Mishahara hewa,wizi bandarini,ufisadi! Mbona hawa watuhumiwa serikali haiwafungi?

projectman

JF-Expert Member
Sep 8, 2015
349
484
Kama nilivyoelezea kichwa cha habari hapo juu!

Tumesikia watumishi hewa na tuhuma mbalimbali! watu wakitumbuliwa majipu kwa ufisadi,wizi na dhuluma mbalimbali dhidi ya ubadhirifu wa fedha za serikali.

Hawa wanaopatikana na majipu ya wizi wa mali za umma mbona hatuoni hatua za kimahakama na sheria zikiwashitaki watuhumiwa hawa ili wawajibike au kufungwa kama sheria inavyosema?

Je, hawa ni wakina nani na kila mmoja alihusika na nani na waliiba shilingi ngapi?

Au ndio business as usual! kuchezeana akili.

Kwani mahakama na magereza ni kwa wakina nani?

Kwa kweli kwa hili suala bado tunahitaji kulijua zaidi suala hili maana haiwezekani mwizi wa kuku anafungwa miaka kazaa lakini mwizi wa bilioni moja au mbili na zaidi anaachiwa huru! hivi kuna kuku wangapi katika bilioni 1.

Tunataka kuona watuhumiwa wanajazana huko mahakamani na gerezani kama sheria inavyosema.

Naomba kuwasilisha.
 
Kwani hujui siku zote serikali hushindwa kesi dhidi ya wenye pesa. Bora wafukuzwe tu isije kuwa hasara juu ya hasara. Ofisi ya DPP itumbuliwe kwanza ndo majizi yaanze kushtakiwa.
 
Back
Top Bottom