Mishahara midogo Madaktari Visiwani- hadi lini?

MzalendoHalisi

JF-Expert Member
Jun 24, 2007
4,643
1,550
Madaktari bingwa Visiwani hapa, hulipwa kati ya sh.150,000 kwa mwezi, kiwango ambacho kinalalamikiwa na wataalamu hao kulinganisha na wenzao wanavyopata Bara.

Source: Majira 21.12.2007

1. Nini kinafanya mishahara kuwa midogo hivi Visiwani? Kwa bara Daktari mpya toka intern hulipwa over 600,000 na 30% zaidi kama posho ya nyumba!

2. Yet unakuta wote mlisoma pamoja Muhimbili- na mnavyojua course za madaktari/wafanyakazi wa afya zilivyo ngumu. Mtanzania anayeajiriwa Bara anaanza na mshahara mzuri over 600,000 na posho na Mtanzania anayeajiriwa Visiwani anaambulia 150,000! Na wote wanaangalia na wanatibu afya za Watanzania! Je huu ni uungwana?

Wandugu mna mawazo gani?
 
Kama mshahara mdogo, si waondoke tu wakatafute sehemu zinazolipa zaidi.............haya mambo ya kubembelezana na serikali juu ya mishahara kwa kazi ngumu unayofanya yashapitwa na wakati. Waingie mitini, nchi kibao zinatafuta madaktari hasa kusini mwa afrika. Hapo kenya tu ukienda hukosi kazi tena kwa mshahara wa zaidi ya $$1200 kwa mwezi. Jamaaaaaaaaani eeenh, tupeni manyanga kana ka-mshahara kadogo!!. Its ok wakisema "uzalendo" umewashinda, kwani Tanzania ya leo kila mtu anaangalia maslahi yake na nduguze wa karibu....dawa ni kumkoma nyani bila aibu.
 
1. Wizara ya afya haiko kwenye muungano (kama nimekosea naomba kusahihishwa), hivyo kila upande una maamuzi yake na mipangilio yake, japokuwa vyuo vinavyotoa elimu hiyo ni hivyo hivyo.

2. Hata hao madaktari wa bongo hawakupata hiyo 600,00 kiulaini, walisota, wakastruggle na kusacrifice, hadi increment ya 100% kwa wafanyakazi wote wa afya.

3.Katika secta ya afya Dr. si peke yake anayeweza kukamilisha 'good therapeutic/patient outcome'. kuna wauguzi, watu wa maabara etc.

4. Angalia mishahara ya wauguzi, bado ni midogo ukilinganishwa na risk wanazokumbana nazo, 'na sina uhakika kama kuna risk insurance serikalini.' Ikatokea ukapata maambukizo ukiwa kazini, tutasema ulikuwa ni uzembe wako na endapo ukafa tutsema ilikuwa kazi ya mungu.

5.Ili na wao weweze kufaidika ni lazima wajitoe muhanga kudai haki yao. 'Punda mbebeshe mzigo hadi atakapolia'.

Kama wako kimya inamaana mshahara unatosha.
 
Kama mshahara mdogo, si waondoke tu wakatafute sehemu zinazolipa zaidi.............haya mambo ya kubembelezana na serikali juu ya mishahara kwa kazi ngumu unayofanya yashapitwa na wakati. Waingie mitini, nchi kibao zinatafuta madaktari hasa kusini mwa afrika. Hapo kenya tu ukienda hukosi kazi tena kwa mshahara wa zaidi ya $$1200 kwa mwezi. Jamaaaaaaaaani eeenh, tupeni manyanga kana ka-mshahara kadogo!!. Its ok wakisema "uzalendo" umewashinda, kwani Tanzania ya leo kila mtu anaangalia maslahi yake na nduguze wa karibu....dawa ni kumkoma nyani bila aibu.

si kuwa wakimbie madaktari zanzbar hakuna wote weshakimbia, kuna waliokimbilia botswana kuna walioko hapo bongo kuna walioamua waanzishe hospitali binafsi na wako wengine hukaa kwa sababu ya kuwa wana miraddi kama ya ukimwi na maaria na mengine.

kwa kweli zanzibar uchumi wake mdogo na pia viongozi hawatilii umuhimu juu ya wataalamu wao.

wenye kukimbia sio m adaktari tu na wafanyakazi wengine kama wanasheria wataalamu wa IT wa uchumi na mengineo.

hili serikali inalijua fika, lkn uchumi mdogo, pili juhudi za kuwathamini wasomi pia ni ndogo.

serikali imejikita zaidi kwenye siasa na sio mambo ya utaalam

hili pia ni suala ambalo serikali ya muungano haiwezi kulikwepa inatakiwa ijitahidi kuwa na master plan itayosaidia kustabalise mambo kule au itafika pahala zanzibar kutakuwa na wajinga watupu. maana sasa hata wanaosomea ualimu wakimaliza chuo kikuu wanaona tabu kurudi zanzibar kusomesha.

kwa nn? hili wakae waliangali ni vipi muungano utaweza kuwasaidia ndugu zao kiuchumi na kijamii hata kwa mambo yasio ya mungano na hasa hiyo nnavyoamini mie ndio kazi ya muungano
 
Nimepost pia habari kama hii, sikuona hint kuwa mwenzangu ameshaposti. Naomba moderator aiunganishe na hii.

Pia nakuombeni msome ombi langu nililoposti kwenye "Hoja Mchanganyiko"
 
Source: Majira 21.12.2007

1. Nini kinafanya mishahara kuwa midogo hivi Visiwani? Kwa bara Daktari mpya toka intern hulipwa over 600,000 na 30% zaidi kama posho ya nyumba!

2. Yet unakuta wote mlisoma pamoja Muhimbili- na mnavyojua course za madaktari/wafanyakazi wa afya zilivyo ngumu. Mtanzania anayeajiriwa Bara anaanza na mshahara mzuri over 600,000 na posho na Mtanzania anayeajiriwa Visiwani anaambulia 150,000! Na wote wanaangalia na wanatibu afya za Watanzania! Je huu ni uungwana?

Mkuu
heshima mbele
naomba ufafanuzi kidogo. Hiyo tzs 600,000 anayopokea daktari jnr nadhani ni gross salary bila makato. Unaweza ukatupa rough figure ambayo ni take home baada ya makato yote? kwani nahisi PAYE inawaumiza sana wafanyakazi wa umma.
 
si kuwa wakimbie madaktari zanzbar hakuna wote weshakimbia, kuna waliokimbilia botswana kuna walioko hapo bongo kuna walioamua waanzishe hospitali binafsi na wako wengine hukaa kwa sababu ya kuwa wana miraddi kama ya ukimwi na maaria na mengine.

kwa kweli zanzibar uchumi wake mdogo na pia viongozi hawatilii umuhimu juu ya wataalamu wao.

wenye kukimbia sio m adaktari tu na wafanyakazi wengine kama wanasheria wataalamu wa IT wa uchumi na mengineo.

hili serikali inalijua fika, lkn uchumi mdogo, pili juhudi za kuwathamini wasomi pia ni ndogo.

serikali imejikita zaidi kwenye siasa na sio mambo ya utaalam

hili pia ni suala ambalo serikali ya muungano haiwezi kulikwepa inatakiwa ijitahidi kuwa na master plan itayosaidia kustabalise mambo kule au itafika pahala zanzibar kutakuwa na wajinga watupu. maana sasa hata wanaosomea ualimu wakimaliza chuo kikuu wanaona tabu kurudi zanzibar kusomesha.
kwa nn? hili wakae waliangali ni vipi muungano utaweza kuwasaidia ndugu zao kiuchumi na kijamii hata kwa mambo yasio ya mungano na hasa hiyo nnavyoamini mie ndio kazi ya muungano

Muungano tena? Si hawa jamaa hawaishi kuingilia masuala ya Zanzibar wakisahau kuwa Zanzibar ni taifa? Leo unataka wawapangie Master Plan!
 
yeah ni muungano

ndugu yangu ukisha kuoa lle familia ya mkeo ni yako.

unayo haki ya kuwasaidia ukawaita mashem na kuwapa nyishauri mbali mbali ikiwezekana kuwawezesha kidogo na hapo ndipo watapojisikia kuwa dada yao kapata mume wa kuwafaa.

nnazani umenifahamu, sikusudii muungano ufanye hayo bila ya kuishirikisha SMZ washirikishwe na wakae kitako jinsi gani ya kuboresha hali kule, na hasa ukizingatia hali hiyo imeharibika wakati tuko pamoja
 
Mkuu Mtu wa Pwani,
Sasa kama familia ya mkeo haikutaki? Utaendelea kujipendekeza? Natumaini hauelekei kwenye kupendekeza mishahara ya madaktari iwe suala la Muungano? Iweje tuu kwenye matatizo ndipo Muungano uonekane una umuhimu? Nakumbuka wenzetu walivyong'aka kuhusu fununu za upatikanaji wa mafuta! Kama nakumbuka vizuri Muungano walionywa wasithubutu kuingiza kidole chao huko! Hili tatizo ni la serikali ya mapinduzi na wao ndiyo walitatue bila kuingiliwa na yeyote. Kama hii haiwezekani basi sekta ya Afya iingizwe katika masuala ya Muungano.
 
yeah ni muungano

ndugu yangu ukisha kuoa lle familia ya mkeo ni yako.

unayo haki ya kuwasaidia ukawaita mashem na kuwapa nyishauri mbali mbali ikiwezekana kuwawezesha kidogo na hapo ndipo watapojisikia kuwa dada yao kapata mume wa kuwafaa.

nnazani umenifahamu, sikusudii muungano ufanye hayo bila ya kuishirikisha SMZ washirikishwe na wakae kitako jinsi gani ya kuboresha hali kule, na hasa ukizingatia hali hiyo imeharibika wakati tuko pamoja

Tatizo ni wenzetu hawakawii kudai kuburuzwa. watakachokitaka ni serikali ya Muungano ichukue jukumu la kubeba bajeti ya Afya wakati wao waendelee kuiendesha bila kuingiliwa! Hili haliwezekani maana matatizo yatabaki palepale. Sasa ndugu yangu unataka kudai kuwa Muungano ndio umesababisha hali kuharibika?
 
mie sikubaliani na ww mbona mengi mnatuburuza?

OIC, kutuchagulia rais, uendeshaji uchaguzi na mengi mengineyo.

hapa ni kukaa na kuzungumza mkikaa na kuzungumza vizuri kuburuzana kutatokea wapi?

hivi mm na ww kama marafiki ukaniita au tukaamua kuelezana matatizo yetu na kusaidiana njia ya kutatua ni kuburuzana?

mie nijuavyo kuburuza ni kufanya jambo kwa kumuamulia mtu bila ya kumshauri na bila ya ridhaa yake liwe zuri au baya
 
Kama mshahara mdogo, si waondoke tu wakatafute sehemu zinazolipa zaidi.............haya mambo ya kubembelezana na serikali juu ya mishahara kwa kazi ngumu unayofanya yashapitwa na wakati. Waingie mitini, nchi kibao zinatafuta madaktari hasa kusini mwa afrika. Hapo kenya tu ukienda hukosi kazi tena kwa mshahara wa zaidi ya $$1200 kwa mwezi. Jamaaaaaaaaani eeenh, tupeni manyanga kana ka-mshahara kadogo!!. Its ok wakisema "uzalendo" umewashinda, kwani Tanzania ya leo kila mtu anaangalia maslahi yake na nduguze wa karibu....dawa ni kumkoma nyani bila aibu.

Umenifanya nicheke na kusikitika......wengi wa wasomi wetu hawajui pa kuanzia wengne hata Email ID hawana sasa dili la kupata job South ni kama kufanya biashara ya Kutoa ndizi Mwanza na kuzipeleka Bukoba
 
mie sikubaliani na ww mbona mengi mnatuburuza?

OIC, kutuchagulia rais, uendeshaji uchaguzi na mengi mengineyo.hapa ni kukaa na kuzungumza mkikaa na kuzungumza vizuri kuburuzana kutatokea wapi?

hivi mm na ww kama marafiki ukaniita au tukaamua kuelezana matatizo yetu na kusaidiana njia ya kutatua ni kuburuzana?

mie nijuavyo kuburuza ni kufanya jambo kwa kumuamulia mtu bila ya kumshauri na bila ya ridhaa yake liwe zuri au baya

Mbona hauzungumzii kuhusu kulipiwa deni la Tanesco? Kunyimwa haki ya kushiriki uchaguzi wale wenye asili ya bara? Hata wakati watu wabara walikuwa wanaingia Zanziba kwa pasi hapakuwa na malalamiko kutoka bara. Tunazungumzia mgao wa misaada lakini hatuzungumzii ulipaji wa deni la taifa?

Sasa kama sisi ni marafiki wa dhati utanisikiliza hata kama ninalolisema utaliona chungu! Tatizo ni pale mnapokaa pamoja mkafikia maamuzi ambayo baadae jamii ya upande mmoja inapoonekana kutokukubaliana nao wenzetu hamkawii kuruka na kudai kuwa mliburuzwa! Ukweli ni kuwa hauwezi kupata ridhaa ya jamii nzima ila ya wawakilishi wao tuu. Hapana, Mkuu, ukishaumwa na nyoka........Serikali ya Muungano ikijiingiza hili nalo litajumuisha na hayo ya OIC, uchaguzi n.k.
 
hili la kunyimwa kupiga kura wenye asili ya bara sio kweli, maana hata wawakilishi wetu na wabunge wetu baadhi yao wana asili ya bara.

kuna waliopiga kura na wala hawana sifa ya kupiga kura nnazani utakuwa mwelewa wa sheria za uchaguzi ni kipindi gani mtu wa bara anaweza kupiga kura zanzibar kwa kuwachagua rais wa zanzibar, wawakilishi, wabunge na madiwani. ila rais wa muungano hatuna mjadala anayo haki hiyo hili ni suala la kikatiba.

hata hivyo wako wengi wasio na sifa walipiga na kupewa vitambulisho wa uzanzibari yote haya nnakubali kuwa siasa tuliiweka mbele kuliko uhalisi wa mambo.

sasa kama hatuaminiani na mnasema mshaumwa na nyoka mnaogopa kutusaidia kuna haja gani ya kung'ang'aniana, tuacheni tujue kuwa tuko peke yetu kuliko kuhisi tuna wenzettu wasiotuamini wala kujali hali zetu
 
Manung'uniko all starz, sijui mtaacha lini katabia hako kabovu!!! thread ni kuhusu mishahara ya ma-MD, ghafla imeacha njia na kutumbukia korongoni(masuala ya muungano)...........Mchundo na Pwani, hamtafikia muafaka kuhusu suala la union....nyie rudini tu kwenye main feature ya thread hii, mnakaribishwa.!!
 
Hapana , Mkuu. Inabidi tukubaliane mipaka ya masuala ya Muungano na tuzingatie mipaka hiyo. Hii itaepusha hizi dhana za "kuburuzwa".
Kwani Muungano ni kwa ajili ya faida ya Zanziba peke yake? Tusisahau ni pande mbili zilizoungana na ni muhimu kuhakikisha maslahi ya pande zote mbili haziathiriki. Kubaki kutupia lawama upande mmoja kwa kila baya hakuashirii
mema kwa Muungano wetu.
 
nimekupata ndugu yangu tusonge mbele ss ndugu na mtu kutoa duku duku lake sio dhambi, hatutaki kujenga taifa la woga kama la nyerere tunataka taifa linalohoji na kujenga utashi wa kimawazo sio zidumu fikra na nnaamini yeye kachangia sana haya matatizo angemsikiliza Jumbe tusingefika hapa
 
1. In 60's and 70's wakati bei ya karafuu iko juu mishahara Visiwani ilikuwa bora kuliko Bara.

2. Mimi ningekuwa raisi wa Muungano ningefidia wafanyakazi wote wa Visiwani mishahara kuwa na wwiano sawa na Bara- kama hali ya Uchumi Visiwani ikiwa mbaya. Hali ya uchumi ikiwa nzuri basi ningesitisha.

3. Visiwani ni nchi ndiyo- ila ni ndogo- not equal in any way na Bara- ni Muungano kweli na tumedumu over 40 years! Swala la Muungano kufidia uchumi Visiwani hata ktk mishahara ni sawa- hii ipo sehemu nyingi tu duniani! Muungano hawawezi kujitoa eti Mishahara ya Madaktari sii swala la Muungano- halafu ndo hao madaktari wakimbilie Bara wote? sasa nini maana ya mantiki ya Muungano?

4. Mtu wa Pwani naafikiana na wewe- Muungano intervention ktk uchumi na mishahara Visiwani- is responsibility of Muungano- not favour- maanake Visiwani ni sehemu ya Muungano. Siyo responsibility ya Kenya- ni ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania!

Naamini haya yote Nahodha na Lowassa wnaweza kujadili!
 
Manung'uniko all starz, sijui mtaacha lini katabia hako kabovu!!! thread ni kuhusu mishahara ya ma-MD, ghafla imeacha njia na kutumbukia korongoni(masuala ya muungano)...........Mchundo na Pwani, hamtafikia muafaka kuhusu suala la union....nyie rudini tu kwenye main feature ya thread hii, mnakaribishwa.!!

Kumradhi Mkuu lakini mshahara huo unalinganishwa na ule wanaopata walio bara. Pwani alipendekeza serikali ya Muungano iingie kuisaidia SMZ na mimi sikukubaliana nae. Lakini Pwani alikuwa na hoja nzito ambayo haikwepeki kwenye hii mada nayo ni, nini wajibu serikali ya Muungano pale ambapo mambo yanaharibika upande mmoja? Kama sisi kweli ni ndugu tutamwangaliaje tuu mwenzetu anapoadhirika? Hawa maMD kwa kulinganisha mapato yao na wale wa bara wana hidden threat kwamba wataweza kukimbilia bara kwenye maslahi mazuri zaidi. Anauliza, ni nini wajibu wa serikali ya Muungano katika hili? Je, izuie madaktari kuhamia kutoka zanziba? Ipunguze mshahara wa madaktari wake ulingane na wale wa Zanziba? Isaidie SMZ kuwalipa maMD wake mshahara unaolingana na ule wanaowalipa wenzao wa bara? Yote haya yako mezani. Sasa tumetoka vipi kwenye mada mimi na rafiki yangu Mtu wa Pwani? Mkuu Pwani, nisahihishe kama nimekukosea.
 
1. In 60's and 70's wakati bei ya karafuu iko juu mishahara Visiwani ilikuwa bora kuliko Bara.

2. Mimi ningekuwa raisi wa Muungano ningefidia wafanyakazi wote wa Visiwani mishahara kuwa na wwiano sawa na Bara- kama hali ya Uchumi Visiwani ikiwa mbaya. Hali ya uchumi ikiwa nzuri basi ningesitisha.

3. Visiwani ni nchi ndiyo- ila ni ndogo- not equal in any way na Bara- ni Muungano kweli na tumedumu over 40 years! Swala la Muungano kufidia uchumi Visiwani hata ktk mishahara ni sawa- hii ipo sehemu nyingi tu duniani! Muungano hawawezi kujitoa eti Mishahara ya Madaktari sii swala la Muungano- halafu ndo hao madaktari wakimbilie Bara wote? sasa nini maana ya mantiki ya Muungano?

4. Mtu wa Pwani naafikiana na wewe- Muungano intervention ktk uchumi na mishahara Visiwani- is responsibility of Muungano- not favour- maanake Visiwani ni sehemu ya Muungano.

Naamini haya yote Nahodha na Lowassa wnaweza kujadili!

Nani aliyetelekeza zao za karafuu kufikia mahali lilipo sasa? Tusitafute mchawi.

Katika federation kuna sehemu ya mambo ya muungano na yale yasiyo. Mishahara katika sekta ambazo si za Muungano zisiingizwe katika mambo ya Muungano.

Leo tunazungumzia hili je hapo Zanziba itakapopata mafuta na uwezo wake kuongezeka mara dufu, serikali ya Muungano iilazimishe SMZ kuwalipa wafanyakazi wa bara mishahara inayolingana na kwao? kuwa pamoja katika muungano hakuondoshi ushindani baina ya nchi husika.

Nionavyo mimi, kama hii sekta imeonekana ina unyeti na umuhimu wa pekee basi iingizwe katika sekta za Muungano. Tusiendekeze hii tabia ya Changu changu, chak chetu!
 
Back
Top Bottom