Mishahara sekta binafsi: TUCTA yashtukia danganya toto ya serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mishahara sekta binafsi: TUCTA yashtukia danganya toto ya serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Apr 21, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  SERIKALI, ambayo inahaha kujaribu kuzuia mgomo wa wafanyakazi uliopangwa kufanyika kuanzia Mei 5, imetangaza nyongeza ya asilimia 100 ya mishahara ya kima cha chini kwa wafanyakazi wa sekta binafsi na kuahidi kutangaza mishahara ya watumishi wa umma kabla ya Mei mosi mwaka huu.

  Lakini Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) limesema hatua hiyo haitabadili
  msimamo wake kwa sababu inahisi ni ya kisiasa hivyo hawatatangaza kusitisha mgomo wao hadi madai yao yote yatekapotekelezwa.

  Madai yaliyoifanya Tucta itangaze mgomo huo ni pamoja na nyongeza ya kima cha chini cha mishahara kwa watumishi wa umma hadi kufikia Sh315,000, kupanua wigo wa kodi ili kumpunguzia mfanyakazi mzigo wa kulipa kodi na makato kwa ajili ya mifuko ya hifadhi za jamii.

  Lakini jana, serikali iliamua kuweka kwanza kiporo madai hayo ya Tucta na kutangaza nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa sekta binafsi.

  Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya jana aliwaambia
  waandishi wa habari kuwa ongezeko hilo la mishahara ya wafanyakazi wa sekta binafsi, liwanagusa wafanyakazi wote katika sekta hiyo.

  Kwa tamko hilo la serikali lililotolewa kwa mamlaka aliyonayo waziri mwenye dhamana kifungu namba 41 (1) cha sheria ya ajira namba 7 ya mwaka 2004, mishahara ya watumishi wote wa sekta binafsi iliyotangazwa Oktoba 8 mwaka 2007 na aliyekuwa Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana John Chiligati, sasa italipwa mara mbili.

  Chiligati alitangaza viwango hivyo vya mishahara ambavyo vilianza kutumika Novemba
  mwaka 2007 baada ya mvutano mkali kati yake na Tucta.

  Viwango vya zamani vya kima cha chini kisekta pamoja na viwango vipya sasa vimetangazwa vitumike ni kutoka Sh65,000 hadi Sh130,000) kwa sekta ya kilimo, meli za mizigo na za abiria (Sh225,000 hadi Sh450,000), meli za uvuvi za ndani (Sh196,000 hadi Sh392000), makuli na wajenzi wa meli (Sh300,000 hadi Sh600,000).

  Wafanyakazi wa majumbani wapo katika makundi matatu; wanaofanya kazi kwa mabalozi
  (Sh90,000 hadi Sh180,000),wanaowafanyia maofisa wanaolipiwa huduma hiyo na waajiri wao (Sh 80,000 hadi Sh160,000) na wengine (Sh65,000 hadi 130,000).

  Wanaofanya kazi mahotelini (Sh150,000 hadi Sh300,000), hoteli za kitalii na hoteli za kati (Sh100,000 (200,000) na hoteli ndogondogo, baa, nyumba za wageni na migahawa (Sh80,000 hadi Sh160,000).

  Katika sekta ya madini, upande wa migodi mikubwa, wafanyakazi wanalipwa Sh350,000 na hivyo watatakiwa kulipwa Sh700,000, lakini waajiri wanaoshughulika na machimbo ya chumvi au chokaa waliwekwa kwenye kundi la viwanda vidogo kwa kuwa uwezo wao ni mdogo.

  Viwanda vidogo itakuwa kutoka Sh80,000 hadi 160,000, ulinzi binafsi, kampuni za
  kigeni (Sh105,000 hadi Sh210,000) na kampuni nyingine (S 80,000 hadi Sh160,000), sekta ya biashara na viwanda inayojumuisha mabenki, kima cha chini kilikuwa Sh150,000 na sasa kitatakiwa kiwe Sh300,000.

  Sekta ya afya imegawanywa katika makundi mawili yanayohusisha hospitali kubwa na maduka ambayo mshahara wake wa kima cha chini ni Sh120,000 na sasa itakuwa Sh240,000) na hospitali ndogo na zahanati (Sh80,000 hadi Sh160,000).

  Wafanyakazi wa huduma za anga mshahara wa kima cha chini ulikuwa Sh350,000 na sasa utakuwa Sh700,000, wasafirishaji wa mizigo (clearing and forwarding) ilikuwa Sh230,000 na sasa itakuwa Sh460,000), mawasiliano ya simu Sh 300,000 (600,000), usafiri wa nchi kavu (makondakta na madereva) sh 200,000 (400,000).

  Wafanyakazi katika vyombo vya habari wamegawanywa katika makundi mawili. Katika kundi linalohusisha vyombo vinavyojiendesha kibiashara, mshahara wa kima cha chini utabadilika kutoka Sh 250,000 hadi Sh500,000.

  Vyombo vingine ni vile visivyojiendesha kibishara kama vile vinavyorusha matangazo ya kidini, ambavyo kima cha chini kilikuwa ni Sh150,000 na sasa kitakuwa Sh300,000.

  Wakati serikali ikitangaza viwango hivyo vya kima chini cha mshahara mwaka 2007,
  iliweka wazi kwamba mwajiri haruhusiwi kulipa chini ya kiwango lakini anaweza kukiongeza kwa kadri anavyopenda ili kuboresha hali za wafanyakazi wao.

  Hata hivyo, viwango hivyo vilizua mtafaruku kwa waajiri wengi wakidai wakivitekeleza watafilisika kutokana na biashara kuwa ngumu na hasa ikizingatiwa wakati huo gharama za mafuta zilipaa na kukawa na wasiwasi pia ya dunia kukumbwa na uhaba wa chakula.

  Kwa kujua yaliyotokea kwenye sekta binafsi baada ya kutangaza viwango vipya mwaka 2007, Profesa Kapuya aliwataka waajiri wajitahidi kuvitekeleza kama vilivyotangazwa na serikali ili kuepusha migogoro sehemu za kazi.

  Aliigeukia Tucta akisema ilitoa mapendekezo saba ya kuitaka serikali kuyatekeleza kwa ajili ya kuondoa mgogoro huo na yoye yametekelezwa.

  Alisema tayari serikali imeridhia mapendekezo hayo na kilichobaki ni kuendelea na taratibu za mazungumzo hayo ili kuendeleza mchakato huo ikiwa ni pamoja na kutangaza siku ya kuanza kutumika kwa viwango vipya vya mishahara.

  Kapuya alisema serikali pamoja na wawakilishi kutoka vyama vya wafanyakazi walikaa kwenye kikao cha utatu kilichoitishwa na Baraza la Upatanishi (Lesco), ili kujadili hoja hizo saba.

  Kuhusu wafanyakazi wa serikali, alisema wataongezewa mishahara hiyo baada ya
  kutolewa notisi kwenye gazeti la serikali hivi karibuni ili waweze kutangaza ongezeko hilo kabla ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi ambayo hufanyika Mei Mosi.

  “Tumemaliza tofauti zetu, hivi sasa tuko kwenye mchakato wa mwisho wa kumaliza mgogoro huu. Kutokana na hali hiyo wafanyakazi wa sekta binafsi watalipwa ongezeko la asilimia mia moja, wakati serikali itatangaza rasmi kuongezwa kwa mishahara hiyo kabla ya sherehe za Mei mosi. Hivyo basi tunaamini kuwa wafanyakazi wataendelea na shughuli zao kama kawaida,” alisema Profesa Kapuya.

  Kutokana na hali hiyo, alisema Aprili 27, mwaka huu watafanya kikao ambacho kitatoa majumuisho ya suala zima la mgogoro huo pamoja na hatua zilizofikiwa juu ya maamuzi yaliyobaki.

  Profesa Kapuya alisema ikiwa wafanyakazi wataaamua kuendelea na mgomo wakati muafaka wa matatizo yao umepatikana, utakuwa ni kukiuka sheria kwa sababu watakuwa wamevunja makubaliano waliyofikia kwa pamoja.

  Lakini hali haikuwa hivyo kwa upande wa Tucta. Naibu Katibu Mkuu Nicholaus Mgaya aliitisha mkutano na waandishi wa habari jana na kuwaeleza kuwa mgomo upo pale pale kama ulivyopangwa.

  Hata hivyo, Mgaya alisema makubalino yao na serikali ni kurudi kwenye meza ya majadiliano na sio kuzima mgomo.

  Mgaya alisema kutokana na hali hiyo wafanyakazi wataendelea kushikilia msimamo wa kugoma ikiwa serikali itashindwa kuyafanyia kazi malalamiko yao kabla ya sherehe za Mei mosi.

  “Tunachokitaka sisi ni kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanaongezwa mishahara yao,” alisema Mgaya.

  Aliongeza kutokana na hali hiyo wameitaka serikali iache siasa badala yake itatue matatizo hayo kwa kutumia busara na utalaamu.

  Alisema makubaliano hayo ni kurudi kwenye meza ya majadiliano wakati serikali inaendelea kurekebisha mishahara ya wafanyakazi.

  Source: Mwananchi
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kwa hapo naisifu sana TUCTA, msuli wao nadhani safari hii utasaidia!...Tunahitaji watu wa roho ngumu kama hao katika sekta nyingi, hasa za utendaji!
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hawana aibu!! Wanapendekeza peanuts huku wao wakiiba matrilioni bila kufuatiliwa. Harakati zao ni only kuput off the strike. Shikilia hapo hapo TUCTA -- the same thread.
   
 4. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  nahis huu msimamo utalowana siku c nyingi
   
 5. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  TUCTA bana serikali ya MAFISADI hasa waziri wa kazi asiyefanya kazi yeyote KAPUYA. mshahara uongezwe hata asilimia 150. wao wanakula sana huko juu sie akina kandambili twateseka
   
 6. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #6
  Apr 21, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  TUCTA kazeni buti mpaka kieleweke.
   
 7. R

  Rayase Member

  #7
  Apr 21, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Napenda serikali itapokuwa sikivu!
   
 8. Zemu

  Zemu JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Jeeeeeee, wapi mishahara ya sekta ya umma? wapi mafao ya uzeeni ya PPF? vipi kupunguza kodi kwenye mishahara ya watunmishi? Huu ni usaniii mtupu.Kapuya ajiuzuru na kura zote kwa CCJJJJJJJJJJJJJJJJJJJJJJJJJJJJJJJJJJJJJJJJ.
   
 9. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #9
  Apr 21, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  TUCTA NI VIDUME, KILA MWAKA INABIDI mkomae hivi hivi kwa ajili ya kusaidia wafanyakazi wawe na maisha ya kuridhisha jamani
   
 10. b

  bonvize Senior Member

  #10
  Apr 21, 2010
  Joined: Feb 4, 2010
  Messages: 126
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Bado nina hofu kam wataendelea na msimamo wao hao Tucta kwa kuwa wameshaanza kutenganishwa katika makundi ya waajiriwa katika sekta binafsi na waajiriwa katika serikali.Na wewe Kapuya kwa niaba ya serikari kwa nini uwaagize wenzako kufanya kile mnachoshinwa kufanya.
   
 11. HeartBreak

  HeartBreak JF-Expert Member

  #11
  Apr 21, 2010
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 346
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  tatizo ni hatuna wasomi wanaojua uchumi wetu ukoje!!!! ndio yote yanatokea.....siasa mbovu,shule mbovu,hatuna lolote la kujivunia,,,,,,nchi imeoza,inanuka migomo kila eneo....
   
 12. t

  tk JF-Expert Member

  #12
  Apr 21, 2010
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hivi ni jipi limebadilika mpaka Serikali ikatangaza hivyo. Kumbuka kuwa wakati Chiligati alipotangaza mishahara hiyo, makampuni na waajiri walishindwa kuilipa kutokana na mapato ya makapuni hayo kutoweza kumudu uongezeko kubwa kama hilo. Waajiri wote nao wakagoma. Sasa itakuwaje maana sioni kama kuna mabadiliko yeyote katika hali ya uchumi wa nchi kuwafanya waajiri wakubali maongezeko hayo. Kitachofuata sasa ni mgomo wa Waajiri.
   
 13. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #13
  Apr 21, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Serikali inataka kutufanya wajinga. Kodi katika mshahara wa mtu hutozwa na serikali bila ya kujali mfanyakazi ameajiriwa na nani, lakini serikali hiyo hiyo ina waajiriwa wake ambao inatakiwa iwalipe mshahara na kukata kodi pia. Kama ni hivyo basi, kwanini serikali hiyo hiyo isipandishe mishahara ya watumishi wake kwanza na kupunguza ukubwa wa kodi ndipo wawe na mazungumzo na waajiri wa sekta binafsi kuona kwa pamoja jinsi ya kupandisha mishahara kwenye sekta hii?
  Chama cha waajiri nao wakiamua kufanya mgomo na kufunga biashara zao, je serikali itaweza kuwapokea na kuwaajiri watakaokosa ajira? Serikali msikurupuke, mmekamatwa kubaya na TUCTA, sasa mnaelekea kwa Waajiri, na baadaye kwa waajiriwa! Poleni Octoba si mbali, CHADEMA na CCJ msicheze mbali!
   
 14. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #14
  Apr 21, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nami pia nina hofu kama hiyo. Migomo genuine iliyotikisa serikali ilikuwa wakati ule kabla ya uhuru, wakati wa serikali ya ukoloni. Nakumbuka mwaka 1959 kulitokea mgomo wa wafanyakazi wa reli (RAU) ulioongozwa na kiongozi machachari wa trade union Christopher Kasanga Tumbo. Huo mgomo ulikuwa 100 per cent na serikali ya ukoloni ilibidi walete madereva kutoka Kenya wazungu kuendesha treni.

  Tangu tupate uhuru hakuna mgomo wowote wa kutisha uliofanyika, labda ule wa mwaka 1993 wa walimu ulioongozwa na Peter Mashanga. Tatizo ni hawa viongozi wa wafanyakazi -- hawana misimamo -- wanayumbishwa sana na serikali na waajiri wengine wakuu. Katika miaka ya 1990 huyo Kasanga Tumbo aliwahi, kabla hajafa, ktamka kwamba hawa viongozi wakuu wa wafanyakazi wa sasa wanaokaa katika ofisi zilizo juu ya magorofa hawawezi kugomesha chochote.

  Alisema yeye, wakati wa mgomo ule wa 1959, kama Katibu Mkuu wa RAU alisafiri kutoka stesheni moja ya gari moshi hadi nyingine akiwashawishi wafanya kazi wagome. Alisema alikuwa analala kwenye mabaraza ya stesheni wakati akifanya hivyo.
   
 15. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #15
  Apr 21, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Usaniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii yaani tushakuwa kama wakenya
   
 16. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #16
  Apr 21, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Nao hao TUCTA ni propaganda tu ili muwaone wako ngangari, lakini ikifika karibu na tarehe 5, mtawaona eti wanajifanya kukaa meza moja na serikali na mgomo kuupa kisogo. Hizi propaganda nachoka kabisa
   
 17. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #17
  Apr 22, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Mi nadhani kinachotakiwa ni uelewa wa Wziri. Yeye ange tangaza kima cha chini kwa Serikali, aachie sekita binafsi zipange mishahara yake kutokana na ufanisi kazini. hili ni swala la kitaalam. Huwezi kupanga mshahara wa kampuni fulani wakati hujui gharama za uzalishaji wa kampuni husika. lazima kuwepo na hesabu zinazo onesha uwezo wa uzalishaji, then mapato( If the Coy is able to break -even point).
  Kwa vyovyote vile kampuni zikilazimishwa kuongeza gharama za mishahara bila kuangalia hili (cost of production), zitakufa. Nadhani tupunguze ushabiki tuongelee facts.
   
 18. bona

  bona JF-Expert Member

  #18
  Apr 22, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  kinachoumiza sekta binafsi si viwango hasa, kinachoumiza ni pay as you earn! icho tucta washike kamba!
   
Loading...