hata kidogo?? Nchi inaendeshwa kaw nguvu za giza?? Nani aliyepora uongozi wa nchi hii mamalaka jamani hata viongozi wawe vipofu hivi hata pua zishindwe kunuza wala ngozi zisifeel mabadiliko yoyote????

Nawakilisha pamoja na waraka wa nyongeza!!!
 
Na bila aibu waziri anasema eti hao madaktari hawana uzalendo. Inashangaza when it comes to people demanding what is rightfully theirs they arevtold they are not wazalendo na hao mawaziri na ufisadi wote wanaofanya mbona uzalendo wao wanausahau.
 
Nafikiri matatizo tunajitakia wenyewe tunapowachagua CCM AKWA 80 %. Wote tunajua kuwa CCM na Mafisadi wake hawako kwa ajili ya maslahi ya wananchi lakini wakitupa Tshirts, kofia na ubwabwa kwenye kampeni tunawachagua.
 
Nafikiri matatizo tunajitakia wenyewe tunapowachagua CCM AKWA 80 %. Wote tunajua kuwa CCM na Mafisadi wake hawako kwa ajili ya maslahi ya wananchi lakini wakitupa Tshirts, kofia na ubwabwa kwenye kampeni tunawachagua.

Mkuu Zero:

Wananchi hawawachagui CCM kwa 80%, bali CCM na Tume yao ya Uchaguzi ndio wanapanga wajipe ushindi kwa percentage ngapi. Kwa aibu ili kuona kuwa Popularity ya CCM imeshuka kutokana na ufisadi 2010 watajipa 73%. Hapa suala ni kufuata mkondo wa Kenya na kupigania tume Huru na kubadilisha katiba ambayo inazuia kuhoji ushindi wa Rais mahakamani pindi tume ikimtangaza. Vinginevyo hata wote tuwanyime kura CCM watajipa ushindi tu, tena wa kishindo na ndio maana hawana wasiwasi hata mkiwaita mafisadi. KUNA WATU WANAFANYA RESEARCH YA KUIBA KURA 2010, NA KUWATULIZA WADANGANYIKA WASIJE JUU.
 
Na bila aibu waziri anasema eti hao madaktari hawana uzalendo. Inashangaza when it comes to people demanding what is rightfully theirs they arevtold they are not wazalendo na hao mawaziri na ufisadi wote wanaofanya mbona uzalendo wao wanausahau.

Kweli kabisa lazima upande wa pili wa shilingi uangaliwe.
Linapofika suala la kugoma eti madaktari hawana uzalendo na ndo wakosaji tu wala wizara haihusiki.Huyo waziri anafanya kitu gani?Wamewahaidi ma dr kuwatimizia mahitaji yao ambayo hayajatekelezwa lakini serikali haisemi chochote.

Hii migomo mpaka lini? juzi juzi walimu nao wameibipu serikali..

Leo madaktari muhimbili.............nyongeza haipo maana hawaioni.

Kesho JWTZ,magereza na polisi wataandamana...............hawana nauli za kulipia daladala baada ya tamko la SUMATRA

Keshokutwa wasomi vyuo vikuu nao watakuwa barabarani..................Ada ya kozi zao imeongezeka

Mtondogoo ma albino nao waandamane..................maana maisha yao yanakatishwa na hawaoni kama wamepewa kinga na serikali.

Endless lists.......................

Wake up GOVT
 
Na bila aibu waziri anasema eti hao madaktari hawana uzalendo. Inashangaza when it comes to people demanding what is rightfully theirs they arevtold they are not wazalendo na hao mawaziri na ufisadi wote wanaofanya mbona uzalendo wao wanausahau.

Hawa mawaziri wetu nao si watu tu wa mtandao wao wa kifisadi! Mzalendo ni yupi kati ya yule anayeamua kubaki nchini na kuacha kwenda nje ya nchi ambako atalipwa vizuri na anahitajika sana! wanashau kwamaba hata wao wanahitaji huduma mbazo hazitolewi free!

Uzalendo sio ATM au credit card itakayokupa chakula cha kila siku na watoto wakasoma huku wakipata huduma za kimsingi
 
Kwa ujumla viongozi wet ambao ndio hao wana-CCM wamepoteza muelekeo na hata maamuzi mengi yanayofanywa unaweza kushangaa kama huyu mtu aliyafanya akiwa na akili timamu au alikuwa ameweka kinywaji kidogo. Suala la kudai kuwa hao wauguzi na madaktari kugoma kuwa sio uzalendo lilitakiwa kuzungumzwa endapo tu yale waliyoahidi serikali wametekeleza then watu wakagoma. Udaktari na unesi ni kazi kama kazi nyingine kama ofisa wa TRA, NSSF, BOT au wizara ya fedha ambaye anapata nyongeza anayostahili kwa wakati. Mtu anayeangalia uhai wa binadamu unamfanya kama mbeba mizigo kariakoo kuwa kesho nitakuongezea malipo na unamtaka aendelee kufanya kazi si jambo jema hata kidogo.

Hawa ni watu wenye mahitaji yote ya kibinadamu wanahitaji kula, kuvaa, kutibiwa na kuhudumia familia zao kutokana na kipato kitokanacho na kazi zao. Hizi propaganda kuwa Udakatri na unesi ni kazi za wito kwa hiyo wafanye kazi tu hata kama mazingira hayako in favour si sahihi.

Lakini kwa kuwa viongozi wetu wamekuwa ni watu wa kuingiza siasa hata pasipostahili ndio hupelekea hii migogoro ambayo mwisho wa siku anayeathirika ni mgonjwa. Wakati ufisadi umeshamiri watu wanaibia serikali mabilioni ya fedha na hawachukuliwi hatua zozote wakati hizo pesa zingeweza kabisa kuboresha huduma za kijamii na marupurupu ya watumishi kusingekuwa na migomo.

Jamani hii serikalli imepatwa na ugonjwa gani kwa kweli mambo yanayotokea sasa huenda ikatufikisha mahali pabaya ni vema serikali iamke na kuyafanyia kazi madai ya watumishi. Kila siku ni malalamiko mara walimu, madaktari, wastaafu wa EAC hakuna jema ni tabu tupu...Tutafika kweli????

Prof. Mwakyusa acha siasa fanyia kazi madai ya hao watumishi wagonjwa watakaopoteza maisha kwa kukosa huduma utakuwa msalaba wako... Sijawahi kusikia mawaziri wametishia kugoma sijui wao ni waadilifu sana au kulikoni?

Endeleeni kugoma mpaka kieleweke kama wanadhani ni kazi rahisi waende wao kuhudumia wagonjwa...
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom