BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,831
- 287,782
WATUMISHI wa sekta ya afya wataka mshahara wa madaktari kuwa Sh 2milioni
Na Nora Damian
WATUMISHI wa sekta ya afya nchini wamependekeza kima cha chini cha mshahara kuwa Sh500,000 na cha juu kuwa Sh2,500,000 kwa kada ya udaktari wakati wauguzi wametaka kuwa kati ya Sh400,000 na Sh800,000 kwa mwezi.
Hayo yalisemwa jana jijini na Mkurugenzi wa Umoja wa Vyama vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karsan baada ya umoja huo kufanya uchunguzi wa kihabari na watumishi hao kupendekeza kiasi hicho.
Karsan alisema uchunguzi huo, ulifanyika Oktoba mwaka jana hadi Januari mwaka huu na watumishi hao kupendekeza kuwa walipwe kiasi hicho kwa kuwa maisha ni magumu na hivyo wanataka walipwe kiasi hicho.
Mkurugenzi huyo alisema, jumla ya wafanyakazi 230 wa sekta hiyo katika mikoa husika walihojiwa na kusema kuwa kutokana na gharama za maisha kupanda, wanalazimika kutumia asilimia 60 ya muda wao kufanya kazi katika hospitali binafsi, biashara, kilimo na kulisha mifugo ili kukabiliana na hali hiyo.
Alisema wafanyakazi walioajiriwa na serikali au na taasisi binafsi walilalamika kulipwa mishahara midogo na kwamba asilimia 70 kwa nyakati tofauti, walisema hawalipwi marupurupu yoyote kama vile posho ya usafiri, malipo ya ziada, posho ya mazingira magumu na posho ya matibabu.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo, wafanyakazi walioajiriwa walilalamika kuwa hawapati nafasi za masomo ya kujiendeleza bila kutoa rushwa ya ngono kwa wanawake na kutoa fedha kama rushwa.
Katika uchunguzi huo pia, asilimia 90 ya wafanyakazi waliohojiwa walisema kuwa hawapewi nyumba na waajiri wao wakati wafanyakazi wa Zahanati ya Endasaki wilayani Babati, walisema wanalazimika kulala kazini kutokana na hofu ya kuliwa na simba wanapokuwa zamu za usiku.
Uchunguzi huo, ulifanywa katika mikoa ya Mtwara, Kigoma, Shinyanga, Ruvuma, Manyara, Rukwa, Arusha na Dodoma.