Mishahara imekatwa: Poleni Watumishi watia nia

Mao Tanzania

JF-Expert Member
Nov 23, 2018
210
231
Pitapita zangu hapa jijini Mwanza zimenikutanisha na watumishi wa umma wenye huzuni, chuki, hasira na kisasi mioyoni baada ya mishahara yao kukatwa kwa sababu walitia nia.

Wanasema, mishahara yao ndo uhai wa familia zao, ndiyo uzima wa Babu na Bibi zao vijijini. Wanasema wanawagonjwa wanaowategemea.

Wako walioomba ruhusa kwa mujibu wa waraka. Wako waliokuwa likizo za kawaida za mwaka.

Wamerudi makazini, walikipenda Chama cha Mpainduzi, wakavaa nguo za kijani, wakaamuka na CCM OYEEE, NG'ARA CCM ng'ara CCM na mengine kadhaa.

Wafanyakazi wanalia, wanasikitika kwanini imekuwa hivi. Wanaona hata yanayoitwa majonzi ya kitaifa ni majonzi yao wao huku na si ya kila mtu.

Taifa kinahitaji uponyaji

Cc: Katibu Mkuu Utumishi
 
No huzuni kubwa Sana . Wengine waliingia kwenye dozi ya kula mayai mabichi ya kienyeji ili wapate sauti nyororo ya kuimbia nyimbo za chama, ona Sasa wamepata kura yai la mbuni.
Halafu hapo walikuwa wameuza resources za familia ili kuhonga wajumbe.
Mweee mweee mweee wanatia huruma bhagwitu
 
Ile sheria nimeisoma. Ni sheria ukiangalia kwa makini utagundua ilitungwa kuzuia flow ya wafanyakazi kukimbilia siasa. Ubaya wa sheria nikwamba inawanyima haki wafanyakazi ya kushiriki kuchaguliwa kwenye siasa. Ni sheria ya kibaguzi flani.

Upande mwingine ,wahanga walijua kitachofuata wasimlaumu mtu. Ni mpaka sheria ibadilishwe
 
Usiichonganishe Serikali Na Wananchi Wake
Chama Dola, Ccm Hoyee, Ng'ara Magufuli Ng'ara!!
Tumeipenda Wenyewe Wala Hatukuandikiwa Barua Acha Ituue!!😀😁😂😅😄😃😃
 
Nilitia Nia... Nikaomba ruhusa....

Nimelipwa mshahara..

Tuache upumbavu wA kupakinishana.
Mkuu acha ulaghai kama ndivyo umependelewa tu na sheria kwako hsikupita. Kunasheria inasema mtia nia hutakiwi kulipwa salary
 
Back
Top Bottom