Misenyi,Kagera: Gari la Tanroads lapata ajali na kuua wafanyakazi watatu

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,816
35,804
Huu mlolongo wa ajali wenye kuhusisha magari ya serikali (STJ, STK, STL, PT, nk) kama hoja za msingi hazitasikilizwa safari ya kupunguza ajali barabarani itakuwa bado mbali sana.

Kinachogomba ni kuwa magari haya kwa kutozingatia vibao barabarani na wengine sisi tusiokuwamo kwenye magari yenu mwatuweka hatarini.

----------
Miili ya wafanyakazi watatu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Kagera waliofariki baada ya gari lao kuteketea kwa moto jana Jumanne Oktoba 23, 2018 imetambuliwa.

Ajali hiyo ilitokea wilayani Missenyi mkoani humo na miili ya wafanyakazi hao waliokuwa wameajiriwa kama vibarua kuharibika na kushindwa kutambulika haraka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi amewataja waliofariki kuwa ni David Dickson (25), Pavin Ibrahim (28)na Hamad Abdu (25) wote wakazi wa Bukoba.

Amesema majeruhi sita waliokuwa katika gari hilo wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Kagera huku baadhi yao wakiwa na majeraha makubwa ya moto.

Ajali hiyo iliyotokea kijiji cha Mushasha amesema ni baada ya gari la Tanroads kupoteza uelekeo baada ya kugongana na gari lililokuwa linakwenda Mutukula na kuanguka kwenye moto uliokuwa unawaka kwenye mbuga.

Kamanda Malimi amesema gari kubwa lilikuwa linaendeshwa na Patrick Yalala mkazi wa Bukavu nchini DRC Congo na gari la Tanroads lilikuwa linaendeshwa na Greyson Rwegasira likitokea Kyaka.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Nelson Lumbeli amesema majeruhi watano wanaendelea vizuri isipokuwa Leah Mussa ambaye ameungua sehemu kubwa ya mwili wake.

Chanzo: Mwananchi
 
Wamewatoa madereva wenye ujuzi na uzoefu wa muda mrefu,wameingia watoto wasiojua hata ethics za udereva hawajui,wacha Wafu watafunane wenyewe
 
Wamewatoa madereva wenye ujuzi na uzoefu wa muda mrefu,wameingia watoto wasiojua hata ethics za udereva hawajui,wacha Wafu watafunane wenyewe

Mkuu kinachogomba tunatafunwa na sisi kina yakhe tusiokuwamo kwenye magari yao (ambayo aghalabu logically yalikuwa ni Mali yetu aka umma).
 
Back
Top Bottom