Misemo na Maneno ya zamani

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
11,513
11,276
Wanajamii tujikumbushe baadhi ya misemo ambayo zamani ilikuwa kwenye chati na sasa haitumiki tena..

Kwa mfano nakumbuka misemo kama kuachwa kwenye mataa, Viatu vya Ndula, lakuchumpa n.k, Pia nakumbuka majina kama Chekibobu.

Karibuni.
 
Laizoni
kokoko
Baba kabwela
Mama chanja
Kuzunguka mbuyu
Amepigwa Ngwala
 
Wanajamii tujikumbushe baadhi ya misemo ambayo zamani ilikuwa kwenye chati na sasa haitumiki tena..

Kwa mfano nakumbuka misemo kama Viatu vya Ndula,

Karibuni.
Ndula ni kiatu moja kwa moja... sio viatu vya ndula
 
Mzula,
Ameupigia ugoko,
Shwaini,
Njagu,
Utabana ngenge,
Shati la Ngwabi na suruali ya pekozi....
 
Kijeba
Kingwangwa
Ndata = polisi
Mbwa (safari buti)
Mkwanja = pesa
Nishai = sio nzuri
Kapigwa mtama
Acha kushangaa ...Kashangae posta/feri nyumba zinaelea baharini
kashangae makaburini watu wanapandwa lakini hawaoti
Sema wee kuku nikisema mimi Bata utasema ninaharisha
Sema wee kiazi nikisema mimi mhogo utasema nina mizizi

Hivi ule ugonjwa wa utangoutango bado upo?
 
Last edited:
Mtasha mmoja kwenye party wa wabongo aliwahi kuacha watu hoi alipoulizwa kinywaji anachotumia akajibu KIPAPLIPAPLI.
 
Last edited:
Naenda Railway station, kupanda gogo.
Tina buu...
Kuku kwa mrija,
Paja la kuku,
Fatuma,
Utachekea cho....,
 
Hapendwi mtu...pochi
Kapanda pipa kaenda mtoni
Mlami
Mdosi
Mnuso
Gangwe
Mkora
Kipusa
Naizi
Naizesheni
 
'Katambuga'
'Kishitobe'
'Pensi-nyanya'
'Raba mtoni'
'Shangingi'
 
Back
Top Bottom