Mishahara mipya: Kasungura kadogo, kwanini tusigawane sawa?

Miwatamu

JF-Expert Member
Oct 2, 2012
1,450
487
Tangu habari za mabadiliko ya mishahara kwa wafanyakazi wa serikalini na mashirika ya umma hapa nchini ziwekwe hadharani, nimekuwa nikijiuliza maswali mengi ambayo kwayo nashindwa kuyapatia majibu. Inakuwaje leo mtumishi wa ngazi ya juu ambaye anapewa;
shangingi bure,
anaishi nyumba ya bure,
Umeme bure
analipiwa gharama za simu,
Chai ofisini ni bure........ Inakuwaje mtu huyu ndiye huyohuyo apate nyongeza ya zaidi ya shilingi millioni moja wakati mimi ninaye panda daladala 4-6 kwa siku
Nalipia kodi ya nyumba
Ada ya watoto wa shule
Bill ya umeme
Maji ndoo moja shilingi 500........ Lakini nimeambulia nyongeza ya shilingi 35,000 tu! Sasa nauliza kama Kasungura ni kadogo kwa nini tusigawane sawa?
Tutafakali pamoja.
 
umenena vyema mkuu! watumie njia mbadala, badala ya kutumia % ya mshahara.
 
Ni ujinga kutegemea mshahara kwa 100%. Weka na miradi.

Labda uwe mwizi wa muda wa muajiri ndipo utakapoweza kufanya mradi kwa 100%. na hii ya kutofanya kazi is killing Tanzania.

Angalia wanaofanya kazi kwenye makampuni na NGO uone kama wanapata muda wa kufanya hiyo miradi kwani hata akilala anawaza jinsi gani ataachieve malengo au kumeet deadlines.
 
  • Thanks
Reactions: Ame

Kaunga umeongea ukweli, yawezekana huyu ndugu yetu hajui ajira za siku hizi kuwa ni za mikataba kwa maana ya ku-achieve targets.
 
Ni ujinga kutegemea mshahara kwa 100%. Weka na miradi.

Hii ya miradi ndo inayosababisha nchi hii isisonge mbele watu wanafanya vizuri kwenye miradi yao na kuacha kazi za serikari matokeo hakuna ufanisi wowote.Angalia walimu wa serikari sasa wanafanya biashara zao hawana muda wa kufundisha. Ni kweli kama sungura ni mdogo aje mzima mezani tugawane sawa lakini anakuja mezani baadhi ya sehemu hazipo huu ni wizi.
 
mbavuu kabisa hao, kuongeza mishahara huku lipesa limedoloala.... haina maana , Kama unaniongezea mshahara huku makodi yana panda, gharama ya maisha juuuuu inamaana gani...? mbavu kabisaa hao
 
Miwatamu kama huna mpango wa kujiajiri kipindi kifupi kijaco basi andaa mpango mkakati wa kukuwezesha upande cheo hadi kufikia hizo nafasi zenye nyongeza ya TShs. 1,000,000/= kama mpango wako wa kati na muda mrefu. Ukiwa na mpango huo, wanachofanyiwa waliojuu yako hakitakuumiza kwa kuwa nawe ndani ya kipindi kisichozidi miaka mitano utakuwa kundi hilo hilo
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli. Amenukuu vibaya msemo wa George Orwell kwenye Animal farm.
Sahihi ni:
"All animals are equal, but some animals are more equal"

Kwa hiyo na wewe Msendekwa unalinganisha binadamu (wafanyakazi wa serikali) na wanyama wa kufugwa?
 
Last edited by a moderator:
Labda uwe mwizi wa muda wa muajiri ndipo utakapoweza kufanya mradi kwa 100%. na hii ya kutofanya kazi is killing Tanzania.

Angalia wanaofanya kazi kwenye makampuni na NGO uone kama wanapata muda wa kufanya hiyo miradi kwani hata akilala anawaza jinsi gani ataachieve malengo au kumeet deadlines.

Hii attitude ya namna hii sijui inatoka kwa wtanzania wa aina gani....Hivi wanajua nini maana ya full time employment na part time employment? Je wanaelewa kweli what is divission of labour? Hata wakati wa ujima haya mambo yalikuwa rahisi kuonekana kwa mama na baba kugawana majukumu leo hii huu mchanyato wa mara kiongozi wa serikali kuuuza petrol, ooh mara ana supply tender...Wanataaluma badala ya kutumia taaluma yao mara utakuta anafuga kuku ng'ombe etc na hakuna effectiveness wala efficiency of resource (time atleast) kwa kila walifanyalo matokeo yake ni marginal returns kuwa negative na maendeleo kuwa retrogressive badala ya kuwa progressive....

Hizi siasa jamani tuziangalie sana zina sehemu yake lakini wanasiasa wasipotumia wataalamu katika kuwapa options za sera zenye tija ndiyo tutaendelea kufanya vitu kama wendawazimu huku sote tukigubikwa na relative poverty..
 
Labda uwe mwizi wa muda wa muajiri ndipo utakapoweza kufanya mradi kwa 100%. na hii ya kutofanya kazi is killing Tanzania.

Angalia wanaofanya kazi kwenye makampuni na NGO uone kama wanapata muda wa kufanya hiyo miradi kwani hata akilala anawaza jinsi gani ataachieve malengo au kumeet deadlines.

UMENIKUNA SANA KAUNGA
NAOMBA NIONGEZE..!
:biggrin1: :biggrin1:
 
Hilo ni jibu lisilo kidhi haja kabisa ,na kwa kweli sio jibu la swali.Kama ni swala la kuweka miradi basi bosi angekuwa kwenye a better position ya kuweka miradi.Why mlala hoi.Ni swali rahisi kwa jibu gumu.Watanzania upendo umekwisha,hatufikirii wengine kabisa,ni u-Freemason mtindo mmoja.Tunaishi zaidi kama wanyama kuliko kama wanadamu.Binafsi sijui hata wametumia vigezo gani kuongeza mishahara so much and so dispropotionately.Naona wamekurupuka tu.
Ni ujinga kutegemea mshahara kwa 100%. Weka na miradi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom