Mishahara na posho za wabunge zina maswali mengi

Dig the EA

JF-Expert Member
Dec 7, 2017
277
270
Katika hali ya kawaida na katika nchi zetu za Kiafrika, hivi kuna sababu gani za kimantiki za wabunge kulipwa mishahara, posho, pension na stahiki nyingine kubwa kuliko maeneo mengine?

Imekuwa ikisemekana na kusikika kuwa wabunge wanalipwa almost 11m kwa mwezi ikiwa ni mishahara na posho kadha wa kadha.

Lkn cha kushangaza, wanapoenda kustaafu, inasemekana pia wanalipwa pension zao kiasi kikadiriwacho kuwa 200 million wakati wametumika kwa kipindi cha miaka mitano (5) tu.

Katika mazingira yetu na maisha ya Kitanzania, ni hela nyingi sana.
Swali, ni kazi gani hasa kubwa wanazofanya wabunge mpaka hizo kazi zitafsiri malipo makubwa hivi ?

Idara au taasisi nyingine za kiutumishi kama Elimu, afya, kilimo, nk hulipwa ujira mdogo sana.

Katika idara hizi kuna mtumishi aweza kulipwa laki 3 tu kwa mwezi, lkn mbunge, hiyo laki tatu hulipwa tu kama posho ya siku akiwa kwenye vikao bungeni.

Kazi ya mwalimu au nurse ni ngumu sana lkn ndo malipo kidogo. Je mbunge ana ugumu gani wa kazi hadi alipwe kiasi kikubwa?

NB: Kiwango cha mishahara na posho kwa hawa watu kipungue, viwango vya mishahara ya watumishi wa chini viongezwe. Hatua hiyo ikichukuliwa, watu hawatao kimbilia ubunge.

Wataenda kwa dhamira ya kuwasaidia wananchi, wa miaka ya nyuma tuliowashuhudia, wengi hufuata kipato cha ubunge.

Lakini kwa nini ilionekana inafaa kuwalipa wabunge hela nyingi?
 
Utachelewa sana kiongozi. .
Piga tarumbeta jiongeze. ... dunia nzima mambo ndivo yalivo
 
Kwa kifupi bunge la Tanzania halifanyi kazi yoyote ya maani, kazi yao kubwa na kupitisha mpiango ya serikali ili kuipa uhalali kuwa imepitishwa na wawakilishi wa wananchi.

Wabunge hua wanalipwa fedha nyingi na pia sheria nyingi kandamizi hua zinaandikwa na serikali zikiwa haziwaathiri wabunge kama njia ya kuwafurahisha na kuhakikisha hawaisumbui serikali.

Kazi yao kubwa hususani wale wa chama tawala (hata CDM ikishika dola kesho watakua hivyohivyo) ni kuishangilia serikali, kupigapiga meza, kununua makahaba Dodoma n.k
 
Kwa kifupi bunge la Tanzania halifanyi kazi yoyote ya maani, kazi yao kubwa na kupitisha mpiango ya serikali ili kuipa uhalali kuwa imepitishwa na wawakilishi wa wananchi.

Wabunge hua wanalipwa fedha nyingi na pia sheria nyingi kandamizi hua zinaandikwa na serikali zikiwa haziwaathiri wabunge kama njia ya kuwafurahisha na kuhakikisha hawaisumbui serikali.

Kazi yao kubwa hususani wale wa chama tawala (hata CDM ikishika dola kesho watakua hivyohivyo) ni kuishangilia serikali, kupigapiga meza, kununua makahaba Dodoma n.k
Malipo ya wabunge nchini ni makubwa mno kulinganisha kazi zao za kupitisha miswada ya hovyo. Hawajawahi kukataa kupitisha sheria hata ni mbaya kiasi gani. Kiukweli sijui ni kwa nn wananchi wanawachagua.
Baadala ya kuwawakilisha wananchi vizuri, wanawakili maslahi ya serikali. Tafsiri yangu ya malipo manono ni rushwa ya kisiasa. Hii rushwa ndiyo chanzo cha kuwania ubunge. Pia watia nia na wagombea wako tayari kufanyia wenzao kila aina ya hila majina yao yapite na wachaguliwe.
Njia sahihi ya kisayansi ya kukabiliana na tatizo hili ni kuwapunguzia malipo kwa angalau 50%.
 
Mbona dawa ni ndogo sana,

1.Kila mtu aliyewahi kuwa mbunge kutokea1995 wakatwe 50% ya mapato yote yaani mshahara+ Posho+ Pension.
2.Wabunge kutokea 2020 November walipwe posho ya kikao tu bila mshahara, pammoja na sh million 50 pension kila kumaliza ubunge.
3.Ubunge kutokea 2020 November ni ruksa kuwa mbunge kwa miaka 15 tu,hakuna kuongeza.
 
Nimesikia kulikuwa na Bunge la viwango lililoendeshwa na marehemu Sita, nadhani nilikuwa darasa la 1.

Bunge hili liliweza kufanya nini kama bunge? Kumshawishi waziri mkuu kujiuzulu?

Kuna rekodi yoyote inayoonesha ni jinsi gani bunge lilifanikiwa kuikatalia serikali jambo lolote kwa maslahi mapana ya taifa?

Nakumbuka bunge lilipitisha miswaada ya sheria za gesi usiku kwa usiku, na siku kadhaa mbele, raisi ambaye wakati huo wa kupitishwa miswaada hiyo alikuwa mbunge na waziri, akatuambia anashughulikia ile Hydro kwakuwa gesi ile iliuzwa, sio yetu ni ya mabwana wakubwa.

Mabunge ya nchi za Africa, kazi yao ni nini hasa? Kusema NDIO au HAPANA?
 
Wapunguze wawaongezee kada ya ualimu na afya
ni kada iliyosahaulika huku kazi zao zikiwa ngumu
 
Back
Top Bottom