Mishahara kwa watumishi hewa:nani wa kuwajibishwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mishahara kwa watumishi hewa:nani wa kuwajibishwa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mpigaji, Jan 18, 2012.

 1. M

  Mpigaji JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2012
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mara kwa mara tumekuwa tukisikia kuwa serikali imepata hasara ya Mabilioni ya Shilingi kwa kulipa mishahara kwa watumishi ambao aidha wameacha kazi,wamestaafu au wamefariki.Swali la kujiuliza ni nani wa kuwajibishwa katika hili?Wizara ya Utumishi,Hazina au Wakuu wa Idara katika Halmashauri,Wizara na Wakala za Serikali?Mfano,mtumishi ameacha kazi katika idara fulani katika halmashauri,mkuu wa idara anapeleka taarifa kwa mamlaka husika,lakini mshahara unaendelea kulipwa kwa miaka kadhaa!Nani wa kuwajibishwa katika hili?
   
 2. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mshahara kuendelea kutolewa na Hazina baada ya kupokea taarifa ya mtumishi kufa, kufukuzwa/kuacha/kuachishwa kazi ni uzembe. Hata hivyo bado mwajiri anapaswa kuzuia mshahara huo na kuukatia ERV na kisha kuuhifadhi kwenye deposits account. Tatizo la baadhi ya waajiri na wakuu wa idara ni kuwa wanakula pesa hizo ama zikiwa kama unclaimed salaries au kupitia utambulisho wa mtumishi husika (aliyekufa/kuacha kazi/kuachishwa/kufukuzwa)...hapo ndipo makosa yanapojitokeza. Huo ni wizi na wanaohusika wanapaswa kuwajibishwa.
   
 3. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  we mzee unajua nafasi za wakuu wa idara ktk halmashauri au unaongea tu mambo bila kujua issues? Mishahara huwa inatafunwa hazina inaporudishwa. Utoh analijua sana hilo sema tu wao hazina wana li-entertain hilo coz ni wao ndiyo wanaofaidika pindi hela zinaporejeshwa na halmashauri ni jumla tumboni mwao. Si unajua serikalini inaporudisha hela, kila mtu anakushangaa. Huwa wanazila na kwa kuwa wao ndo wanaozipeleka huko halmashauri zikirudishwa wanajua nini cha kuzifanyia.
   
Loading...